Jaji Francis Mutungi atangaza kuzuia Mikutano na Makongamano ya Vyama vya Siasa kwa muda kutafuta suluhu

Chama kongwe dola cha CCM inahusika pia na katazo hili la msajili wa vyama vingi? Kwa maana CCM nacho kisitishe shughuli za kisiasa mpaka jeshi la polisi litoe tamko.

Je ni rasmi jeshi la usalama kwa maana ya Polisi sasa limechukua hatamu, na kusitisha (suspend) katiba ya nchi inayohusu siasa mpaka litakapotoa mwongozo?

Je nchi ya Tanzania sasa inatawaliwa kijeshi na siyo kwa kufuata katiba na sheria zilizotungwa na kupitishwa na Bunge?
Kwani katiba inasema Polisi ndio wanatoa ruhusa watu kujadili mambo yao ya kitaifa??

ccm wamefika mwisho sasa🤣🤣
 
Msajili wa milele wa vyama vya siasa Tanzania , Francis Mutungi amekubali kutumika hadharani na ccm baada ya kutoa Tangazo la kukataza makongamano ya vyama vya siasa , kwa maelezo kwamba wanasiasa wasubiri kwanza kikao na IGP katika tarehe isiyojulikana .

Kwa wasiojua katiba ya nchi , Francis Mutungi kama mtu binafsi au kama Msajili wa vyama vya siasa HANA , HAJAWAHI KUWA NA HATOKUJA KUWA NA MAMLAKA YA KUZUIA MIKUTANO YA KISIASA WALA MAKONGAMANO , hili si jukumu lake

----
View attachment 1926218
PICHA: Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi, amevitaka vyama vya siasa nchini kusimamisha makongamano na mikutano ya kisiasa kwa muda ili kupisha mazungumzo baina ya vyama vya Siasa, Polisi na Ofisi ya Msajili ili kutafuta suluhu ya mikutano na makongamano.

Jaji Mutungi ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam na kwamba katika kipindi hiki cha kuelekea mazungumzo hayo ni vyema vyama vikasitisha makongamano na mikutano ya kisiasa mpaka hapo mazungumzo yatakapo fanyika ili kuondoa sintofahamu iliyoibuka baada ya polisi kudaiwa kuingilia mikutano ya kisiasa.

Hatua hiyo imekuja baada ya siku za hivi karibuni Chama cha NCCR- Mageuzi kilinukuliwa kikilalamikia kuzuiwa na Jeshi la Polisi kufanya mkutano wa Kamati Kuu katika eneo la Msimbazi baada ya Polisi hao kuvamia mkutano huo.

PIA SOMA
1. Polisi wasambaratisha kikao cha Kamati Kuu ya NCCR-Mageuzi
2. ACT Wazalendo: Tunalaani vikali kitendo cha Jeshi la Polisi kuvamia na kuzuia Kikao cha Kamati Kuu ya NCCR Mageuzi
3. Kyela: Polisi wazuia kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Chadema
4. Musoma: Polisi Wazingira ofisi ya CHADEMA kulikopangwa kufanyika kongamano la Katiba Mpya
As long as Mutungi haja cite sheria yoyote inayokataza mikutano na makongamano, status quo inasimama.

So.... vyama viendelee na shughuli zao kama kawaida hadi pale sheria ya kuzuia mikutano na makongamano itakapokuwa enacted.

Nakaribisha maswali kama yapo!
 
Mbona ukimwi upo hamjasimamisha kukimbiza mwenge
Unaweza kufananisha effects za COVID na UKIMWI in short term basis? UKIMWI umeshawahi kusababisha mipaka ya nchi zote duniani kufungwa? Acha hizo mkuu! Hii COVID inatesa watu, imeharibu uchumi!! Unajua ni watu wangapi wamefungiwa katika nchi siyo zao hapa duniani since February mwaka jana?
 
Ila tunaishukuru Corona kutuondolea dhalim mwendazake
Ndiomaana sasahivi mnapumua,
Kodi mmeshushiwa,
Magaidi wamekamatwa,
Democrasia kila kona,

Mataga na sukuma gang wanakiona cha moto.

Kumbe yule dahalimu akikuwa analea hadi magaidi
 
Bunge lipitie upya sheria ya uanzishwaji wa vyama vya siasa,ikiwezekana wavifute visiwepo kwa kuwa uwepo wake kwa sasa hauna nguvu ya kupinga vile wafanyiwavyo na msajili wao.
Uhuru wa kutoa maoni/kukusanyika pamoja/vikao vya ndani kwa mujibu wa katiba za vyama husika unapozuiliwa unaondoa dhima ya uanzishwaji wa Taasisi nzima ya Msajili wa Vyama vya siasa.
Msajili anaposhindwa kusimamia majukumu yake na badala yake kulitupia mzigo Jeshi la Polisi huko ni kulichonganisha Jeshi letu na Wananchi.
Huu unaitwa 'mchanganyiko maalumu' au 'anything can go'. Hata mimi niko interested kujua ni kifungu au vifungu gani vya sheria vinampa hayo mamlaka na anaweza kufanya hivyo kwa miezi au miaka mingapi ndipo aruhusu tena! Haya mambo tukiyaacha tu yaende kwa namna hii tutajikuta sheria zetu hazina maana tena.
 
Msajili wa milele wa vyama vya siasa Tanzania , Francis Mutungi amekubali kutumika hadharani na ccm baada ya kutoa Tangazo la kukataza makongamano ya vyama vya siasa , kwa maelezo kwamba wanasiasa wasubiri kwanza kikao na IGP katika tarehe isiyojulikana .

Kwa wasiojua katiba ya nchi , Francis Mutungi kama mtu binafsi au kama Msajili wa vyama vya siasa HANA , HAJAWAHI KUWA NA HATOKUJA KUWA NA MAMLAKA YA KUZUIA MIKUTANO YA KISIASA WALA MAKONGAMANO , hili si jukumu lake

----
View attachment 1926218
PICHA: Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi, amevitaka vyama vya siasa nchini kusimamisha makongamano na mikutano ya kisiasa kwa muda ili kupisha mazungumzo baina ya vyama vya Siasa, Polisi na Ofisi ya Msajili ili kutafuta suluhu ya mikutano na makongamano.

Jaji Mutungi ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam na kwamba katika kipindi hiki cha kuelekea mazungumzo hayo ni vyema vyama vikasitisha makongamano na mikutano ya kisiasa mpaka hapo mazungumzo yatakapo fanyika ili kuondoa sintofahamu iliyoibuka baada ya polisi kudaiwa kuingilia mikutano ya kisiasa.

Hatua hiyo imekuja baada ya siku za hivi karibuni Chama cha NCCR- Mageuzi kilinukuliwa kikilalamikia kuzuiwa na Jeshi la Polisi kufanya mkutano wa Kamati Kuu katika eneo la Msimbazi baada ya Polisi hao kuvamia mkutano huo.

PIA SOMA
1. Polisi wasambaratisha kikao cha Kamati Kuu ya NCCR-Mageuzi
2. ACT Wazalendo: Tunalaani vikali kitendo cha Jeshi la Polisi kuvamia na kuzuia Kikao cha Kamati Kuu ya NCCR Mageuzi
3. Kyela: Polisi wazuia kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Chadema
4. Musoma: Polisi Wazingira ofisi ya CHADEMA kulikopangwa kufanyika kongamano la Katiba Mpya
Tulipofika ni pabaya zaidi kuliko wakati wowote. Anatafuta suluhu gani, na nani juu ya uvunjaji wa katiba aliyoshindwa kabisa kuuzuia?
 
Baada ya kuzuia hiyo mikutano na makongamano tuitafute Suluhu mpaka 2025 naamini itakuwa haijapatikana 🤣🤸🐒
 
I met him in person alipokuwa administrator wa mahakama pale kwenye ofisi zao karibu na Kempinsky. I saw a gentleman. Ila alipokwenda huko kwenye usajili, niliona mtu tofauti kabisa
wakiendaga huko ubongo huwa wanamkabidhi mwenyekiti wa chama cha kijani afu wao wanabaki vichwa-nazi.
 
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi, amevitaka vyama vya siasa nchini kusimamisha makongamano na mikutano ya kisiasa kwa muda ili kupisha mazungumzo baina ya vyama vya Siasa, Polisi na Ofisi ya Msajili ili kutafuta suluhu ya mikutano na makongamano.

Jaji Mutungi ameeleza kushtushwa na kitendo cha polisi kujazana na mabomu katika kila mkutano wa chama cha siasa nchini jambo linaloleta taswira hasi kuwa hali ya kisiasa nchini angeifuta tu chadema inawateaa sana na wanakoaa usingizi sioni mahusiano ya kikao.cha igp naa makongamano yanayofanyakia wilayani
 
Huyo ni mhuni mwingine anayetumika na hii Serikali haramu kuminya haki za Watanzania na vyama vya siasa nchini.
Msajili wa milele wa vyama vya siasa Tanzania , Francis Mutungi amekubali kutumika hadharani na ccm baada ya kutoa Tangazo la kukataza makongamano ya vyama vya siasa , kwa maelezo kwamba wanasiasa wasubiri kwanza kikao na IGP katika tarehe isiyojulikana .

Kwa wasiojua katiba ya nchi , Francis Mutungi kama mtu binafsi au kama Msajili wa vyama vya siasa HANA , HAJAWAHI KUWA NA HATOKUJA KUWA NA MAMLAKA YA KUZUIA MIKUTANO YA KISIASA WALA MAKONGAMANO , hili si jukumu lake

----
View attachment 1926218
PICHA: Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi, amevitaka vyama vya siasa nchini kusimamisha makongamano na mikutano ya kisiasa kwa muda ili kupisha mazungumzo baina ya vyama vya Siasa, Polisi na Ofisi ya Msajili ili kutafuta suluhu ya mikutano na makongamano.

Jaji Mutungi ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam na kwamba katika kipindi hiki cha kuelekea mazungumzo hayo ni vyema vyama vikasitisha makongamano na mikutano ya kisiasa mpaka hapo mazungumzo yatakapo fanyika ili kuondoa sintofahamu iliyoibuka baada ya polisi kudaiwa kuingilia mikutano ya kisiasa.

Hatua hiyo imekuja baada ya siku za hivi karibuni Chama cha NCCR- Mageuzi kilinukuliwa kikilalamikia kuzuiwa na Jeshi la Polisi kufanya mkutano wa Kamati Kuu katika eneo la Msimbazi baada ya Polisi hao kuvamia mkutano huo.

PIA SOMA
1. Polisi wasambaratisha kikao cha Kamati Kuu ya NCCR-Mageuzi
2. ACT Wazalendo: Tunalaani vikali kitendo cha Jeshi la Polisi kuvamia na kuzuia Kikao cha Kamati Kuu ya NCCR Mageuzi
3. Kyela: Polisi wazuia kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Chadema
4. Musoma: Polisi Wazingira ofisi ya CHADEMA kulikopangwa kufanyika kongamano la Katiba Mpya
 
Tunajenga uchumi kwanza kwa sasa, kipindi hiki kigumu ambapo uchumi wa dunia nzima umeshuka! Hivi saa hizi uene nchi kama India au USA uwaambie kipaumbele chako ni katiba mpya si watakuona chizi!!

Dunia nzima inahangaika inajikomboa vipi na hili janga nyie mnataka kipaumbele cha taifa kiwe katiba mpya! Kila jambo litafanyika, ila kwa wakati muafaka, muwe mnajua kusoma alama za nyakati na kubadilika
Kudai katiba mpya kuna zuia vp maendeleo Mwrhu wewe? Kila mtu anajua jukumu lake. Mkulima anaendelea na kulima. Mfanya biashara anaendelea na biashara zake, hali kadhali mfanyakazi.
Waachwe wanasiasa nao wafanye majukumu yao.
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom