Jaji Francis Mutungi atangaza kuzuia Mikutano na Makongamano ya Vyama vya Siasa kwa muda kutafuta suluhu

Msajili wa milele wa vyama vya siasa Tanzania,

Francis Mutungi amekubali kutumika hadharani na CCM baada ya kutoa Tangazo la kukataza makongamano ya vyama vya siasa , kwa maelezo kwamba wanasiasa wasubiri kwanza kikao na IGP katika tarehe isiyojulikana.

Kwa wasiojua katiba ya nchi, Francis Mutungi kama mtu binafsi au kama Msajili wa vyama vya siasa HANA, HAJAWAHI KUWA NA HATOKUJA KUWA NA MAMLAKA YA KUZUIA MIKUTANO YA KISIASA WALA MAKONGAMANO, hili si jukumu lake

----
View attachment 1926218
PICHA: Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi, amevitaka vyama vya siasa nchini kusimamisha makongamano na mikutano ya kisiasa kwa muda ili kupisha mazungumzo baina ya vyama vya Siasa, Polisi na Ofisi ya Msajili ili kutafuta suluhu ya mikutano na makongamano.

Jaji Mutungi ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam na kwamba katika kipindi hiki cha kuelekea mazungumzo hayo ni vyema vyama vikasitisha makongamano na mikutano ya kisiasa mpaka hapo mazungumzo yatakapo fanyika ili kuondoa sintofahamu iliyoibuka baada ya polisi kudaiwa kuingilia mikutano ya kisiasa.

Hatua hiyo imekuja baada ya siku za hivi karibuni Chama cha NCCR- Mageuzi kilinukuliwa kikilalamikia kuzuiwa na Jeshi la Polisi kufanya mkutano wa Kamati Kuu katika eneo la Msimbazi baada ya Polisi hao kuvamia mkutano huo.

PIA SOMA
1. Polisi wasambaratisha kikao cha Kamati Kuu ya NCCR-Mageuzi
2. ACT Wazalendo: Tunalaani vikali kitendo cha Jeshi la Polisi kuvamia na kuzuia Kikao cha Kamati Kuu ya NCCR Mageuzi
3. Kyela: Polisi wazuia kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Chadema
4. Musoma: Polisi Wazingira ofisi ya CHADEMA kulikopangwa kufanyika kongamano la Katiba Mpya
Anatangaza kama Msajili, au KWa katiba hipi? mh Jaji mtungi akafute vyama vya kisiasa, ujinga tu , yeye ni nani FANYA kile anakifanya ,hata mwendazake hakufanya hivi pamoja na udikiteta uchwara ,je Hawa wataweza?????????
 
Kwisha habari yako !
Achana na huo msukule. Kuandika matusi Ni ushahidi kwamba muandishi Ni mtu 'uncouth' tafsiri rahisi Ni chokoraa ambaye hakulelewa na responsible parents.
Akili ya watu Hawa Ni Kama utumbo wa nguruwe.
 
Msajili ndio mlezi wa vyama vya siasa hivyo hana budi kutoa muongozo kwa watoto wake jinsi ya kuishi na kuvumiliana ktk ulimwengu huu wa siasa.
 
Msajili wa vyama vya siasa kama angelikuwa hatumiki na CCM kisiasa angelisema "Tanzania sio dola la kipolisi" na amtake IGP awaeleze askari wake wasiingilie shughuli za vyama vya siasa kwa kuwa shughuli hizo zipo kwa mujibu wa katiba na sheria.

Wewe uliona wapi haki za kikatiba zikijadiliwa jinsi ya kutekelezwa? Ni uhuni mtupu!IGP kazi yake ni kulinda utekelezaji wa sheria za nchi na wala siyo kukaa meza moja na wahalifu na kufanya nao maridhiano.

Kama vyama vya siasa vinavunja katiba na sheria kwa kufanya vikao vya ndani pamoja na makongamano si avichukulie hatua za kisheria?Kama vyama vya siasa vinavunja katiba na sheria kwa kufanya vikao vya ndani pamoja na makongamano ya katiba inakuwaje IGP atake kukaa meza moja na wahalifu wanaovunja sheria za nchi?
 
Mleta uzi bila shaka umesahau..mwaka 2018 Bunge lilipitisha sheria kwa hati ya dhalura ya vyama vingi vya Siasa..sheria hiyo imempa mamlaka msajili ya kufanya alichokisema,imempa kinga dhidi ya kushitakiwa nk..Sheria hiyo ilipitishwa na JPM alitia sahihi
 
Hawa ndio wa kula nao sahani moja,hawa ndio wanaotekeleza maagizo kutoka juu,hawa ndio vitimbakwiri wanaoivuruga Tanzania.

Je, ni kweli wanapata maelezo kutoka juu au ni wale wanaojipitisha na kujipendekeza ,
Ni bora aje Hamza mwingine atusaidie kuliondoa hili dudu. Kilangila.
 
Msajili wa milele wa vyama vya siasa Tanzania,

Francis Mutungi amekubali kutumika hadharani na CCM baada ya kutoa Tangazo la kukataza makongamano ya vyama vya siasa , kwa maelezo kwamba wanasiasa wasubiri kwanza kikao na IGP katika tarehe isiyojulikana
Je ametumia kifungu gani cha sheria kutoa mapendekezo hayo ?
 
Tunajenga uchumi kwanza kwa sasa, kipindi hiki kigumu ambapo uchumi wa dunia nzima umeshuka! Hivi saa hizi uene nchi kama India au USA uwaambie kipaumbele chako ni katiba mpya si watakuona chizi!!

Dunia nzima inahangaika inajikomboa vipi na hili janga nyie mnataka kipaumbele cha taifa kiwe katiba mpya! Kila jambo litafanyika, ila kwa wakati muafaka, muwe mnajua kusoma alama za nyakati na kubadilika
Umeishia darasa la pili au la saba kama babu tale?
 
Tunajenga uchumi kwanza kwa sasa, kipindi hiki kigumu ambapo uchumi wa dunia nzima umeshuka! Hivi saa hizi uene nchi kama India au USA uwaambie kipaumbele chako ni katiba mpya si watakuona chizi!...
Japo pengine pia unaweza usijue jinsi ambavyo katiba mbovu au isiyofuatwa inavyoweza kudidimiza uchumi na maendeo ya nchi.
 
Japo pengine pia unaweza usijue jinsi ambavyo katiba mbovu au isiyofuatwa inavyoweza kudidimiza uchumi na maendeo ya nchi.
Mbona mother aliongea vizuri sana, alisema katiba ni muhimu ila kwa sasa siyo wakati muafaka wa kuanzisha mavuguvugu ya malumbano, tusubiri!! Sasa hapo alikosea kitu gani? Wananchi tukamwelewa, ila wanasiasa ambao wanataka kutumia kivuli cha katiba kushibisha matumbo yao wakaanza "chokochoko", sasa "wamechokonolewa" hawana hata pa kukimbilia.

Mkuu the world is fck up now with this Covid issues, Mimi sipo huko, huku nilipo ndio naona jinsi gani Covid imeathiri watu, kila siku unasikia serikali ya US inatoa trilions kuwapa wananchi wao wajikimu, Mabunge mengi duniani Mijadala ya Covid tu ndiyo inaendelea, In the midst of that wewe unataka uanzishe mchakato wa katiba mpya? nani atakuelewa?

Hii pressure unayoiona mzee ni njaa ya hawa wapinzani baada ya JPM kuwafanya alichowafanya, walitegemea kupitia katiba angalau wangeokoteza vijisenti
 
Juzi nimemsikia MSAJILI wa Vyama vya Siasa Akiungana na Jeshi la Polisi KUVUNJA KATIBA kwa Kusitisha MIKUTANO ya Vyama vya Siasa kwa Madai kuwa Yafanyike MARIDHIANO baina ya Vyama Jeshi la Polisi na Msajili.

Binafsi NAPINGA MARIDHIANO hayo kwa Sababu Kwanini kuwe na MARIDHIANO wakati Suala la Vyama kufanya Mikutano lipo KIKATIBA wala halihitaji Msajili au Jeshi la POLISI LITAKE.

Kinachotakiwa kufanyika ni MSAJILI wa Vyama kutimiza Wajibu wake kwa KUTII KATIBA.

JESHI la Polisi litimize Majukumu yake kuhusu Kulinda Mikutano ya Vyama na sio KUZUIA kwa Mujibu wa KATIBA.

Vyama vya Siasa vifanye Mikutano yao kwa Mujibu wa KATIBA.

Tusipoteze Muda kwa kufanya MATIDHIANO yasio na TIJA

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom