Jaji Francis Mutungi atangaza kuzuia Mikutano na Makongamano ya Vyama vya Siasa kwa muda kutafuta suluhu

Kipaumbele cha dunia nzima sasa hivi ni kuangalia jinsi gani tunavuka kwenye mkwamo wa kiuchumi uliojitokeza, mambo hayaendi! Wewe kwa sababu upo huko Litapwasi unakula mihogo usidhani wote wanaishi kama wewe!! Nenda nchi yeyote saa hii duniani uwaambie mimi kipaumbele changu katiba mpya, utaonekana ni kichaa na jinga! Watu wamefunga makampuni, kuna nchi zimesitisha hadi uchaguzi mkuu, Corona imeondoa watu madarakani, millions of money zimepotea kwenye kada mbalimbali zimepotea na zinaendelea kupotea sababu ya Corona, hapa kwetu tumepoteza billions kupitia utalii na mambo mengine na bado tunaendelea kupoteza, watu wametengana na familia zao unaenda mwaka wa pili huu, watu wamepoteza kazi!! Halafu wewe na ujuha wako ulete story za katiba mpya......!! Lazima uvunjwe kiuno
Utetezi wakitoto na kijuha sana.Uwezo wenu umeshaisha ilo liko wazi kwakila mwenye akili timamu.bado kukata roho tu.Hizo hoja unazozitoa hazileti maana kwenye nchi yenye umri wa mtu mzima na bado hali ni hii tuliyonayo.
 
Hua ujaji wanaupataje? kwani katiba inasemaje kuhusiana na maswala la vyama vya siasa kujiusisha na mambo ya siasa?
 
Msajili wa milele wa vyama vya siasa Tanzania,

Francis Mutungi amekubali kutumika hadharani na CCM baada ya kutoa Tangazo la kukataza makongamano ya vyama vya siasa , kwa maelezo kwamba wanasiasa wasubiri kwanza kikao na IGP katika tarehe isiyojulikana.

Kwa wasiojua katiba ya nchi, Francis Mutungi kama mtu binafsi au kama Msajili wa vyama vya siasa HANA, HAJAWAHI KUWA NA HATOKUJA KUWA NA MAMLAKA YA KUZUIA MIKUTANO YA KISIASA WALA MAKONGAMANO, hili si jukumu lake

----
View attachment 1926218
PICHA: Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi, amevitaka vyama vya siasa nchini kusimamisha makongamano na mikutano ya kisiasa kwa muda ili kupisha mazungumzo baina ya vyama vya Siasa, Polisi na Ofisi ya Msajili ili kutafuta suluhu ya mikutano na makongamano.

Jaji Mutungi ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam na kwamba katika kipindi hiki cha kuelekea mazungumzo hayo ni vyema vyama vikasitisha makongamano na mikutano ya kisiasa mpaka hapo mazungumzo yatakapo fanyika ili kuondoa sintofahamu iliyoibuka baada ya polisi kudaiwa kuingilia mikutano ya kisiasa.

Hatua hiyo imekuja baada ya siku za hivi karibuni Chama cha NCCR- Mageuzi kilinukuliwa kikilalamikia kuzuiwa na Jeshi la Polisi kufanya mkutano wa Kamati Kuu katika eneo la Msimbazi baada ya Polisi hao kuvamia mkutano huo.

PIA SOMA
1. Polisi wasambaratisha kikao cha Kamati Kuu ya NCCR-Mageuzi
2. ACT Wazalendo: Tunalaani vikali kitendo cha Jeshi la Polisi kuvamia na kuzuia Kikao cha Kamati Kuu ya NCCR Mageuzi
3. Kyela: Polisi wazuia kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Chadema
4. Musoma: Polisi Wazingira ofisi ya CHADEMA kulikopangwa kufanyika kongamano la Katiba Mpya
Hii nchi mbona imeshakuwa lawless,msajili hana mamlaka ya kukataza mikutano!

Are we turning into gangstar republic! Really? Haujulikani kama kuna Rais au muigizaji wa filam
 
CCM maji ya shingo wameona kila siku watu wanaandaa makongamano bila kikomo hata PoliCCM wamechoka kuzuia, IGP ameomba poo!
 
Tunamuunga mkono maana atatufikisha tunapohitaji kufika, ila sina uhakika kama atazuia ya ccm, labda ya vyama pinzani
CCM ilishajifia hata ikifanya mikutano yake mwaka mzima Haina madhara kwa upinzani.Wananchi wanajua wanataka nini!
 
Mimi kwa hili nitamuunga mkono kama kweli atalitafutia muafaka, lakini kama atakaa kimya basi nitafahamu kwamba anatumika.
Ebu tumpe muda kidogo ili tujue kama kweli atalitafutia muafaka.
Angekuwa nadhamira njema na yadhati,asingeacha hali iliyopokuchukua muda wote, Bila kukemea uonevu namanyanyaso ya wazi kwa wapinzani ila kile kingine kupewa haki zote bila kisingizio chochote.
 
Hapa kinachofanyika ni kujaribu kubadilisha picha inayoendelea ya vyombo vya usalama kuzuia kwa nguvu mikutano halali ya vyama vya siasa. Picha za magari na polisi kuzingira ofisi za vyama vya siasa, kumbi za mikutano na mpaka makanisani kweli hazipendezi, kama ambavyo Msajili alivyokiri mwenyewe. Sasa wanakuja na hii ya ahadi ya mazungumzo ambayo hayana tarehe (na ukweli ni kuwa wote tunajua matokea yake) ili lengo la kutokuwepo mijadala ya Katiba Mpya litimizwe bila kuweko na hizo picha na taarifa za watu kuwekwa mahabusu kila kukicha. Naona Zitto amekubali lakini sidhani kama walengwa watakubali. Wawaachie tuu wafanye mikutano na makongamano yao bila kuwaingilia.

Amandla...
 
Enzi za Nyerere ukisikia mtu Ni jaji muangalie Mara tatu. Maana walikua wanakaangwa na kukaangika kwenye vikaango vikaangizi vya Sheria.
Leo hii mtu akiongea kisukuma hadharani kesho utamsikia jaji.
Mtu akimhukumu mzee Rungwe asipike mchele kesho utasikia jaji.
Jaji anatanua kwenye foleni?
Jaji anakula kwa mama ntilie?
 
Hiki kijamaa chenyewe siku zote ni kutishia kuifuta CDM; hakinaga jipya.
 
Enzi za Nyerere ukisikia mtu Ni jaji muangalie Mara tatu. Maana walikua wanakaangwa na kukaangika kwenye vikaango vikaangizi vya Sheria.
Leo hii mtu akiongea kisukuma hadharani kesho utamsikia jaji.
Mtu akimhukumu mzee Rungwe asipike mchele kesho utasikia jaji.
Jaji anatanua kwenye foleni?
Jaji anakula kwa mama ntilie?
Jaji wa kwanza kumjua alikuwa Jaji Nyalali - ile Tume ya Nyalali then Jaji Warioba. Miaka hiyo ukisikia neno Jaji aisee ni balaa, mwili unakusisimka.

Sasa hivi tuna majaji maandazi wengi sana hata kuandika hukumu ni matatizo.
 
Jaji wa kwanza kumjua alikuwa Jaji Nyarali, then Jaji Warioba. Miaka hiyo ukisikia neno Jaji aisee ni balaa.

Sasa hivi tuna majaji maandazi wengi sana hata kuandika hukumu ni matatizo.
Majaji maandazi vihiyo!🤣🤣🤣
 
Msajili wa milele wa vyama vya siasa Tanzania,

Francis Mutungi amekubali kutumika hadharani na CCM baada ya kutoa Tangazo la kukataza makongamano ya vyama vya siasa , kwa maelezo kwamba wanasiasa wasubiri kwanza kikao na IGP katika tarehe isiyojulikana.

Kwa wasiojua katiba ya nchi, Francis Mutungi kama mtu binafsi au kama Msajili wa vyama vya siasa HANA, HAJAWAHI KUWA NA HATOKUJA KUWA NA MAMLAKA YA KUZUIA MIKUTANO YA KISIASA WALA MAKONGAMANO, hili si jukumu lake

----
View attachment 1926218
PICHA: Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi, amevitaka vyama vya siasa nchini kusimamisha makongamano na mikutano ya kisiasa kwa muda ili kupisha mazungumzo baina ya vyama vya Siasa, Polisi na Ofisi ya Msajili ili kutafuta suluhu ya mikutano na makongamano.

Jaji Mutungi ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam na kwamba katika kipindi hiki cha kuelekea mazungumzo hayo ni vyema vyama vikasitisha makongamano na mikutano ya kisiasa mpaka hapo mazungumzo yatakapo fanyika ili kuondoa sintofahamu iliyoibuka baada ya polisi kudaiwa kuingilia mikutano ya kisiasa.

Hatua hiyo imekuja baada ya siku za hivi karibuni Chama cha NCCR- Mageuzi kilinukuliwa kikilalamikia kuzuiwa na Jeshi la Polisi kufanya mkutano wa Kamati Kuu katika eneo la Msimbazi baada ya Polisi hao kuvamia mkutano huo.

PIA SOMA
1. Polisi wasambaratisha kikao cha Kamati Kuu ya NCCR-Mageuzi
2. ACT Wazalendo: Tunalaani vikali kitendo cha Jeshi la Polisi kuvamia na kuzuia Kikao cha Kamati Kuu ya NCCR Mageuzi
3. Kyela: Polisi wazuia kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Chadema
4. Musoma: Polisi Wazingira ofisi ya CHADEMA kulikopangwa kufanyika kongamano la Katiba Mpya
We Lofa elewa kuwa kuwa, kila haki ina wajibu, na kuna limitations, na hizo limitations zipo za aina 2 , moja ni zile Principle limitations na General limitations,
Hakuna haki ambayo haina mipaka, Principle limitations zinatoka kwenye mazuio ya sheria za nchi e.g Penal code, Economic, wildlife etc, na General ni zile zilizomo ndani ya katiba yenyewe ibara ya 30(2) sasa wahuni kama wewe wa machadema hamsomi katiba vizuri, mnapotosha wanachama wenu bure! hakuna haki isiyo na mipaka, hamuwezi kuamka asubuhi mnaamua lolote kwa kisingizio cha uhuru ovyo nyie
 
Umeokota wapi hayo uliyoyaandika ?
 
Back
Top Bottom