Jaji Elinaza Luvanda ajiondoa kuendesha kesi ya Mbowe na wenzake baada ya washtakiwa kudai hawana imani naye

Jaji asikubali upuuuzi na ushenzi huu wa Mawakili wa Mbowe na Mbowe mwenyewe.

Huko ni kumtusi Jaji na Mahakama,

Mbowe na mawakili wake hawana sababu ya msingi zaidi ya kutaka kumyumbisha Jaji, tuhuma wanazo zitoa dhidi ya Jaji ni za kipuuuzi na hazina uthibitisho wowote zaidi ya kudhania na kuhisia tu, hakuna hoja hapo, kwa hiyo anamtaka Jaji ambaye ni RAFIKI YAKE ili asikilize kesi yake.

kwa hiyo imefikia sasa Mtuhumiwa kuchagua Jaji wa kusikiliza kesi yake aisee! hata marekani hakuna kitu kama hicho.

ninacho sema Jaji angeweza kujitoa kama tuhuma zinazo tolewa na Mbowe zina uthibitisho la sivyo Jaji aendelee tu kungurumisha kesi.......asikubali kubabaishwa na hoja za kipuuzi na za kuokoteza na zenye lengo la kuchelewesha haki kutendeka.
Umefuatilia kesi lakini we boya,au unaandika tu.
 
Hakuna unachokijua ni bora ukae kimya ujifunze

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
Baada ya Jaji Luvanda kutupa mapingamizi yote yaliyotolewa na Mawakili wanaomtetea Mbowe na wenzake, Mbowe amesimama na kumtaka Jaji Luvanda ajiondoe kuendesha kesi hiyo kwani ameonyesha upendeleo na taarifa zinasema ana maelekezo ya kupindisha sheria ili amfunge Mbowe na wenzake.

Jaji Luvanda amesema hati ya mashtaka ni batili amewashauri Mawakili wa serikali wakaibadilishe, Mawakili upande wa utetezi wamegoma wamemwambia kama hati ya mashtaka ni batili basi futa kesi Jaji akakataa ila amekubali kujiondoa kuendesha kesi.

====

Jaji Elinaza Luvanda wa Mahakama Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Makosa ya Rushwa na aliyekuwa anaisikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi namba 16/2021 yenye mashtaka sita yakiwemo ya Ugaidi, amejitoa kusikikiza kesi hiyo.

Sababu ya kujitoa katika kesi hiyo ni kutokana na mshtakiwa wa nne katika kesi hiyo, Freeman Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa, kuieleza mahakama hiyo kuwa yeye na washtakiwa wenzake watatu hawana imani na Jaji huyo katika kutenda haki dhidi ya kesi yao.

Kesi imehairishwa mpaka jaji mwingine atakapopatikana. Pia awali Jaji Elinaza Benjamin Luvanda alikataa kutoa uamuzi wake leo juu ya mapingamizi ya upande wa utetetezi mpaka atapopata hansard / kumbukumbu za majadiliano ya Bunge kuhusu sheria ya ugaidi.

Wote walikubaliana kuwa kesi hii ina masilahi mapana kwa umma wote waliopo ndani ya Mahakama na nje.

Hoja 3 za upande za upande wa utetezi zilikuwa zinashambulia madhaifu na kasoro ya hati ya mashtaka. Hoja ya kwanza ilikubaliwa na jaji wakati hoja ya pili ilikubaliwa kwa nusu yake na jaji wakati hoja ya tatu ya kutupiliwa mbali au kufutwa kesi, jaji aliikataa.

Na kwa msingi huo mtuhumiwa Freeman Mbowe kwa niaba ya wenzake akasimama na kusema hawana imani na Jaji Elinaza Benjamin Luvanda kuendelea kusikiliza kesi hiyo, na mheshimiwa Jaji E.B Luvanda akaafiki ombi hilo na kujiengua kusikiliza kesi hii.

Source : Mwananchi Digital

UPDATE: Jaji Luvanda akubali
Jaji Elinaza Luvanda aliyekuwa anaisikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi nyenye mashtaka 6 yakiwemo ya ugaidi, amejitoa kusikiliza kesi hiyo, sababu ya kujitoa kwake, ni kutokana na mshtakiwa wa nne katika kesi hiyo, Mhe. Freeman Mbowe na wenzake kuwa hawana imani na Jaji huyo.

Pia soma >
Mahakama ya Uhujumu Uchumi: Mvutano mkali kesi ya Mbowe na wenzake. Hatma ya kesi kujulikana Septemba 6
. "Jaji Mwenzangu Luvanda" Machozi ya samaki majini hayatakufikia wewe na kizazi chako mpaka cha nne, tekeleza maagizo
. CHADEMA tusimpe vitisho Jaji Luvanda, mpaka sasa hajapendelea pande yoyote. Kibatala na jopo lake walichemka
Sisi Mahakama tujitafakari,maslahi yetu yapo hivi:-
1. Mshahara zaidi ya Tshs 6,000,0000/-kwa mwezi
2. Nyumba masaki
3. Gari VXR
4. Likizo nje ya nchi kila mwaka.
5. Posho ya suto kila mwezi.
6. Overtime nyingi sana.
7>Fedha za sessions , kila tunapokwenda mikoani.
8.Ukistaafu kinua mgongo zaidi ya Tshs 200 milion.
9. Kila mwezi ukistaafu unapata 4,000,000 /- milioni 4.
10. Kusomeshewa watoto.
11. Uklinzi, house boy and girl,
14. NSSF , Bima ya afya.

Hayo yote bado tu mtu haridhiki anataka kukandamiza kitoto kama Mbowe kweli, Mungu anaona mjue .
 
kumbe ndio wanafaidi keki ya Taifa kiasi hiki.
Duh!
 
Katiba imezuia mengi na kuweka ukomo lakini ina bagazwa tu ndg yangu.
Mtanzania amejaa uovu na ubatili

Tunahitaji kubadilika mno, hata tuwe katiba kama ya Marekani unafikiri yupo wa kuisimamia na kuiheshimu?
Bunge lingekuwa huru, viongozi wa kuteuliwa na nao wangekuwa wanafanya interview tungekuwa mbali sn
 
Bunge lingekuwa huru, viongozi wa kuteuliwa na nao wangekuwa wanafanya interview tungekuwa mbali sn
Ooh ukitaja bunge unaniharibia siku.
Ndugai ni pepo kabisa, ukilitaja bunge namkumbuka.
Huyu anapaswa kunyongwa hakika.
Anafuja kodi zetu bure hajui anafanya nini pale
 
Ooh ukitaja bunge unaniharibia siku.
Ndugai ni pepo kabisa, ukilitaja bunge namkumbuka.
Huyu anapaswa kunyongwa hakika.
Anafuja kodi zetu bure hajui anafanya nini pale
Ndiyo hivyo mkuu, bunge na mahakama vingekuwa huru leo tugepiga hatua kubwa sn kimaendeleo, now tunaishi kwa hisani ya Rais
 
Ndiyo hivyo mkuu, bunge na mahakama vingekuwa huru leo tugepiga hatua kubwa sn kimaendeleo, now tunaishi kwa hisani ya Rais
Hapa dawa sisi ufike wakati tujitambue.
80% ya wabongo ni vilaza totoro, ili mradi liende.
Huoni kelele tu za juzi zimemwengua Jaji?
 
Hapa dawa sisi ufike wakati tujitambue.
80% ya wabongo ni vilaza totoro, ili mradi liende.
Huoni kelele tu za juzi zimemwengua Jaji?
Lakini si Mbowe kabaki ndani? muda wake aliokaa gerezani utafidiwa na nani? hata Mandela alitolewa gerezani wakazungumza yakaisha.
 
Ni heri angeifuta na kumuachia kisha Polisi wakamkamata na kumshitaki kama pilato alivyo elekeza...
Mahakama kuu imepata ejea mbaya kwenye maktaba yake. Yaani jaji ana kiri mashtaka yamekosewa. Badala ya kufuta kesi waka jipange upya, ana sema wakaandae mashtaka upya. Kwa tafsiri nyingine ni kwamba mahakama ina didimiza haki kwa kuwa onea washtakiwa. Bora ange ifuta kesi, halafu polisi imkamate tena. Huyo jaji ange baki na heshima. Na haki inge onekana.
 
Back
Top Bottom