Vikao vimekuwa vizito vya tume ya uchaguzi kufuatia utata wa uraia wa mgombea wa CCM. Hali hiyo imeibuka kufuatia uhalisi wa kisheria kuwa SIOI hakuwa kuukana uraia wa kenya ambao aliupata kwa kuzaliwa nchini humo.
Jaji Lubuva inasemekana ameelezea mtego huo kuwa, kwa mazingira ya kawaida Wazazi wa SIOI ni watanzania hata yeye ni mtanzania lakini kisheria alitakiwa kuukana uraia wa kenya alipofika miaka 18 kwa sababu aliupata kwa kuzaliwa nnchini humo. Jambo hili watu wengi waliozaliwa nje hulisahau kabisa kwa sababu za kawaida kabisa kuwa wazazi ni watanzania na kuacha sheria kutimiza matakwa ya sheria.
Uhalisi wa suala hili kisheria ni kuwa mgombea SIOI SUMARI hakuwahi popote kuukana uraia wa kenya na kuchukua uraia wa watanzaia. Jaji lubuva ameendelea kukuna kichwa na viongozi wa ccm wameendelea kutengeneza sababu na kujaribu kutengenza viambatanisho ambavyo mpaka kufika mchana wa leo jaji lubuva hakuwa amekubaliana nao kwa vile huu ni mtihani mkubwa sana kwa Lubuva kuhusu kusimamia haki na sheria na kitendo cha kupindisha sheria katika hatua hizi za mwanzo ni kama kujifukuzisha kazi mapema.