Jaji Bomani: Wageni wanaimaliza nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji Bomani: Wageni wanaimaliza nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Dec 24, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 55,631
  Likes Received: 20,218
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Jaji Bomani: Wageni wanaimaliza nchi
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Friday, 23 December 2011 19:48
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Burhani Yakub,Tanga
  Mwananchi

  MWENYEKITI wa Tume ya Kufuatilia Kampuni za Madini Serikalini (TEITI), Jaji Marck Bomani, amesema wageni wanazidi kuimaliza nchi kupitia sekta ya madini, yakiwa ni matokeo ya sheria mbovu.

  Jaji Bomani imeishauri Serikali kubadilisha haraka sheria zilizopo kuhusu sekta hiyo ili kuwawezesha wananchi kujua kila kinachopatikana kutokana na raslimali hiyo.

  Alisema uchimbaji wa madini utaendelea kuwanufaisha wageni kwa kuhamishia fedha na madini nchi za nje na kwamba hilo linatokana sheria zilizopo kuwapa mwanya.Jaji Bomani alisema hayo jana alipokuwa akizungumza katika warsha ya uelimishaji na uhamasishaji umma juu ya taarifa ya kwanza ya ulinganisho wa malipo na mapato kutoka kampuni za uchimbaji madini na gesi asili, katika mwaka wa fedha 2008/2009 iliyofanyika jijini Tanga

  Alisema ni jambo la kushangaza kuona Tanzania pekee ikitoa mwanya kwa wawekezaaji kuchimba madini na kuyasafirisha nje kwa ajili ya kuyauza.Jaji Bomani alisema mabaya zaidi makampuni hayo yametakiwa kulipa kodi baada ya kuondoa gharama zote za uendeshaji au uzalishaji.

  "Hakuna mfanyabiashara anayeweza kusema ukweli juu ya faida ganayoipata kutokana na kuchimba madini, haiwezekani Tanzania tuendelee kuwa masikini wakati madini yetu yanayotoka yangeweza kusukuma mbele maendeleo yetu,"alisema Bomani.

  Alisema katika taarifa ya awali imebainika kuwa uchambuzi uliofanyika kuna tofauti kubwa ya taakribani zaidi ya Sh 46 bilioni kati ya malipo yaliyodaiwa kulipwa na kampuni na fedha iliyopokelewa serikalini.

  Akiwasilisha mada ya mtizamo wa wadau na jamii juu ya ripoti ya kwanza ya TEITI na matarajio ya ripoti ya pili, mjumbe wa kamati hiyo, Askofu Stephen Munga alisema unahitajika uzalendo wa hali ya juu kwa viongozi waliopewa madaraka ya kuwaongoza wananchi.

  Alisema haiwezekani rasilimali ya nchi kuendelea kuvunwa na kutoroshwa nje ya nchi kijanja na kuwanufaisha wageni huku Watanzania wakiendelea kuwa masikini na kwamba ni lazima hatua za makusudi za kuinusuru nchi
  zichukuliwe.  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Kitaja

  Kitaja JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 2,070
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  Hivi hup uhauri si ulitolewa muda mrefu sana katika ripoti ya Bomani na akina Zitto? mbona hadithi inaendelea? ina maana Rais aliunda kamati bila kuwa na utashi wa kutekeleza mapendekezo ya kamati? yangu ni hayo tu.
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,809
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  zitto alipozwa mambo yakapoa....

  kuna laana kali inaendelea na rasilimali zetu kutokana na mchwa wachache wabaya
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 55,631
  Likes Received: 20,218
  Trophy Points: 280
  Tumethubutu usanii tumeuweza sasa tunasonga mbele na usanii wetu.
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Dec 25, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 55,631
  Likes Received: 20,218
  Trophy Points: 280
 6. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #6
  Dec 25, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,847
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Rais hana utashi kabisa
   
Loading...