Jaji anasoma hukumu anamaliza, mkiomba hukumu mnaambiwa haiko tayari, how come?

Verrazanno

JF-Expert Member
Sep 15, 2021
383
781
Inakuaje hapo

Jaji au Hakimu anasoma hukumu halafu mkiomba nakala haiko tayari

Alikuwa anasoma nini?
 
Jaji anakuwa anasoma summary ya hukumu ila ile nakala kamili iliyosainiwa inakuwa bado kukamilika.

Kuandika hukumu kunahitaji uangalifu sana haswa kwa mahakama za rekodi kama Mahakama Kuu
 
  • Thanks
Reactions: cmp
Sawa na kuuziana kiwanja ila hati...

Sawa na kuomba (kupewa) mkopo ila makato baadae

Sawa na kufanya mtihani wa fom fo ila kuhitimu...

Sawa na kupewa result slip ila academic certificate baadae sana!
 
Jaji anakuwa anasoma summary ya hukumu ila ile nakala kamili iliyosainiwa inakuwa bado kukamilika.

Kuandika hukumu kunahitaji uangalifu sana haswa kwa mahakama za rekodi kama Mahakama Kuu
Punguza upimbi jombaa, nini maana ya summary? Hivi huko vichwani huwa mmejaza funza au tatizo ni nini hasa? Narudia nijibu maana ya summary halafu nitarudi...
 
Mkuu hukumu mara nyingi huandikwa kwa mkono kwenye jalada la kesi husika.

Wakati anaandika hupitia muenendo wa kesi wakati ilipoanza hadi ilipofikia, muenendo wa kesi huwepo kwenye file husika hivyo hufanya ulinganifu na uchambuzi wa vifungu na pia huweza kurekodi case tofauti za rejea.

Kimsingi uandaaji wa hukumu huchukua muda kutayarishwa na hukumu inaposomwa mahakamani inakuwa ni directly kutoka kwenye file imeandikwa kwa mkono, hii ni kuiepusha hukumu kuvuja kabla ya muda.

Baada ya hukumu kusomwa na hatua kuchukuliwa file hupelekwa kwa katibu mahsusi kwaajili ya uchapaji.

Uchapaji unapokamilika nakala hurudishwa kwa hakimu/ jaji kwa ajili ya kuhariri makosa ya kiuchapaji na hivyo hurekebishwa palipokosewa na hukumu husainiwa na hakimu husika.

Nakala ya hukumu huombwa kwa barua ambapo hakimu akiridhia kuwa upatiwe utapatiwa pasipo kuilipia.

Kumbuka;Nakala ya hukumu hutolewa bure.
 
Punguza upimbi jombaa, nini maana ya summary? Hivi huko vichwani huwa mmejaza funza au tatizo ni nini hasa? Narudia nijibu maana ya summary halafu nitarudi...
Summary ni muhtasari au ufupisho wa andiko lolote.
 
Hadi watoe copy..!! naona mashine zina shida kidogo mtapewa tu hukumu ni haki yenu ya kisheria kupewa.
 
Back
Top Bottom