Jaji aamuru Rama anayetuhumiwa kuua apimwe akili

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
216,612
728,446
Wednesday, 05 October 2011 19:44


James Magai
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imeamuru mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya tuhuma za mauaji ya kukusudia, Ramadhani Selemani, aliyekutwa akitafuna kichwa cha mtoto katika eneo la Hospitali ya Taifa Muhimbili, akapimwe akili.Ramadhani na mama yake mzazi Hadija Ally, wanashtakiwa kwa kosa la mauaji ya kukusudia ya mtoto Salome Yohana (3) katika eneo la Tabata jijini Dar es Salaam.

Kesi hiyo ilitarajiwa kuanza kusikilizwa kwa washtakiwa kusomewa maelezo ya awali ya mashtaka yao , lakini ilishindikana baada ya wakili wa washtakiwa hao Yusufu Shehe, kuiomba mahakama iamuru mshtakiwa huyo akapimwe akili.

"Mheshimiwa Jaji, kulingana na ushahidi wa kesi hii, chini ya kifungu cha 219 (1) Sura ya 20 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), ninaiomba mahakama yako iruhusu mshtakiwa wa kwanza akapimwe akili zake kwanza,"alisema Wakili Shehe.Alisema ameamua kutoa ombi hilo ili kujiridhisha na utimamu wa akili za mshtakiwa kabla ya kuanza kwa usikilizaji wa kesi hiyo kulingana na kumbukumbu za maelezo ya ushahidi ulioko.

Wakili Shehe alibainisha kuwa anakusudia mshtakiwa apimwe akili kwa wakati ule tu anaodai kutenda kosa analokabiliwa nao na si kwa wakati mwingine wowote.

Wakili wa upande Jamhuri, Dionisia Saiga, , alisema kulingana na ushahidi katika kesi hiyo hata wao hawana pingamizi dhidi ya ombi la wakili wa utetezi kuhusu mshtakiwa kupimwa akili.

Baada ya kuzisikiliza pande zote, Jaji Karua alikubaliana na ombi hilo la wakili wa utetezi na kutoa amri rasmi kwa mshtakiwa kupimwa akili kabla ya kuendelea na kesi hiyo.Jaji Karua aliahirisha kesi hiyo hadi itakapopangwa tarehe nyingine ya kuendelea nayo katika awamu nyingine ya vikao vya mahakama vya kesi za jinai.

Kabla ya kutoa ombi la mshtakiwa kupimwa akili, Wakili Shehe aliomba mahakama itoe amri ya kutafutwa kwa wakili mwingine kwa ajili ya kumtetea mmoja wa washtakiwa katika kesi hiyo.Wakili Shehe ambaye alikuwa akiwatete washtakiwa wote wawili alisema kwa mazingira ya kesi hiyo na ushahidi yakiwamo maelezo ya washtakiwa, asingeweza kuendelea kuwatetea wote.

Moja ya maelezo ambayo yalimsukuma Wakili Shehe aombe kutafutwa kwa wakili mwingine ni mshtakiwa wa kwanza, Ramadhani kumsukumia mama yake mzigo kuwa ndiye aliyefanya mauaji hayo.Hata hivyo mama yake Ramadhani naye anakana tuhuma hizo akidai kuwa siyo yeye aliyemuua mtoto huyo, maelezo ambayo pia yanaashiria kuwa anamwachia mzigo huo Ramadhani, aliyekutwa na kicha cha mtoto huyo.

Mahakama ilikubaliana na ombi hilo la wakili wa utetezi na kuamuru atafutwe wakili mwingine wa kumtetea mshtakiwa mwingine, kabla ya kesi hiyo haijapangiwa siku.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo
Ramadhan alikamatwa Aprili 26 mwaka 2008 na mlinzi wa Hospiltali ya Taifa ya Muhimbili, Fulgence Michael, akiwa na kichwa cha mtoto kikiwa kimesukwa nywele akidai kuwa alikuwa anampelekea zawadi muuguzi mmoja wa hospitali hiyo.

Kichwa hicho kilikuwa ndani ya mfuko wa Rambo huku akikitafuna hadharani huku akidai kuwa yeye na bibi yake walikuwa wamezoea kula nyama za watu.Tukio hilo liliwafanya wafanyakazi wa hospitali hiyo na watu wengine kuacha shughuli zao na kwenda kumshuhudia kijana huyo akitafuna kichwa hicho.

 

Malolella

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
366
109
Wana jf naomba kuuliza hvi ile kesi ya yule dogo Rama mlavichwa vya watu iliishia wapi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom