Jairo hana kosa lolote, ni majungu matupu-Mchungaji Lusekelo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jairo hana kosa lolote, ni majungu matupu-Mchungaji Lusekelo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Dec 27, 2011.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  MCHUNGAJI Kiongozi wa Kanisa la Maombezi (GRC) lililopo Ubungo Dar es Saama, Mchungaji Antoni Lusekelo, ameibuka na kusema kuwa sakata la Katibu Mkuu wa
  Wizara ya Nishati na Madini Bw. David Jairo, na Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Philemon Luhanjo, ni majungu na haina tatizo.

  Bw. Jairo anadaiwa kuchangisha fedha za umma kwa ajili ya kugharamikia kupitisha bajeti ya wizara hiyo kinyume cha utaratibu huku Bw. Luhanjo akidaiwa kumjingia kifua.

  Mchungaji Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako amesisitiza kuwa wapo viongozi wengi waliofanya kitendo sawa na ya Bw. Jairo lakini hayajulikani hivyo kutaka Watanzania kuacha tabia ya kuchafuana.

  Akizungunza na waandishi wa habari Kanisani kwake jana, Mchungaji Lusekelo alisema haiwezekani mtu mmoja kupanga kuchangisha fedha za wizara bila kuwa na mtandao na viongozi wengine na kudai kuwa kilichotokea ni siri kuvuja na si vinginevyo.

  "Ninachojua ni kwamba wezi wote wako mahakamani, unapoona mtu analalamikiwa kila siku wala hakamatwi ujue ni majungu tu na mambo hayo hafanyi, angefanya angekuwa selo

  Ikumbukwe kwamba kuharibiana na kuchafuana kupo, mfano mimi niliwahi kuambiwa kwamba nimeenda nchini Nigeria kutafuta nguvu za giza wakati sijawai hata kuwaza kufanya kitendo cha namna hiyo,"alisema Mchungaji Lusekelo.

  Aliendelea "Lazima tukiri kwamba watu wanachafuana na ndio maana ninasema hata kwa Bw. Jairo ni siri tu ilivuja na hawezi kufanya peke yake," alisisitiza.

  Kuhusu maadili ya uongozi alisema anasikitishwa na kutoweka kwa desturi ya viongozi wa zamani ambao walilala na kuamka wakiwa na mawazo ya nini kifanyike tofauti na ilivyo sasa.


  Source Majira.
   
 2. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sasa kama Jairo ni muumini wake na anatoa sadaka kubwa unadhani atamkandia! Nakumbuka moja ya kauli ya Yesu katika kitabu cha Biblia ni kwamba moja ya dalili za mwisho wa dunia ni kujitokeza kwa wanabii na watumishi wa mungu feki!
   
 3. S

  Song'ito JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  mkubwa kichwa cha habari chako hakiendani na habari, kimekaa kiuchochezi zaidi...habari inaonyesha kuwa jairo anahusika na hata lusekelo kasema hilo..ila tu anacholalamika ni kuwa anachafuliwa jairo peke yake na ndo kawaida ya serikali yetu, wanafanya madudu wengi then mmoja anabeba msalaba kwa yaliyofanywa na wote...jaribu kurekebisha kichwa cha habari,najua unatafuta support ya watu waseme maaskofu wanamtetea jairo, acha ipotoshaji na chokochoko hizi hazisaidii
   
 4. M

  Molemo JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  mkuu nimekosea eapi.Tafuta gszeti la majira na heading yake ndio hiyo hiyo.Sasa uchochezi wangu ni upi.Au bado una hangover ya xmass
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  Dec 27, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,872
  Likes Received: 6,222
  Trophy Points: 280
  tantalila tu....
   
 6. S

  Song'ito JF-Expert Member

  #6
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  asante kaka, naomba tu nikuhakikishie kuwa sinywi maishani mwangu hivyo kama ni hang over ya juisi nakubali!!! nafurahi pia kuona unaweza kuwa kuwa great thinker bila kutukana japo umenipa kashfa kidogo ya uhang over, umejitahidi katika hilo!!

  hapo kwenye red inaonyesha ushiriki wa jairo mkuu, sasa labda unambie kuwa napo sikui kiswahili... mimi si mmoja wa kondoo wa lusekelo bali ni mkristu!! Lusekelo anasema kama jairo angekuwa mwizi angekuwa ameshtakiwa na ukiangalia hawajamshtaki kwa nini? kwa kuwa wanajua kuwa jairo amebeba msalaba wao..madhambi wametenda wengi ila lazima awepo mmoja wa kumtoa kafara... ila lusekelo anaendelea kusisitiza kuwa hili limetokea kwa ajili ya kuvuja siri tu ndo mana wanatoana kafara... kiuhalisia hapo kwenye red inaonyesha jairo yumo ila amebebeshwa zigo na wenzake na kwa kuwa wanajua wamefanya wote ndo mana wanamgwaya
   
 7. M

  Molemo JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  appreciate sir
   
 8. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #8
  Dec 27, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,995
  Likes Received: 2,650
  Trophy Points: 280
  Mbuzi wa kafara.
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Huyu Mch. Lusekelo anastahili maombi maana anafuka vapour sana siku hizi
   
 10. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #10
  Dec 27, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Karibu atasema na CCM hamna mafisadi (haina Gamba), hawa watu bwana mi ndo maana nampenda Mchngaji Z. Kakobe hana unafiki wala hajikombi kwa serikali wala chama chochote
   
 11. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #11
  Dec 27, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hebu waanike yale majina kama makanisa hayajabaki wazi bila watu
   
 12. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #12
  Dec 27, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kama unaweza kuwa na kiongozi wa kiroho asiyetaka kukemea uovu na badala yake kwake kukemea uovu ni majingu basi ujue huyo ni chui kavaa ngozi ya kondoo, katika biblia kote hajatokea nabii wala mitume walioogopa kukemea uovu na kuita majungu wale waliokemea ila kwa mara ya kwanza nimemsikia "Mzee wa Upako" akitamka hilo..
   
 13. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #13
  Dec 27, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  30 March 2011

  Mzee wa upako aibuka akimfagilia JK

  Na Edmund Mihale

  MCHUNGAJI wa Kanisa la Maombezi, Anthony Lusekelo 'Mzee wa Upako' amesema kuwa wanaompinga, Rais Jakaya Kikwete katika utawala
  wake wapo katika ushindani lakini hawatashinda katika vita hiyo.

  Akizungumza na mwandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu kile alichokiita Afya ya Amani, Umoja, Upendo na Uvumilivu, Mchungaji Lisekelo alisema kuwa ili nchi iwe na afya inahitaji matunzo na si kelele za kulaumiana.

  Alisema kulaumiana kumeshika kasi tangu Rais Kikwete ashike madaraka kwa miaka mitano lakini mazuri aliyoyafanya hayasemwi bali mabaya ndiyo yanayozungumzwa hata kama yamejificha.

  Kauli za Mchungaji Lusekelo zimekuja kukiwa na malalamiko ndani ya jamii, kuhusiana na utendaji kazi wa serikali ya awamu ya nne, hasa kushindwa kupunguza mfumuko wa bei za bidhaa muhimu na kupunguza umaskini.

  Lakini yeye alisema, "Unapojenga afya ya kitu chochote ni lazima ujue misingi ya nchi ni lazima tuheshimu na kuwapenda viongozi wetu tuliochagua na kuwapigia kura. Hata katika maandiko kiongozi anatakiwa aonywe kwa hadhari, heshima na hekima na si kwa makelele.

  "Utawala ni mamlaka inayowekwa Mungu lakini inaashiria wazi kuwa tumeanza kuondoka katika misingi hiyo na sasa mtu yeyote anasimama na kumsema Rais Jakaya Kikwete anavyotaka. Hapana. Hili jambo halipendezi mbele ya Mungu," alisema Mchungaji Lusekelo.

  Alisema imejengeka tabia kuwa ukimsema Rais Kikwete ndiyo unaonekana kuwa jasiri na mzalendo, utamaduni ambao ni mbaya.

  "Hatupo tayari kumpongeza kiongozi akiwa hai, watu wanasifu maiti kuliko mtu akiwa hai hizi ni fikra za kishetani na hazipaswi kunyamaziwa.

  "Mfano Mwalimu alipokuwa hai hakuwa na sifa hizi tunazoziona sasa, walisema wazi wamechoka na 'unyerere' leo hii tunamasifu kwa kila nderemo. Watu wamebadilika wanasifu viongozi wanapotoka ndani ya madaraka.

  "Inakuwaje Rais Kikwete tunayemfahamu aliingia madarakani akiitwa Masia na chaguo la Mungu leo ni adui wa kwanza. Hili linatokana na wachache wanaomsaidia rais kukiacha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa na nguvu na kikaacha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa dhaifu. Hivi sasa kukitokea tatizo kama la kutonyesha mvua basi lawama atatupiwa rais," alisema

  Alisema kuwa ana imani kuwa rais atakayekumbukwa maishani ni Rais Kikwete hivyo aachwe atekeleleze mchakato wa katiba kupunguza mfumko wa bei na kujenga barabara za hewani.
   
 14. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #14
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,198
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Hili ndilo tatizo la watu kuingilia fani za watu. Mtu hana wito wa uchungaji anaenda kuwa mchunfgaji matokeo yake ndio kama haya.

  Ni sawa sawa tu na Mtu hawezi kuwa Rais na kuiongoza nchi, anafanya ujanja ujanja na anakuwa Rais, unategemea nchi itaenda sawa hiyo? matokeo yake si ndo hivi tunaona nchi inaenda yenyewe bila rais

  Khaaaaaaaaaaa
   
 15. M

  Magwero JF-Expert Member

  #15
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Ndugu mbona kupindisha maelezo ya kwenyebiblia..
  Usimwonee haya huyu ndugu..
  Imesema Manabii wa UONGO..
  Sio fek..
  Nikikurahsishia maelezo ulikuwa unamahanisha Lusekel ni Muongo..
   
 16. M

  Magwero JF-Expert Member

  #16
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Mim sitamani kuanza kuulizana uwezo wetu wa kuelewa au elimu tulizonazo...
  Hivi wew unadhani mzee wa upako asinge kuwa na maneno mazuri kama hayo uliyofafanua wew...!?
  Acha kujiongopea Kaka/dada..
  Jamaa ametoa maelezo ya kumtetea tu..
  Rudia tena kusoma utagundua..
   
 17. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #17
  Dec 27, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hawa waandishi wa habari nao ni kama ROBOTS, inamaana wao kazi yao ni kuandika kila kitu na kuchapisha?.... Hawa ni vilaza kabisa wanafahamu kilichotokea sasa wanapoandika habari kama hii wanamaanisha nini? wakati hadi PM alikubali kwamba jamaa kaiba kinoma....

  Hawa ndiyo wale wanaouza daw- z- kul----ya wanatafuata pa kutokea.
   
 18. S

  Song'ito JF-Expert Member

  #18
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  kaka usijugde elimu za watu bila kujua, hilo ni hosa kubwa sana!! unaweza kuongea bila kuonyesha kuwa wewe ni msomi maana waweza kukuta unayemuhubilia usomi ni msomi zaidi yako, lakini pia ni nani aliyekuambia usomi wa hali ya juu ndio ujuaji wa kila kitu?... na labda nadhani uanahitaji kuisoma hiyo habari vizuri, nakubali tatizo ni uelewa na sio uelewa unaoujua wewe, bali uelewa hapa ni juu ya lugha!! lugha uiliyozungumzwa na lusekelo inampoint moja kwa moja jairo, isipokuwa tu ametolewa kafara maana anasema katika usainiji kama huo lazima watu wengi walishirikishwa! kwa nini aonekane jairo pekee? ndo mzee wa upako anavyosema!!! na anaendelea kuhoji kama jairo angalikuwa na makosa angekuwa mahakamani, nikuulize swali, je jairo yupo mahakamani? na kama hayupo unadhani kwa nini hapelekwi mahakamani?
  ukijibu hilo ndo turudi tutazame wewe mwenye elimu unayodai unayo kama kweli unajua kile unachokiongea... Sipo kumtetea jairo ama lusekelo kwani si mmoja wapo na sipo nchini kabisa mkuu!! ila lugha iliyozungumzwa ni ya kueleweka kabisa
   
 19. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #19
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,269
  Trophy Points: 280
  Mimi huyu nilimwonaga bichwa lake limejaa maji baada ya kumuona ni rafiki wa karibu na Sheikh Yahya, maana nilijiuliza mfuga majini na mtumishi wa Mungu wapi na wapi?
   
 20. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #20
  Dec 27, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Huyu si mchungaji bali mchunaji anayewachuna akina Jairo ili awasafishe kama wenzake wengi wenye kufikiri kwa matumbo wanavyofanya kumsafisha Lowassa. Huyu ana uroho na roho mtakakitu badala ya roho mtakatifu. Hakika hawa ndio Yesu alisema ni chui kwenye ngozi ya kondoo. Wapaswa kuchomwa moto kama vibaka kwa kujiingiza kwenye mifuko ya mafisadi. Washindwe na walegee pia walaaniwe. May you perish Lusekelo mbwamwitu mchunaji!
   
Loading...