Jairo awatikisa Kikwete, Pinda; Luhanjo, Ngeleja ‘kubebeshwa msalaba?” | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jairo awatikisa Kikwete, Pinda; Luhanjo, Ngeleja ‘kubebeshwa msalaba?”

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 2, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145


  Waandishi Wetu Raia Mwema
  31 Aug 2011
  Toleo na 201


  [​IMG]
  • Luhanjo, Ngeleja ‘kubebeshwa msalaba?"
  • Serikalini sasa kwafukuta kila eneo
  BAADA ya Bunge kuunda Kamati Teule ya kuchunguza sakata la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, hali sasa si shwari serikalini na Rais Jakaya Kikwete, anaelezwa kujiandaa kufanya maamuzi mazito kusafisha hali ya hewa ya kisiasa inayoelekea kuvuruga mkakati wake kukisafisha Chama cha Mapinduzi (CCM) katika mtindo maarufu sasa wa ‘kujivua gamba'.

  Habari za ndani ya Serikali zimethibitisha kwamba kwa sasa kuna mtikisiko mkubwa uliotokana na mkanganyiko uliosababishwa na uamuzi wa Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, kutangaza kurudishwa kazini kwa Jairo aliyekuwa likizo akisubiri kuchunguzwa, uamuzi ambao ulitenguliwa na Rais Kikwete.

  Sakata hilo la Jairo sasa limewagusa kwa namna isiyo nzuri viongozi wote wa juu wa Serikali, akiwamo Rais Kikwete mwenyewe, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, (aliyetamani hata kutimuliwa kabisa kwa Jairo), Luhanjo (aliyemrudisha kazini) na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, aliyempokea wizarani kwa mbwembwe, akiruhusu hata wafanyakazi wengine kusukuma gari lake.

  Kuguswa kwa waandamizi hao wa juu serikalini, kunatishiwa zaidi na hatua ya Bunge kuunda Kamati Teule kuchunguza sakata hilo, jambo ambalo si ishara nzuri kwa kuwa hii ni mara ya kwanza kwa Bunge kuchunguza mtendaji wa juu wa Ofisi ya Rais Ikulu, ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi.

  Habari za ndani ya Serikali zinaeleza kwamba uamuzi wa kutengua uamuzi huo, saa chache baada ya kuwa umetangazwa na Luhanjo, ulitokana na Rais Kikwete kukwerwa na uamuzi huo ambao imethibitika kwamba ulifanyika katika mazingira tata.

  Ikulu ililazimika kutoa taarifa ya ufafanuzi baada ya baadhi ya vyombo vya habari kutafsiri kwamba kulikuwapo na ugeugeu kwa ofisi moja (Ikulu) kutoa maamuzi yanayokinzana; yaani uamuzi wa kumrudisha Jairo kazini kwa mbwembwe na uamuzi wa kutaka aendelee kuwa likizo akisubiri hatima yake.

  Taarifa ya Ikulu iliyotolewa Agosti 26, 2011 kwa vyombo vya habari ikionyesha kuwa na uharaka (urgent) ilieleza hakukuwa na mkanganyiko wowote kati ya Rais Kikwete na Katibu Mkuu Kiongozi wake, Luhanjo, kwa maelezo kwamba wote walikua sahihi kwa mamlaka waliyonayo kisheria.

  Taarifa ya Ikulu iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, ikiwa na baadhi ya meneno yaliyowekewa msisitizo kwa herufi kubwa ilieleza;
  "Julai 21, 2011, Katibu Mkuu Kiongozi Phillemon Luhanjo, akitumia madaraka yake ya Mamlaka ya Nidhamu ya Watumishi wa Umma, alitangaza hatua ya kumpa likizo ya malipo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishatai na Madini, David Kitundu Jairo, ili kupisha uchunguzi aliokuwa ameuagiza ufanyike dhidi yake.

  "Luhanjo alichukua hatua ya kumsimamisha Jairo kufuatia tuhuma zilizokuwa zimeelekezwa dhidi yake (kwake) na baadhi ya wabunge wakati wa mjadala kuhusu Makadirio na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka 2011/12 katika kikao cha Bunge kilichofanyika tarehe 18 Julai, 2011.

  "Katika mjadala huo, baadhi ya wabunge walihoji uhalali wa Wizara kuomba michango ya fedha kutoka kwenye taasisi zilizoko chini ya usimamizi wake ili kusaidia Bajeti ya Wizara hiyo kupita kwa urahisi.

  "Kufuatia hatua hiyo ya kumsimamisha kazi Bw. Jairo, Katibu Mkuu Kiongozi alimwomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh kufanya ukaguzi maalumu na uchunguzi wa awali juu ya tuhuma hizo.

  "Tarehe 9 Agosti, 2011, Utouh aliwasilisha Ripoti yake kwa Katibu Mkuu Kiongozi, na tarehe 23, Agosti, 2011, Katibu Mkuu Kiongozi akiambatana na Utouh, alitangaza mbele ya waandishi wa habari matokeo ya ukaguzi huo maalumu na uchunguzi wa awali juu ya tuhuma dhidi ya Jairo," ilieleza taarifa hiyo.

  Katika Ripoti yake mbele ya waandishi wa habari, taarifa ya Ikulu ilinukuu taarifa ya Utouh ikieleza: "Ukaguzi maalum haukuthibitisha kuwapo kwa usahihi wa tuhuma zilizotolewa dhidi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini David Kitundu Jairo."

  Taarifa hiyo ya Ikulu ilieleza kwamba Katibu Mkuu Kiongozi alitumia taarifa ya CAG kuwaambia waandishi wa habari kwamba: "Matokeo ya uchunguzi huo ni kwamba tuhuma zilizotolewa Bungeni tarehe 18 Julai, 2011, hazikuweza kuthibitika."

  Akitumia vifungu vya sheria, Luhanjo amenukuliwa na Ikulu akisema; "mimi kama Mamlaka ya Nidhamu ya Katibu Mkuu, Nishati na Madini, David Kitundu Jairo, sitaweza kuendelea na hatua ya pili ya kumpa taarifa ya tuhuma (notice) na Hati ya Mashitaka kwa sababu Bwana David Kitundu Jairo, hajapatikana na kosa la kinidhamu (disciplinary offence) kwa mujibu wa Taarifa ya Ukaguzi Maalumu."

  Luhanjo alinukuliwa akisema kwamba kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa Sheria Na. 8 ya Utumishi Umma ya Mwaka 2002 na kanuni zake za Mwaka 2003, aliamuru Jairo aendele kazini siku ya Jumatano Agosti 24, 2011.

  Katika ufafanuzi wake, Ikulu ilieleza kwamba, "baada ya kupokea taarifa ya uchunguzi ya CAG na uamuzi wa Katibu Mkuu Kiongozi kuhusu suala hilo asubuhi ya tarehe 25 Agosti, 2011, Rais Kikwete, aliamua kuwa Jairo asirudi kazini mpaka kwanza yeye Rais atapoamua namna gani ya kurudi kazini, lini na wapi.

  "Katibu Mkuu Kiongozi alifikisha uamuzi huo wa Rais kwa David Jairo ambaye mapema asubuhi ya siku hiyo alikuwa ameripoti kazini. Ndugu Jairo alitii uamuzi huo wa Rais. Tunapenda kusisitiza kuwa Rais hajawa kigeugeu kwa sababu alifanya uamuzi mmoja tu baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi."

  Taarifa ya Ikulu ilionyesha pia kwamba uamuzi huo aliufanya kabla ya Bunge kulizungumzia suala hilo na hivyo uamuzi huo wa Rais haukutokana na shinikizo la Bunge na kwamba pamoja na kumweleza Katibu Mkuu Kiongozi, Rais pia alimfahamisha Waziri Mkuu kuhusu uamuzi wake huo asubuhi hiyo ya Agosti 25, 2011.

  Maelezo hayo ya Ikulu yanaashiria kwamba kwamba uamuzi wa Luhanjo umechokoza mambo mengi yanayomhusu mtendaji huyo wa juu serikalini, zikiwamo taarifa zinazohusu muda wake wa kustaafu na maamuzi na mahusiano yake kikazi na watendaji wengine katika wizara alizowahi kufanya kazi kabla ya kuhamishiwa Ikulu.

  Luhanjo amewahi kuwa Katibu Mkuu katika Wizara za Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na WIzara ya Maliasili na Utalii kabla ya kuhamishiwa Ikulu kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, nafasi ambayo inaelezwa kwamba alitarajiwa kuwa amestaafu kabla ya uchaguzi wa mwaka 2010.

  Baadhi ya wachambuzi na asasi za kiraia na vyombo vya habari vimekuwa vikitoa tafsiri mbaya kwa Serikali kuhusu suala hilo la Jairo vikianzia na kauli ya Pinda Bungeni kwamba angekuwa na mamlaka kisheria angemchukulia hatua Jairo siku hiyohiyo ya tuhuma, kabla ya Serikali kumpa likizo na kutokea kwa utata baada ya taarifa ya CAG.

  Miongoni mwa waliotoa matamko waziwazi ni Mbunge wa zamani wa Bumbuli na mtendaji mwandamizi mstaafu serikalini William Shellukindo, ambaye alisema moja kwa moja kwamba Luhanjo ameshindwa kumsaidia Rais Kikwete.

  Shelukindo ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Rais Ikulu (cheo ambacho sasa kinaitwa Katibu Mkuu Kiongozi) katika Serikali ya Awamu ya Kwanza ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Rais Ali Hassan Mwinyi, amenukuliwa na gazeti la Mwananchi Jumapili iliyopita akisema Luhanjo ameonyesha utovu wa nidhamu na ameidhalilisha Ikulu kutangaza kumrejesha Jairo bila kupitia bungeni.

  "Sipendi kuzungumza hivi sasa kwa sababu nimeamua kukaa kimya, lakini kwa kuwa naheshimiana na vyombo vya habari na mmetaka nizungumzie suala hili, nasema Luhanjo amemdhalilisha Rais Kikwete na alitaka kumchonganisha na mhimili muhimu wa Bunge," alisema Shellukindo ambaye mke wake Beatrice Shellukindo ndiye ‘aliyewasha moto' wa Jairo bungeni.

  Kutokana na utata huo wabunge walionekana kukerwa na kuitikisa serikali bungeni, baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe kutoa hoja ya kutaka ripoti maalumu ya CAG kuhusiana na sakata hilo kuwasilishwa bungeni vinginevyo wabunge wasusie shughuli za serikali kabla ya Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka kupendekeza kuundwa kwa Kamati Teule.

  Tayari Bunge Spika wa Bunge, Anne Makinda ameunda Kamati Teule kuchunguza utaratibu uliotumiwa na Wizara ya Nishati na Madini, kukusanya fedha kutoka katika taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo kwa ajili ya kufanikisha mchakato wa kupitisha wa bajeti pamoja na utata uliojitokeza kumrudisha kazini Jairo.

  Makinda alisema kamati hiyo itakayofanya kazi kwa wiki zisizozidi nane pia itachunguza iwapo hatua ya Katibu Mkuu Kiongozi, Luhanjo, kutangaza matokeo ya uchunguzi dhidi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo uliingilia haki na madaraka ya Bunge.

  Hii ni kamati teule ya pili kuundwa wakati wa uongozi wa Rais Jakaya Kikwete, kwa wizara hiyohiyo ya Nishati na Madini, ikitanguliwa na Kamati Teule iliyochunguza sakata la ununuzi wa mitambo ya dharura ya kuzalisha umeme, kamati iliyosababisha kujiuzulu kwa mawaziri watatu akiwamo aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na mawaziri, Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha.

  Kamati hiyo iliongozwa na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Dk Harrison Mwakyembe. Mwakyembe sasa ni Naibu waziri wa Ujenzi.

  Wanaounda kamati ya kumchunguza Jairo ni mbunge wa Tunduru Kaskazini, Injinia Ramo Makani (CCM), Mbunge wa Karagwe, Goesbert Blandes (CCM), Mchungaji Israel Natse (Karatu-CHADEMA), Khalifa Suleiman Khalifa (Gando-CUF) na Mbunge wa Viti Maalum, Martha Jachi Umbulla (CCM).

  Katika taarifa yake ya kuunda Kamati Teule, Makinda alisema "Bunge lilipitisha azimio la kuunda Kamati Teule kwa ajili ya kuchunguza uhalali wa utaratibu wa Wizara kuchangisha fedha kwa ajili ya kupitisha bajeti na kubaini kama kitendo cha Katibu Mkuu Kiongozi, kutoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya uchunguzi wa suala la fedha zilizokuwa zikichangishwa na Wizara ya Nishati na Madini kimeingilia na kuathiri madaraka ya Bunge.

  Utaratibu huo umekamilika na kamati hiyo nimeiunda kwa mujibu wa Kanuni ya 2(2) na 117(4) ya Kanuni za Bunge toleo la 2007".

  Makinda alisema kamati hiyo itafanya kazi kwa kuongozwa na hadidu tano za rejea ambazo ni kuchunguza utaratibu uliobainika wa kukusanya fedha kwa ajili ya kukamilishwa kwa uwasilishaji wa Hotuba za bajeti za wizara bungeni na kwamba, hadidu hiyo ya kwanza itakuwa na vipengele vitatu.

  Vipengele hivyo ni pamoja na kuchunguza uhalali wa utaratibu huo kisheria na kwa mujibu wa kanuni, iwapo fedha hizo huwa zinakasimiwa katika bajeti husika pamoja na matumizi halisi ya fedha zilizokusanywa.

  "Hadidu rejea ya pili ni kupitia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu uchunguzi alioufanya kuhusiana na agizo la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini kuchangisha fedha taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kwa ajili ya kufanikisha uwasilishaji wa Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni," alisema Makinda na kuongeza:

  "Hadidu rejea ya tatu ni kuchunguza mfumo wa Serikali kujibu hoja zinazotolewa bungeni na taratibu za kuarifu Bunge matokeo ya utekelezaji wa hoja hizo".

  Makinda alisema hadidu rejea hiyo ya tatu ina vipengele viwili ambavyo ni kuchunguzwa kwa usahihi wa utaratibu uliotumiwa na Katibu Mkuu Kiongozi kwa suala la Jairo na kubaini iwapo utaratibu huo umeathiri dhana ya haki na madaraka ya Bunge.

  Aliitaja hadidu ya rejea ya nne kuwa ni kuangalia nafasi ya Mamlaka ya Uteuzi kwa ngazi za Makatibu Wakuu katika kushughulikia masuala ya nidhamu ya anaowateua na ya mwisho inawaelekeza wajumbe wa Kamati hiyo kuangalia mambo mengine yoyote yenye uhusiano na uchunguzi huo.

  "Ni imani yangu ya wabuge wote na Watanzania wote kwa ujumla kwamba ninyi niliowateua mtafanya kazi hii kwa umakini, busara na uaminifu mkubwa mkiongozwa na Katiba ya nchi, sheria na kanuni zetu na vilevile mtatoa haki kwa watu wote watakaohusika na suala hili," alisema Spika Makinda.
   
 2. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  • Wabunge hawawezi kufanya kazi kwa umakini sababu katika walioteuliwa hatuwezi kujua kama wapo walipokekea hizo pesa a jairo auza wizara nyingine.
  • wabunge hawawezi kutoka haki wote kwa wahusika hasa waabunge wenzao sababu wao pia ni wabunge. Maamuzi yao yatakuwa na upendeleao kwa wabunge. maaamuzi ya kamati yatainyonga zaidi serikali bila kuonyesha udhaifu na tamaa mbaya za wabunge kupenda zaidi na zaidi
  Kamati iliyotakiwa kuunda ilitakiwa kuwa amati huru hasa si ya serikali wala ya wabuge bali kamati maalum ya bunge lakini wajumbe wangekuwa ni majaji au mahakama.
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Jk hana jipya bwana anawaza mafutari ya sita swala tu hana lolote
   
 4. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 740
  Trophy Points: 280
  Kulindana ndio tatizo.
   
 5. Power to the People

  Power to the People JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2011
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 1,193
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Sasa kama JK ndio ataamua tume imeundwa ya nini hii ni kupoteza muda tu kwa kweli. Hata tume ije matokeo gani huyu bwana ataenda kupata ulaji mahala pengine
   
 6. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2011
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  No doubts tunavuna tulichopanda. Hii system nzima tokea juu kabisa needs total overhauling! Hatuna jinsi maana kama juu kuna matatizo makubwa,how could we talk of problems at lower level when the biggest problems manifested to be at the senior level?
   
 7. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  naunga mkono
   
 8. u

  ugali Member

  #8
  Sep 2, 2011
  Joined: Mar 31, 2010
  Messages: 25
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Ndugu zangu wa JF, nimesikia kuwa hawa jamaa wawili walisoma pamoja. Naomba mwenye ukweli wa haya anijuzu.
   
 9. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #9
  Sep 2, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  JK alivyomwoga eti atafanya maamuzi magumu!?? Kamwe halitatokea kwake, pamoja na kwamba Jk ndiye mkuu wa nchi, bado ana mabosi wake wanaomremote wha to do.
   
 10. Umutimbaru

  Umutimbaru Member

  #10
  Sep 2, 2011
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 91
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Alikuwa na haraka gani huyo mkubwa huyu kutangaza kurudishwa kazini kwa bwana jairo. huko ni kulewa madaraka.
   
 11. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #11
  Sep 2, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Luhanjo naona kama amemess up na kitu kinaitwa Chain of Command kama sikosei
   
 12. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #12
  Sep 2, 2011
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Yaani hapa siombi cha muongozo wa spika naunga mkono hoja kwa asilimia mia
   
 13. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #13
  Sep 2, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,155
  Trophy Points: 280
  Raia Mwema si gazeti ls Mbowe hili? tutegemee nini zaidi ya kuwafitinisha CCM na Serikali yao?
   
 14. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #14
  Sep 2, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,155
  Trophy Points: 280

  Kwani walioipeleka hii habari bungeni walikuwa kina nani?
   
 15. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #15
  Sep 2, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Chawa. Nkapa, EL, RA, Chenge, Jairo, Manji hawa ni wahujumu wa uchumi wako free wanapeta Msemakweli baada ya jana tu yupo ndani tayari anahojiwa, vipi waliokwapua pesa BOT ambako ushahidi upo na unajulikana tena kwa maandishi, Jairo kuomba pesa na kutoa rushwa ushahidi upo. Mwambie Fisadi papa umegonga ukuta.
   
 16. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #16
  Sep 2, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Raia Mwema halijawahi kumilikiwa na Mbowe inafahamika ni mali ya kada maarufu wa CCM Jenerali T. Ulimwengu, ambaye amejipambanua ndani na nje ya nchi kama mwandishi makini tangu akiwa Habari Cop. Hii serikali kwenye hili la Jairo imekosea sana kwasababu ya kulindana maana wengi kati yenu ni mafisadi hakuna wa kumuumbua mwengine.
   
 17. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #17
  Sep 3, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Ukipewa story za Luhanjo utabaki unashangaa sana! hii nchni nadhani hata hivyo vyeo watu wasafi hawawezi kuvishika hata siku moja, maana Luhanjo ni mchafu kuliko uchafu wowote ambao nimewai kuuona, ila ajabu sijui kwanini sehemu nyingi sana ameonekana kumpiga kanzu Mkuu wake sio swala la Jairo tu! kuna mengi; ukinzia kwenye uteuzi wa mawaziri na swala la spika. Kinachonishangaza sana, au Rais anaumwa hajitambui? maana Luhanjo amekuwa anafanya mambo kama anavyotaka pale Ikulu!

  Alilazimisha wizi wa kura jimbo moja huko Njombe ili apite ndugu yake ambaye baadae akaja kupewa uwaziri, mtu amefanya kazi serikali na alikuwa mwizi mkubwa sana TANROADS Dodoma bado ana retire na kupewa uwaziri kwa mgongo wa undugu? Luhanjo ni mshenzi na hana maana zaidi ya ubinafsi na ukabila.
   
 18. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #18
  Sep 3, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo angesubiri Bunge wahailishe?
   
 19. k

  kiloni JF-Expert Member

  #19
  Sep 3, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mwanamke anapokuwa GAMBA!!!
   
 20. matungusha

  matungusha JF-Expert Member

  #20
  Sep 3, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  mume wako hana mke!!!!
   
Loading...