Jahazi imezama wakati ikielekea Mafia kutoka Kisiju

Habari zenu wakuu

Kwanza nawashukuru kwa wale wote walionipa ushauri, kwa sasa nipo vizuri nimeachana na mawazo ya kufakufa.

Kuna jambo limetokea na mpaka sasa hakuna taarifa ya hawa watu wako wapi. Kuna jahazi imetokea Kisiju ikalala kisiwa cha Koma. Siku ya pili ikatoka Koma kuelekea Mafia (namaanisha Leo Jumanne asubuhi)

Kwa habari zilizopo mpaka sasa wamezama sababu kulikuwa na boti ilikuwa ikivinjari maeneo ya bahari ndipo wakaona ishara ya kuombwa msaada baada ya wenye jahazi kuwapungia wakitaka msaada. Boti wakati inaenda kuwasaidia ndio ile jahazi imezama mazima ikiwa na watu wanaofikia sita mwanamke akiwemo.

Binafsi katika hao sita ndugu zangu wapo watatu na mpaka sasa hawajaonekana wamezama kati ya Nyororo na mkondo
wa Nyara.

Taarifa zaid nitawajuza

NB: Picha haihusiani na ajali ya leo

======

Jahazi, Mashua ya Mizigo iliyokuwa Ikitoka Kisiju kuelekea Kilindoni Mafia. Mashuhuda wanadai Mashua hiyo ilikuwa na Wafanyakazi watano.

Inadaiwa hapakuwa na upepo mkali wa kuzamisha Jahazi hivyo wanahia inawezekana Jahazi ikawa imegonga Fungu(sehemu ya Mchanga) au ikawa imegonga Mwamba.

Ashuhuda wanadai Jahazi lilizama saa tatu asubuhi, lilikuwa limepakia Cement. Kati ya Watano waliozama, Wawili wamepatikana, watatu bado hawajapatikana.

Waliopatikana wakiwa hai ni:

1. Haji Salum Mkazi wa Kisiju na Mafia
2. Msiwao Mkazi wa Mafia.

Ambao hawajapatikana ni;

3. Hanifa Mohamed Mkazi wa Mafia
4. Ally Omary Mkazi wa Mafia
5. Saidi Mkazi wa Mafia
Mmh Poleni
 
Poleni sana.. Naifahamu hiyo route.... Tuwaombee wepesi ambao bado hawajapatikana

Jr
 
MUNGU awasaidie..INAONYESHA BOTI HAIKUWA NA LIFE SAVING EQUIPMENTS? vifaa vingekuwapo WANGEOKOKA..

Sent using Jamii Forums mobile app
Wavuvi wetu wenyeji huwa wanajiamini SANA, ukizingatia na mambo yetu ya kiswahili kupitia kwa Madokta vilingeni, huwa wanajiamini SANA..
Vifaa cya uokozi siyo kipaumbele..
SUMATRA iliyovunjika sijui kwann ilifeli katika hili..

Everyday is Saturday.............. :cool:

Poleni ndugu kwa hili....
 
namba 3 alipatikana akiwa kafa ashazikwa hao walibak mpaka leo hawajapatikana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom