Jafo wa CCM ampiku tena Mnyika wa CHADEMA muswada fao la kujitoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jafo wa CCM ampiku tena Mnyika wa CHADEMA muswada fao la kujitoa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Habarindiyohiyo, Oct 17, 2012.

 1. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jafo wa CCM ampiku tena Mnyika wa CHADEMA muswada fao la kujitoa

  Jemadari wa CCM Selaman Jafo kwa mara nyingine tena amemzidi kete Mnyika wa CHADEMA kwa kuwasilisha muswada kuhusu fao la kujitoa kwa hati ya dharura. Awali Jafo katika mkutano uliopita wa bunge aliomba muongozo wa Spika kuhusu malalamiko ya wafanyakazi kufuatia kuondolewa kwa fao la kujitoa na kupewa nafasi na bunge ya kuzunguka kukusanya maoni kwa ajili ya kuwasilisha hoja binafsi.

  Wakati Jafo akizunguka kukusanya maoni ratiba ya bunge ilibadilishwa na hoja binafsi za wabunge kuondolewa hali iliyomfanya Mnyika kuomba muongozo mwingine wa kutaka ratiba irekebishwe kuruhusu kuwasilishwa kwa muswada binafsi kwa hati ya dharura kufanya marekebisho katika mkutano wa nane wa bunge.

  Pamoja na muongozo huo Mnyika alifanya mkutano na waandishi wa habari Dodoma na kueleza kwamba Serikali na Uongozi wa Bunge wameshawaacha solemba wafanyakazi kwa kuwa suala hilo limeondolewa kwenye ratiba na pia hata kama ikiwa kwenye ratiba ya bunge hoja binafsi haiwezi kuwa suluhisho la haraka kwa kuwa inategemea utayari wa serikali kutekeleza maazimio ya bunge.

  Mnyika alidai kuwa badala ya hoja binafsi kuwasilishwa na Jafo kushughulikia matokeo kwa kuwa chanzo ni sheria uwasilishwe muswada binafsi wa sheria kwa hati ya dharura ama na serikali, au kamati au mbunge yoyote kurekebisha hali hiyo na kueleza kusudio lake kufanya hivyo.Kufuatia hatua hiyo ya Mnyika, Kamanda Jafo alirejea haraka kutoka migodini na kufanya mkutano na waandishi wa habari kueleza kuwa tayari uongozi wa bunge umemhakikishia kuwa atapewa nafasi ya kuwasilisha hoja binafsi hata kama haiku kwenye ratiba hivyo hakuna sababu ya Mnyika kupewa nafasi ya kuwasilisha muswada binafsi wa sheria.

  Ili kuepusha Bajeti ya Wizara ya Kazi na Ajira isikwamishwe na wabunge kutokana na mgogoro wa fao la kujitoa, na kwa kuwa hoja binafsi za wabunge huwasilishwa mwishoni mwa mkutano wa bunge baada ya hoja za serikali na hoja hizo kwa mkutano uliopita ziliondolewa kwenye ratiba; Kamanda Jafo alipewa fursa ya kuwasilisha maelezo binafsi na Spika kuagiza kwamba Waziri katika hotuba ya bajeti ya Wizara yake azungumze pia maelezo hayo kesho yake.

  Spika alichukua hatua hiyo kwa kuzingatia kuwa kwa mujibu wa kanuni za Bunge maelezo binafsi hayapaswi kujibiwa wala hayajadiliwi na bunge kwa ajili ya kupitisha maazimio. Katika maelezo yake binafsi Jafo alitaka Serikali ikubali kuwasilisha muswada binafsi katika Mkutano wa Bunge wa tisa wa Bunge.Siku moja baada ya Kamanda Jafo kuwasilisha maelezo yake Waziri wa Kazi na Ajira alitoa hotuba na kukubaliana na maelezo hayo na kuahidi Serikali kuwasilisha muswada kwa hati ya dharura katika mkutano wa tisa wa Bunge uliopangwa kuanza 30 Oktoba 2012. Baada ya majibu hayo ya serikali, Spika alihoji wabunge iwapo wanakubaliana na swala hilo na wabunge wengi wakaitikia kukubali.

  Hata hivyo, Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha bajeti ya Wizara hiyo Jafo aliipongeza serikali kwa kukubaliana na hoja yake yake huku Mnyika akitaka bado Serikali itoe maelekezo ya kisera ya kutengua tangazo la SSRA ya kusitisha fao la kujitoa ili utaratibu wa zamani uendelee kuwepo mpaka pale muswada wa sheria kwa hati ya dharura utakapowasilishwa kwa kuzingatia kuwa hakuna kanuni iliyotungwa kufuatia marekebisho ya tarehe 13 Aprili 2012 na pia marekebisho hayo juu ya fao la kujitoa yalihusu mfuko mmoja tu wa PPF.

  Waziri Kabaka alimjibu kuwa Serikali itatoa muongozo na toka kuisha kwa mkutano huo wa bunge Mnyika amenukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari akiendelea kutaka Waziri kutoa maelekezo ya kuwezesha fao la kujitoa kurejeshwa huku Jafo akizungumza na vyombo vya habari kuipongeza serikali kwa kuwa sikivu na kukubaliana na hoja yake binafsi na hivyo mgogoro huo kupata ufumbuzi.

  Mwanzoni mwa wiki hii Mnyika amenukuliwa tena na vyombo vya habari akieleza kwamba amewasilisha kusudio la kuwasilisha muswada binafsi kwa hati ya dharura kama alivyofanya awali baada ya Serikali kuonyesha kutoka na dhamira ya kuwasilisha muswada huo kwa hati ya dharura kwenye mkutano wa tisa wa bunge pamoja na kuahidi hivyo bungeni.

  Siku chache baada ya Mnyika kutoa kauli hiyo Jemedari Jafo kwa mara nyingine tena alimpiku kwa kueleza kuwa mara baada ya kusudio lake yeye amekwenda kwa katibu wa bunge na kuwasilisha muswada huo kwa hati ya dharura. Kamanda Jafo amewaeleza waandishi wa habari kwamba Mnyika anadandia hoja yake na kwamba ni yeye anayepaswa kuwasilisha muswada binafsi bungeni.

  Kwa mujibu wa habari ya gazeti la Uhuru la leo lenye kichwa cha habari “Mnyika aumbuka, adaiwa kudandia hoja” Mheshimiwa Jafo ameeleza kwamba tayari amepata saini kutoka wabunge kumi wa CCM ili kujiandaa kuwasilisha muswada huo na kumkanya Mnyika aache tabia ya kudandia hoja kwa mbele. CCM imetoa pongezi kwa Jafo ambaye zaidi ya hoja binafsi amechukua suala la muswada binafsi la Mnyika na kulifanyia kazi ikiwa ni ushahidi wa kuwa mbunge wa chama kinachojali maslahi ya wafanyakazi.

  .....ndiyohiyo
   
 2. K

  KIROJO Senior Member

  #2
  Oct 17, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  So what?
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Huyo jafo kashachoka ubunge wa kisalawe amuulize janguo.
   
 4. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Bila umakini wa mnyika jafo asingeweza kuandaa muswada wa hoja binafsi. Kinachofanyika yeye anasubiri mnyika ateme madini yeye anafanya kuokota tu.
   
 5. S

  Serayamajimbo Senior Member

  #5
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona kwa maelezo yako Mnyika ndio wa kwanza kuwasilisha kusudio la muswada binafsi bungeni kwa hati ya dharura mara zote mbili? Jafo yeye alisema anawasilisha hoja binafsi na si muswada binafsi lakini hatimaye kwa maelezo yako Serikali na Jafo wote sasa wanafuata mkondo wa Mnyika wa muswada kwa hati ya dharura. Hapa Mnyika aliona mbali na kama wote wangemfuata mapema mbona suala hili lingekuwa limeshapata ufumbuzi toka mwezi Agosti? Ona sasa kwa kutokuona mbali mpaka sasa wafanyakazi wanalia na mafao. Jafo na wenzake wamechelewesha hili kurekebishwa, sasa inaonyesha mpaka mwakani; Serikali hii ya CCM ina nini na fedha zetu wafanyakazi?

  serayamajimbo
   
 6. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,330
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  sisi tunachotaka ni kazi ifanyike hata kama ingepelekwa na chizi kama ina maslahi ya Taifa sawa. kuwa wa kwanza au wa mwisho kuwasilisha haina tija kwetu. Misifa hiyo
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Jafo kinyozi pale hostel 3 USA...hhaaaaaa GPA ya 2.9 .....kazi ipo
   
 8. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Shemeji kwa kauli hii nakukubali sana.
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Jafo Unamsikilizia mnyika afanye na wewe uanze kukurupuka,ulikaa kimya mda wote ulivyoona mnyika kapeleka na wewe unaibuka mafichoni kwa nyodo,acha ujinga wewe jafo usifikiri utakua na position hyo milele,kwani wewe ndio wa kwanza kuwa mb wa kisarawe? Hao magamba wanakutumia kama mundoko angalia mwisho watakutupa jalalani......Weka maslahi ya taifa kwanza hiyo sheria itakuja kumsaidia hata mjukuu wako usiangalia karibu think big broda......
   
 10. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Jf siku iz ina mzaha sana.....?
  Hivi jafo naye ni jemedari kweli ?
   
 11. Codon

  Codon JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2012
  Joined: Dec 16, 2011
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Endekezeni mbwembwe tu!2015 Mtapata majibu tu!Mtajua hoja zipi watanzania walizipenda nazipi zilikuwa laghai!Tunachoomba ni Uchagu HURU NAWAHAKI BASI.
   
 12. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Wafanyakazi tuandamane, wafanyakazi ndo wasomi wa nchi hii. Tuwaonyeshe wakulima njia

  Ukondoo wetu ndo mwisho wake huu tunakatwa mkia tukiwa hai
   
 13. Mjamii

  Mjamii JF-Expert Member

  #13
  Oct 17, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 941
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 60
  Am smelling a rat here! Kuna ka mchezo kachafu ka kuchelewesha hii hoja ili baadhi ya wakubwa wa haya mashirika waendelee kutunyonya. Hivi kama Jafo ana tetea wafanyakazi kwa nini asiungane na mwenzake jamani lets open our eyes!
   
 14. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #14
  Oct 17, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  kwani wanashindania nini katika hilo?!
   
 15. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #15
  Oct 17, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Hebu pitia approach ya Jafo mwanzoni (rangi nyekundu), then pitia approach ya Mnyika (Rangi ya bluu), alafu angalia conclusion (palipokuzwa na kuwa bolded), alafu tuangalie ni nani kati ya hawa wawili alikuwa na right approach from the beginning, na kisha ujiulizwe nani kadandia 'approach' ya mwenzake...
   
 16. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #16
  Oct 17, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Jafo wala hana la kujivunia hapo maana anatekeleza wajibu wake na CCM inakula matapishi yake baada ya kubanwa koromeo na Mnyika.
  Kazi ya upinzani ni kuisimamia serikali na kwa mantiki hiyo nadhani wa kupewa sifa (kama zina faida yoyote) ni CHADEMA kupitia kwa Mnyika.

  Ni habari njema kuwa CHADEMA inatoa mwongozo na serikali ya CCM inatekeleza.
   
 17. M

  MLERAI JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 673
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Huyo Jafo kwanini unamwita jemedari wakati anaonekana Kama vile Ndio nakwamisha huo mswada usishughulikiwe kwa wakati muafaka?
   
 18. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #18
  Oct 17, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kuna mijitu inakurupuka siku hizi humu jukwaani!
   
 19. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #19
  Oct 17, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Sisi hatutaki kujua nani ni nani cha msingi hela zetu tupewe hayo mengine ni utumishi tu wa kila mmoja basi
   
 20. F

  FredKavishe Verified User

  #20
  Oct 17, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,090
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Jamaa anatoka 2015 makamanda tunajiandaa kuchukua jimbo la kisarawe
   
Loading...