Jafo ateua wajumbe saba kuishauri Serikali kuhusu elimu katika Muungano

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,000
9,862
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (muungano na mazingira), Seleman Jafo amewateua wajumbe saba wa kamati watakaotoa ushauri wa kitaalamu kuhusu uboreshaji wa elimu.

Wajumbe hao ni Profesa Alexander Makulilo (Naibu makamu wa mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma) ambaye ni mwenyekiti, mbunge wa viti maalumu, Najma Murtaza Giga (makamu mwenyekiti), Abdulmarik Mollel ambaye ni mkurugenzi wa mtendaji wa Global Education Link.

Wengine ni Khalid Bakari Hamrani (mkurugenzi wa uratibu wa shughuli za Serikali, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais , Sera , Uratibu na Baraza la Wawakilishi na katibu mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani (Necta), Dk Charles Msonde.

Katika kamati hiyo pia naibu katibu mkuu wa Tamisemi anayeshughulikia elimu Gerald Mweli, pamoja na Said Hamad Shehe ambaye ni mkufunzi wa Chuo cha Utumishi Umma Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa jana Jumatatu Mei 17, 2021 na mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini, Lulu Mussa imeeleza kuwa uteuzi umefanyika ikiwa ni hatua ya kushughulikia maoni yaliyotolewa na wadau mbalimbali kuhusu tofauti ya ufaulu kati ya wanafunzi wa sekondari wa shule za Tanzania bara na Zanzibar kwa matokeo ya kidato cha nne na sita.

“Wabunge mbalimbali wamekuwa wakiwasilisha hoja hiyo wakati wa mjadala wa bajeti ya ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira). Kamati iliyoundwa itafanya kazi kwa siku 35 kuwasilisha taarifa kwa Jafo.”

“Mheshimiwa Jafo kwa kushirikiana Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi wataweza kukaaa na mawaziri wanaohusika na elimu Tanzania bara na Zanzibar kushauri namna bora ya kuboresha elimu pande zote mbili za Muungano,” amesema Lulu katika taarifa hiyo.
 
Posho za watu wa Serikali nzuri Sana kweli Serikali inapenda Sana watu na watu wanaipenda Serikali safi sana.
 
Back
Top Bottom