JAFO ATAKA VIKWAZO KWA VIJANA WENYE UFAULU WA CHINI VIONDOLEWE ILI WAWEZE KUENDELEA NA ELIMU YA JUU

NOKIALUMIA

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
396
275
Pasted

Na Mathew Kwembe, Tabora

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo imezitaka Taasisi zinazosimamia mifumo ya elimu kutoweka vikwazo na masharti magumu kwa vijana wenye ufaulu mdogo kuendelea na kozi mbali mbali katika ngazi ya chuo.

Ametoa kauli hiyo leo wakati akizindua Kitaifa Mpango wa Elimu Changamani kwa vijana walio nje ya Mfumo rasmi wa Elimu (IPOSA).

Jafo alisema kuwakwamisha vijana wenye ufaulu mdogo kuendelea na kozi mbalimbali kwa vigezo vya kuwa na ufaulu wa chini ni kuwanyima vijana haki ya kupata ujuzi.

“Tuache kuweka mifumo yenye roho mbaya inayokwamisha vijana kielimu na ndoto zao za kishiriki uchumi wa viwanda” alisema.

Jafo alisema kuwa wapo watalaamu wanakaa Ofisini na kuweka vigezo ambavyo vinalenga kukwamisha vijana kuendelea na mafunzo yakiwemo ya ufundi na kuwafanya kushindwa kushirikia katika ujenzi wa uchumi wa viwanda

Waziri Jafo aliitaka Taasisi ya Elimu ya watu Wazima kuweka mpango kwa vijana ili waweze kuendelea na vyuo vya juu ili taifa liweze kuwa na wataalam wengi.

Kuhusu Mpango wa Elimu Changamani ( IPOSA) alisema umekuja kujibu kauli ya utekelezaji wa uchumi wa viwanda kwani unajengwa na vijana wenye Maarifa.

Waziri Jafo amewaagiza Wakuu wa Mikoa nane na wilaya zake ambako mpango wa IPOSA unatekelezwa kusimamia ipasavyo na baadae uweze kuenea nchi nzima kama ilivyokusudiwa.

Alisema utekelezaji wa Mpango wa IPOSA usiwe wa zimamoto bali uwe endelevu ili vijana wanufaika waweze kushiriki katika ujenzi wa maendeleo ya Taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jafo alisema kuwakwamisha vijana wenye ufaulu mdogo kuendelea na kozi mbalimbali kwa vigezo vya kuwa na ufaulu wa chini ni kuwanyima vijana haki ya kupata ujuz
Basi ondoa mitihani watu watiririke kama maji mpaka University!
 
Hakuna bado facilities za kutosheleza wanafunzi wote,waliofaulu na wenye ufaulu mdogo,unless serikali I invest heavily kweye elimu.
 
Pasted

Na Mathew Kwembe, Tabora

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Seleman Jafo imezitaka Taasisi zinazosimamia mifumo ya elimu kutoweka vikwazo na masharti magumu kwa vijana wenye ufaulu mdogo kuendelea na kozi mbali mbali katika ngazi ya chuo.

Ametoa kauli hiyo leo wakati akizindua Kitaifa Mpango wa Elimu Changamani kwa vijana walio nje ya Mfumo rasmi wa Elimu (IPOSA).

Jafo alisema kuwakwamisha vijana wenye ufaulu mdogo kuendelea na kozi mbalimbali kwa vigezo vya kuwa na ufaulu wa chini ni kuwanyima vijana haki ya kupata ujuzi.

“Tuache kuweka mifumo yenye roho mbaya inayokwamisha vijana kielimu na ndoto zao za kishiriki uchumi wa viwanda” alisema.

Jafo alisema kuwa wapo watalaamu wanakaa Ofisini na kuweka vigezo ambavyo vinalenga kukwamisha vijana kuendelea na mafunzo yakiwemo ya ufundi na kuwafanya kushindwa kushirikia katika ujenzi wa uchumi wa viwanda

Waziri Jafo aliitaka Taasisi ya Elimu ya watu Wazima kuweka mpango kwa vijana ili waweze kuendelea na vyuo vya juu ili taifa liweze kuwa na wataalam wengi.

Kuhusu Mpango wa Elimu Changamani ( IPOSA) alisema umekuja kujibu kauli ya utekelezaji wa uchumi wa viwanda kwani unajengwa na vijana wenye Maarifa.

Waziri Jafo amewaagiza Wakuu wa Mikoa nane na wilaya zake ambako mpango wa IPOSA unatekelezwa kusimamia ipasavyo na baadae uweze kuenea nchi nzima kama ilivyokusudiwa.

Alisema utekelezaji wa Mpango wa IPOSA usiwe wa zimamoto bali uwe endelevu ili vijana wanufaika waweze kushiriki katika ujenzi wa maendeleo ya Taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Jafo huwa unaeleweka sana ila uko chini ya wenye roho mbaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom