Jafo aagiza walimu wapya walipwe Fedha za kujikimu ndani ya siku 7

Komando tamimy

Senior Member
Nov 18, 2020
108
121
Posho za Kujikimu kwa Ajira Mpya za Walimu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. Selemani Jafo amewaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanawalipa walimu wote wa ajira mpya walioripoti kwenye Halmashauri zao posho za kujikimu ndani ya muda wa wiki moja kuanzia leo tarehe 22/01/2021.

Waziri Jafo ameyasema hayo alipokua akitoa taarifa ya uboreshaji wa shule za Ufundi Tanzania mapema leo Kwenye Ofisi za TAMISEMI Jijini Dodoma.

Hii haingii akilini tangu tarehe 14/12/2020. Mpaka leo 22/01/2021 hao waalimu walikuwa wanaishije?! Ina maana halmshauri ziligoma kuwapa posho zao waalimu mpaka jaffo aseme?!

---

Sasa kama ni hivyo inamaana DED wa halmashauri wanatakiwa watumbuliwe kwa kuwatesa waalimu walimu wapya.Tunasubiria watumbuliwe tuchukue nafasi hizo.

Kaada mtiifu
Kwa sasa niko peramiho
 
Peramiho sehem gan, hospital, kanisani, au maposeni secondary,
Baas sawaaah
 
Nchi hii ina watendaji wabovu sana tena na siasa inaingilia kati basi kila kitu huenda according to politics.
 
Selemani Jafo amewaelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanawalipa walimu wote wa ajira mpya
Serikali ya kiki hii.
Wanatafuta ukoko wa fedha zilizobqkia baada ya kuchotwa na kupekekwa Chatto. Halafu fedha ikipatikana ndiyo wanakuja na Futuhi ya maagizo ya vitisho.
 
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo, ametoa wiki moja kwa halmashauri nchini ambazo hazijawapa fedha za kujikimu walimu wapya, kuhakikisha wanawalipa ndani ya muda huo.

Jafo alitoa agizo hilo jana jijini hapa alipozungumzia uboreshaji wa shule za ufundi nchini.

Alisema mwishoni mwa mwaka jana, serikali iliajiri walimu wapya ambao walipangwa kwenye shule mbalimbali nchini na halmashauri ziliagizwa kulipa fedha za kujikimu kwa wakati pindi watakaporipoti kwenye shule walizopangwa.

Hata hivyo, alisema kuna halmashauri hadi sasa bado hazijawapa fedha hizo na kutoa siku saba kuwalipa walimu hao.

"Sitaki kuona wanafanya kazi wakiwa na msongo wa mawazo, ninatoa wiki moja kwa halmashauri ambazo hazijalipa fedha hizo," aliagiza.
 
Alikuwa wapi watu wameteseka hivi. Naziona siku za Jafo hapo wizarani ni chache saana.
 
Eeeh ina maana fedha za kujikimu mpaka waziri aagize? Na je kama asingeagiza ina maana wasingepata?

Mimi nilijua ni utaratibu au sheria kwamba Mtumishi akiwa anaenda kuripoti kituo kipya/ajira mpya anatakiwa apate fedha za kuanzia maisha?
 
Sasa alishindwa kuwapigia simu au kuwatumia email.
Sisi tusiohusika tunatangaziwa ili iweje?
Haya matamko hayatusaidii chochote.
 
Nimeona niliseme hili kwa kifupi, ili wadau wengine waliona kwa upana zaidi. Haya ni sehemu ya maisha yanayogusa watu, mtu ndo kaanza ajira hana chochote, inakuwaje wakurugenzi na naafisa elimu wakae kimya!?
 
Dogo tulia,
HELA YA SERIKALINI INATOKA KWA UTARATIBU MAALUMU.

Afisa elimu na mkurugenzi ni KAMA SISIMIZI TU.......!
Sasa hao ukiwaendea sijui wewe unakuwa NANI??

Sent from my SM-J700H using JamiiForums mobile app
 
Una uhakika wamepewa fungu? Watu tunapenda kulaumu .
Kama waziri kasema baadhi ya maeneo hawajawalipa na amewape siku saba,huekewi nini hapo?We unaona ni sawa. Kuanza kazuvbila hela ya motisha?usitete ujinga,penyevkweli uongo hujitenga na wala huku sio kulalamika
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom