Jafo aagiza kwa kukamatwa Mfanyabiashara aliyetelekeza makontena ya uchafu Bandarini

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo ameagiza kukamatwa kwa Bw. Kaissy Mkurugenzi wa Kampuni ya Seif for Tobacco Trading Co. Ltd aliyeingiza nchini makontena zaidi ya mia tano (500) yenye malighafi ya Molasesi iliyoharibika na kuyatelekeza katika Bandari ya Dar es Salaam.

Waziri Jafo ameagiza hayo hii leo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam na kushuhudia makontena hayo yakiwa yametelekezwa bandarini hapo na mengine kutawanywa katika baadhi ya bandari kavu jijini Dar es Salaam.

Amesema kamwe Tanzania haiwezi kugeuzwa kuwa dampo kwa kuruhusu bidhaa kutoka nje ya nchi ambazo muda wake wa matumizi umeisha kuingizwa nchini kwa lengo la kutupwa kiholela.

“Ndugu zangu katika kusimamia mazingira hatuna mzaha, afya za binadamu na mimea ni dhamana yetu, sitaruhusu afya za watanzania kuwekwa rehani” Jafo alisisitiza.

Imebainika kuwa mfanyabiashara huyo aliyetambulika kwa jina moja tu la Bw. Kaissy aliingia nchini kwa hati ya utembezi (tourist) na baadae kupatiwa kibali cha uwekezaji kupitia Export Processing Zone (EPZA) kilichomruhusu kuwekeza katika uzalishaji wa shisha kibali ambacho kilifutwa baada ya kugundulika kuwa kuna udanganyifu mkubwa kuhusu uwekezaji wake.

Aidha, Waziri Jafo amemwagiza Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa na Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samwel Gwamaka kufanya kaguzi katika Bandari kavu zote nchini kubaini bidhaa zilizoingizwa nchini zikiwa zimeisha muda wake wa matumizi ambazo zimetelekezwa kwa lengo la kuzitupa nchini na kuchukua hatua za kisheria.

Pia Waziri Jafo amesema NEMC, TBS na Mamlaka ya Bandari ndani ya siku tatu kuwasilisha taarifa ya kina kuhusu mwekezaji huyo na idadi kamili ya makontena yaliyoingizwa nchini na mfanyabiashara huyo.

“Kwa kuwa vipimo vilivyofanywa na TBS vinaonyesha kuwa Molasesi yote imekwisha haribika na ni hatari kwa afya ya binadamu na mazingira, namwagiza mfanyabiashara huyo kurudisha makontena hayo yalikotoka kwa gharama zake mwenyewe” Jafo alisisitiza.

Waziri Jafo pia ametembelea bomba za kusafirishia mafuta kutoka kwenye meli na kubaini uvujaji wa mafuta katika mabomba hayo unaosabishwa na uchakavu wa mitambo hiyo, Waziri Jafo ameagiza hatua za haraka kuchukuliwa kudhibiti uchafuzi wa Mazingira.
 
inaonekana jamaa alitaka anzisha kiwanda cha kuzalisha zile shisha flavors kwa kutumia hizo Molases sasa Kimeumana da! na kwa sababu ni Chemical na inavutwa as Moshi uenda aina madhara,so ilitakiwa serikalibiangalie hili kisayansi bila kukurupuka.Kwa kuwa imshasemwa kuwa ni Shisha malighafi basi waangalie formula inayozalisha SHiSha wajilizishe kama akuna madhara au yapo.kabla ya kuhamuru yarudi yalipotoka
Screenshot_20210503-204034.png
 
inaonekana jamaa alitaka anzisha kiwanda cha kuzalisha zile shisha flavors kwa kutumia hizo Molases sasa Kimeumana da! na kwa sababu ni Chemical na inavutwa as Moshi uenda aina madhara,so ilitakiwa serikalibiangalie hili kisayansi bila kukurupuka.Kwa kuwa imshasemwa kuwa ni Shisha malighafi basi waangalie formula inayozalisha SHiSha wajilizishe kama akuna madhara au yapo.kabla ya kuhamuru yarudi yalipotokaView attachment 1772470
Jafo na Aweso ni wakurupukaji sana.

Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
 
Mademu na mabrazamen mnavuta hayo mashisha mitaa ya small planet tabata kuna ujumbe wenu huku.
 
Hiyo molases ni kwa ajili ya kutengenezea moto wa kuchomea tumbaku hvyoo haina madhara kwenye shisha.
Bwana shisha sijui anasemaje?
 
Hii kesi itaisha kimyakimya na hayo makontena hayaendi popote.

Huyo alieleta kontena 500 hajaleta bahati mbaya. Kuna mkono wa mtu mkubwa.
Kwani ni uongo mkuu?

Kwanza kichefu chefu kinaanzia uhamiaji kinasonga Tbs, Bandari na Takukuru.

Aliingiaje nchini na kisha kupata kibali cha uwekezaji kwa hati za kitalii?

Bidhaa zilizokwisha muda wake zinapataje kibali cha Tbs kuingizwa na kusambazwa nchini?

Bandari wameshindwaje kuibumburusha kashifa hiyo mpaka waziri anuse na kushitukiza ukaguzi?

Takukuru wana kigugumizi gani kutumia hadidu za rejea nilizoziainisha, wakaingia mzigoni na kumfunga paka kengele?

Hapo lazima kuna namna mkuu na huenda hiyo taarifa ikawa ni ya mwisho kwetu sisi raia kuhabarishwa.
 
Poleni, waombolezaji. Tanzania njema yaja, yenye asali na maziwa!
 
Back
Top Bottom