kantalambaz
JF-Expert Member
- Dec 24, 2017
- 1,878
- 872
Hata sasa hivi shule bado zinajengwa naona kinachokosekana ni utashi wa kutosha kwakua inawezekana watoto wa watu wenye maamuzi hawasomi hizo shule hivyo hawana uchungu nazo. Hapa inapaswa kila halmashauri ionyeshe mpango kazi wa kuondoa tatizo la ukosefu wa madarasa, nyumba za waalimu, vyoo, mshahara n.k na ifatiliwe kwa karibu na hatua zichukuliwe pale inapobidi. Ifanyike km kipindi cha Lowassa au kipindi cha JPM kwenye madawati hii itasaidia sana.kina lowassa walipambana kuhakikisha kila mtoto wa kitanzania anapata elimu ya sekondari,walijenga shule kila kata ili watoto wapate nafasi ya kuendelea kupata elimu,awamu yenyewe ina vipaumbele vyake,sio elimu,elimu imeachwa ijiendee yenyewe hakuna wa kujali,matokeo yake ni kutengeneza wahalifu wengi na wajinga wasioweza kupambana kuondoa umasikini katika jamii