Jafari Kubecha aitaka ACT Wazalendo kuteua vijana makini

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Na Mwandishi wetu,
Dodoma

Mjumbe wa halmashauri kuu ya ccm Nec kupitia vijana Jaffari Kubecha amekitaja chama cha Act Wazalendo kiteue watendaji vijana makini wenye maono, upeo na kufanya upambanuzi katika kujadili na kujibu hoja za kisiasa kwa uyakinifu bila kuingilia mambo ambayo aidha hayajathibitika au kutotolewa hukumu na vyombo vya kisheria vilivyotajwa kikatiba .

Pia amekishauri chama hicho kufahamu kuwa kumzungumzia mtu yeyote au ushauri ambalo bado halijatolewa uamuzi au mtu kutiwa hatiani kisheria ni kosa kumtuhumu mtu, kumnanga mbele ya jamii au kutamja kwa nia ya kumvunjia hadhi, utu au kubaribu heshima yake.

Matamshi hayo yametamkwa jana na jafari Kubecha Mnec kupitia UVCCM aliyesema vyama vya upinzani bado vinakabiliwa na tatizo la baadhi ya viongozi wake hususan vijana kuwa na upeo mdogo wa kujua , kupambana na kuielewa dhana ya usimamizi katika mgawanyo wa madaraka na utekelezaji wake.

Kubecha alisema shaka alijibu hoja iliotolewa na upinzani unaotaka yafanyike mabadiliko ya kuandikwa katiba mpya na kuachana na ya mwaka 1977 wakati ambao serikali ilioshinda uchaguzi na kuunda dola ikiwa katika juhudi za utekelezaji wa kisera na kutimiza ahadi za kimaendeleo zilizoahidiwa kwa wananchi.

Alisema jawabu la dai hilo limeelezwa kwa ufafanuzi wa kutosha na katibu wa itikadi na uenezi Shaka Hamdu Shaka ambaye alitoa ushahidi jinsi mchakato wa katiba mpya ulivyoanza, kuundwa kwa tume ya kukusanya maoni , uteuzi wa wabunge hadi kuandikwa katiba iliopendelezwa na bunge maalum la katiba na jinsi ambavyo baadhi ya viongozi wa upinzani walivyoukwamisha mchakato huo.

"Nimeshangazwa na matamshi ya kijana mmoja toka ngome ya vijana ya ACT Wazalendo alivyokosa upeo na maarifa ya kujibu hoja kwa hoja .Badala ya kujibu hoja ameanza porojo na kutamka matamshi yenye viashiria vya jinai. Kuwa Kiongozi wa chama cha siasa bado hujawa polisi, mpelelezi, hakimu au jaji wa mahakama. Hivi Mohamed Rajab mhabeshi amepata wapi nguvu za kumtuhumu Shaka mwizi? "Alihoji Kubecha.

Mnec huyo alisema hata Naibu Katibu mkuu wa Chadema Benson kilagai kitendo chake cha kutoa matamshi yanayoitaka serikali kuwalipa fidia masheikh 36 wa jumuiya ya Uamsho waliokuwa mahabusu kwa miaka minane ni madai yanayokwenda kinyume na dhana ya mgawanyo wa madaraka.

"Kabla hujainuka na kusimama mbele ya kipaza sauti kwanza tafakari unakwenda kusema nini,kwa madhumuni gani na iwapo hutajikwanisha kisheria. Siasa haibatilishi sheria za nchi. Penda kujadili hoja epeuka kuropoka. Kumwita mwenzako mhakufu wakati wewe si mahakama kimantiki na kisheria hiyo ni jinai" Alieleza Mnec huyo.

Kubecha alisema kimsingi katiba iliopo sasa ni katiba bora na makini yenye uwezo na vigezo vinavyojitosheleza kujibu maswali yote magumu unapotokea utata wa kikatiba na kisheria na katiba hiyo haijawahi kupwerewa na kushindwa kuelekeza au kutokikidhi viwango vya matakwa ya ufafanuzi kulingana na mahitaji ya wakati.

'Tumebahatika Tanzania kuwa na katiba ya kizalendo ilioongoza Taifa letu kwa miaka zaidi ya hamsini. Ni katiba iliosimamia na kulinda umoja, utulivu na kujali usawa .Katiba yetu imetuelekeza kila yalipotufika matukio magumu katiba imetulinda ili tusipotee huku ikituonyesha njia sahihi "Alisisitiza Kubecha.

Aidha alisema ni Katiba inyoheshimu misingi ya utawalabora wa sheria, iliojenga jamii yenye uwazi,i kuenzi haki za binadamu , inayothamini utu,haki na kuendesha siasa safi pia ni katiba ilioliweka Taifa letu pamoja na kutambua mantiki ya demokrasia huku kila mmoja akiheshimiwa.

Hata hivyo Kubecha alikieleza ACT Wazalendo kama si juhudi za serikali za ccm za kuweka mbele maslahi ya umma, matokeo ya mikakati ya kisera ,viongozi kama kina zitto kabwe, Juma duni Haji, Freeman Mbowe, James Mbatia na wengine wasingepata elimu iliowapa maarifa ya kuanzisha vyama vya siasa ili kushindana na chama kilicholeta uhuru na ukombozi.

IMG-20210618-WA0043.jpg
 
Kubecha ambaye ni UV-CCM anapinga Mashekhe wa Uamsho kulipwa fidia baada ya kuwekwa kizuizini kwa miaka 9 na serikali kushindwa kuthibitisha tuhuma dhidi yao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom