Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi: Nimezuiwa kuingia kwenye kaburi la mume wangu. Nimechoka na sitakubali

Dejane

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
49,617
68,529
Aliyewahi kuwa Mwanamuziki Nchini na ambaye ni mke wa Marehemu Regnald Mengi, Jacqueline Mengi maarufu kama K-Lyinn amedai kuzuiwa kuingia kwenye kaburi la mumewe, Reginald Mengi

Bila kusema ni nani anaowazungumzia, kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter ameandika “Nimenyamaza kwa mengi sana tu. Mmefikia hatua ya kunizuia mimi na wanangu kuingia kwenye kaburi la mume wangu.”

Ameendela na kuandika “Tunafukuzwa eti mpaka tuombe ruhusa ya kuingia kwenye kaburi la mume na Baba wa watoto wangu. Nimechoka, sitakubali kuendelea kuona wanangu wakisononeka na sitakaa kimya.”

Reginald Mengi ambaye alikuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP alifariki dunia Mei 2, 2019 na kuacha mke (Jacqueline Mengi) na watoto wanne ambao ni Regina, Abdiel, Jayde na Ryan. Watoto hao amezaa na Mercy Mengi pamoja Jackline Mengi

506DB1D5-BB68-4EB4-9CFB-0731E466111E.jpeg


BAADHI YA MAONI YA WADAU:

9FAB185E-C726-455E-8305-E9CE0E3B42EB.jpeg

CE501129-1602-434C-9D1C-323994A255AF.jpeg

54591DAD-D04C-4086-AA17-0FBF984336B3.jpeg

680516C2-11E7-447D-956B-BFA3631AFD1C.jpeg

F9F3265D-ACAE-4E2E-9837-C272354A0E8A.jpeg

8C55B918-1003-45CC-AED2-0E4E73BD9F10.jpeg
 
1.Pesa
2.pesa
3.pesa

Katika ukurasa wake wa Twitter, ameandika hivi;
Nimenyamaza kwa mengi sana tu, mmefikia hatua ya kunizuia mimi na Wanangu kuingia kwenye kaburi la Mume wangu, tunafukuzwa eti mpaka tuombe ruhusa ya kuingia kwenye kaburi la Mume na Baba wa Watoto wangu!, nimechoka, sitakubali kuendelea kuona Wanangu wakisononeka na sitakaa kimya"-Jacqueline Mengi
IMG_20200222_113217.jpg

Jacquiline Ni Mwanamuziki , mfanyabiashara na aliwahi kushinda taji la malkia wa Urembo nchini Tanzania (2000).

Ni Mwanzilishi wa kampuni ya samani ilioshinda tuzo Amorette Ltd .

Babake alitoka kutoka eneo la Kigoma akiwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake huku mamake akiwa nesi.

Alisomea elimu yake ya msingi katika shule ya bweni ya Nyakahoja Primary mjini Mwanza kabla ya kuelekea mjini Dar es Salaam ambapo aliendelea na elimu yake ya msingi katika shule ya Forodhani.

Jackline ni msichana wa mwisho katika familia ya watoto watatu wa kike

Katika utoto wake alikuwa msichana mwenye haya jingi lakini alipendelea sana kusoma vitabu

Muziki
Alianza usanii 1997 akishirikiana na bendi ya Tanzania kwa jina the Tanzanites.

Aliimba kama mmojawapo wa viongozi kwa miaka mitatu.

Mnamo mwaka 2004 alitoa kibao chake 'Nalia kwa Furaha'. akimshirikisha Bushoke

Mwaka 2007 alitoa albamu nyengine kwa jina 'Crazy over You' akimshirikisha Squeezer ambacho kilikuwa kibao cha kwanza cha albamu yake mpya.

Pia aliimba 'Nipe Mkono' akimshirikisha Mr Blue

Anasema kwamba umaarufu wake ulianza alipoanza kuimba

Kulingana na mjasiriamli huyo muziki ndio uliokuwa ndoto yake kubwa akiwa mtoto .

Alitizama kanda za video za wanamuziki tajika kama vile Mariah Carey na Whitney Houston ili kujifunza kuimba

Malkia wa urembo
2000 Alichaguliwa malkia wa Urembo nchini Tanzania baada ya kushinda taji la malkia wa urembo la miss Ilala.

Alitumikia taji la miss Tanzania kwa mwaka mmoja akizishughulikia jamii mbalimbali

Katika kushiriki katika shindano hilo alishawishiwa na mmoja wa waandalizi wa shindano hilo kujaribu bahati yake.

Katika shindano la dunia lililofanyika nchini Uingereza , alikutana na watu tofauti waliokuwa na malengo tofauti ambapo anadai kujifunza mambo mengi tofauti

Tuzo alizoshinda
2007: Alishinda tuzo ya mwanamuziki bora wa kike pamoja Tanzania na kolabo bora kupitia wimbo wake Crazy over you

2007: Alishinda tuzo ya Mwanamuziki bora kutoka Pearl Music Award

2008: Alishinda tuzo nyengine ya mwanamuziki bora wa Tanzania

2008: Alipata tuzo ya Mwanamuziki bora wa kike Tanzania kutoka Pearl Music Awards

2013: Alishinda taji la mwanamke mwenye mitindo bora katika tuzo za fesheni za Swahili

2017: Alijishindia tuzo ya shaba ya kimatifa kwa jina, Sayari amp,

2017: Alijishindia tuzo nyengine ya shaba katika orodha ya samani kwa jina Ngorongoro settee,

Ndoa
Mwaka 2015 alifunga ndoa na Bilionea wa Tanzania Reginald Mengi, na wamejaliwa watoto wawili wavulana .

Marehemu mumewe alikuwa mwenyekiti wa makampuni ya IPP nchini Tanzania

Zaidi, soma: TANZIA: Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Abraham Mengi afariki dunia akiwa Dubai, UA

2). Umoja wa Chama cha Wajane Wamtembelea Bi Jackline Mengi
 
Back
Top Bottom