Jacqueline Ntuyabaliwe acharuka Twitter hatma ya mirathi, aweka nyaraka za hospitali afya ya Reginald Mengi

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,444
7,808
Baada ya hukumu ya mahakama kubatilisha wosia ulioachwa na Reginald Mengi, mjane wake, Jackline amesikitishwa na hali hiyo ikiwemo sababu zilizopelekea mahakama kutokubali wosia huo.

Jackline ameshangazwa na uwezo wa kuandika na kuzindua kitabu kwa mume wake ingali alikuwa na shida ya kiakili. Pia Jackline ameweka rekodi za afya za mume wake katika jitihada za kuthibitishia walimwengu kwamba mume wake alikuwa timamu wakati anaandika wosia.

Jana Mahakama iliwateua watoto wakubwa wa Reginald Mengi kuwa wasimamizi wa mirathi na kutengua wosia unaodaiwa uliandikwa na Reginald Mengi kwa kukosa sifa za kisheria.

Pia, Soma=> Wosia wa Mirathi ya Dkt. Reginald Mengi: Jacqueline Ntuyabaliwe adondokea pua

Jackline.jpg
 
Kuna kesi fulani hivi ilitokea Ulaya.

Mama akiwa anaelekea ukingoni akaandika wosia ana mali za kutosha tu lakini mwanae mmoja akaandika anamuachia dola 1. Huyu mwanae ndiye mchafua mada katika familia, haelewani na kila mtu.

Basi jamaa akaenda mahakamani kupinga huo wosia. Na kumbe sheria inaelekeza mzazi kumuachia urithi mwanae ila haielekezi ni kiasi gani kwa hiyo ingetokea yule mama kaandika wosia na jamaa hajagewa kitu basi hapo ingebidi familia ikae chini kwa agizo la mahakama na kugawana sawa kwa sawa.

Ila kwakua mwenye mali ameshasema anamuachia dola 1 basi hiyo imepita tayari.

Kwa kukumbuka hiyo kesi nafikiri kinachopindua rufaa ya Aunt Jaki ni vile wosia umewacancel watoto wa marehemu utasema hawapo duniani.

Na pia wosia huandikwa kipindi mtu ana afya na akili timamu hivyo inatarajiwa kwamba mwandika wosia atakumbuka kwamba ana watoto now labda hakua na wakili wa kumwambia awaandikie hao watoto chochote kitu lakini nafikiri kesi itaendelea kwenda in favor ya hawa watoto wa marehemu iwe isiwe.
 
Why is she putting some of his medical records in public? What’s to gain from that?

What the F is wrong with her???!!

Personal medical records are supposed to be confidential and not for public consumption! Huyu mwanamke hana adabu, amemvunjia heshima marehemu mumewe; sasa Kila mtu anajua kuwa mzee alikuwa na urinary infection!! Itakusaidia nini to wash your dirty linen in public?
 
Mwili ukiwaka tamaa unazuia uwezo wa ubongo kufanya kazi inavyotakiwa.....msukumo wa moyo unakuwa juu kuliko kawaida.....ikifikia hatua hiyo fahamu zinakaa mbali na mwili....na msukumo wa moyo ndio unaoamrisha matendo ya mwili badala ya akili.......hapo ndipo unapoona mtu anafanya matendo yatakayokuacha kinywa wazi......baada kipindi hicho kupita mwili unarudia hali ya kawaida na kuzaliwa majuto makuu.....huku ukiilaumu nafsi yako........

NB;
A fly that doesn't heed advice, follows the corpse to the grave......
 
Jackline hii kesi hawezi kushinda hata aende court of appeal. R.Mengi hakuwa makini kwenye kuandaa na kuhifadhi wosia wake.

Kama haya ni kweli (hata ukiacha hilo la kuwa/kutokuwa na akili timamu):
1. Kujumuisha mali alizochuma pamoja na mtaliki wake katika wosia.
2. Kutohusisha ndugu katika wosia (ndugu hata mmoja tu anatakiwa ajue kuwa umeandika wosia). Hata sasa hivi ukitaka kuandika wosia kupitia RITA, ndugu ni sharti mojawapo.
3. Kuwanyima urithi baadhi ya watoto wake bila kutoa sababu za msingi na zinazokubalika kisheria.
4. Saini yake kwenye wosia kutofautiana na nyaraka nyingine.
5. Wosia wenyewe kuhifadhiwa na mojawapo ya wenye haki ya kurithi.

Hayo matano, kama yapo hivyo kweli, hakuna namna anaweza kushinda hiyo kesi. Atulie tu, ili apate mgao wake pamoja na wenzake. Akiwavuruga atakosa vyote!
 
Huyu dada anahitaji ushauri wa kina maana asipokuwa makini anaweza kujitengenezea kesi nyingine ya ku- disclose medical records ya mtu in public. Legal matters angezielekeza mahakamani, sometimes seeking Public sympathy kwa mtindo huu ni so cheap
 
Mwili ukiwaka tamaa unazuia uwezo wa ubongo kufanya kazi inavyotakiwa.....msukumo wa moyo unakuwa juu kuliko kawaida.....ikifikia hatua hiyo fahamu zinakaa mbali na mwili....na msukumo wa moyo ndio unaoamrisha matendo ya mwili badala ya akili.......hapo ndipo unapoona mtu anafanya matendo yatakayokuacha kinywa wazi......baada kipindi hicho kupita mwili unarudia hali ya kawaida na kuzaliwa majuto makuu.....huku ukiilaumu nafsi yako........

NB;
A fly that doesn't heed advice, follows the corpse to the grave......
Ameeeeeeen
 
Back
Top Bottom