Jacqueline Mengi: Maneno ya kashfa na kumchafua mume wangu yamesemwa mahakamani, sikubali usuluhishi hadi yakafutwe

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
1,407
2,000
Millard Ayo amekaa na mwanadada Klynn au Jacqueline Ntuyabaliwe na kuzungumzia tweet maarufu aliyoiweka wiki iliyopita.

Fuatilia mahojiano:

Millard: Ulikutanaje na Reginald Mengi?

JNM: Mara ya kwanza tulikutana kwenye ndege. Tulikuwa tunaelekea London. Tulisalimiana na kubadilishana namba.

Millard: Mengi alipohojiwa na Jeff Koinange alidai kwa alikuita London hukutokea. Akawa anakupigia hupokei. Ni kweli na kwanini?

JNM: Kwanza nilikuwa namuogopa halafu nilikuwa nje ya London hivyo nisingeweza kutoka mwenyewe na kwenda London.

Millard: Unauzungumziaje uhusiano wenu?

JNM: Ulikuwa bora kuliko mahusiano yote niliyowahi kuwa nayo maishani mwangu.

DEF4D38B-2C7A-467B-804A-EBC2ADE2CFEA.jpeg


Kwa waliomjua “Reg” alikuwa kijana sana ndani. Tulikuwa tunasafiri sana na kutoka. Tushaenda pamoja show ya Rihanna.

Millard: Alipokutongoza ulitafuta washauri?

JNM: Tulikuwa marafiki kwa muda mrefu wa takribani mwaka 1 kabla ya kuwa wapenzi hivyo sikutafuta mshauri.

Millard: Ulikubali siku hiyo hiyo?

JNM: (Anatabasamu) Sio lazima siku hiyo hiyo ila nilifanya maamuzi mwenyewe.

Millard: Umetimiza miaka 41 hivi karibuni. Je, unatarajia kuolewa tena?

JNM: Ni ngumu kujibu hili swali nikiwa bado nina maumivu ya kufiwa.

Wanasema never say never ila sio lazima kwangu kwani nimeshabarikiwa kupata mume ambaye alikuwa kwa ajili yangu

Millard: Juzi uliandika ujumbe twitter.
ED3DFB5C-F3F4-4743-87A9-8647DFCEFAA5.jpeg
Je, ni mara ya ngapi kuzuiwa?

JNM: Kuzuiwa ni mara ya kwanza ila kuna mengi zaidi ya hilo ndo yamepelekea niandike tweet ile

Shemeji wa mume wangu alifariki hivyo nikaenda na watoto na dada yangu kuzika. Baada ya mazishi nikataka kwenda kuweka maua kwenye kaburi la mume wangu.

Mume wangu amezikwa kwenye makaburi ya familia ambayo yako kwenye nyumba ya familia anapoishi Shemeji yangu Benjamin ambaye ni mdogo wa mwisho wa mume wangu.

Tulienda na kukuta geti limefungwa hivyo tukagonga. Mlinzi akaja na kukataa tusiingie akisema lazima nimuombe Benjamin kuingia. Haijawahi kutokea na tumewahi kwenda mara nyingi hivyo nilipata hasira tukaanza kujibishana.

Iliniuma sana kwa sababu watoto walikuwa wanasikia. Wakaanza kulia. Ilinikwaza sana.

Wakati marehemu mume wangu amefariki tulipata mzozo wa wapi azikwe.

Hatukuwa na nyumba kule Machame hivyo tulikuwa tukienda tunafikia kwenye nyumba ya familia ambapo Benjamin anaishi kwa sababu ndiye mtoto wa mwisho wa kiume. Mume wangu akataka ajenge nyumba ili tukifika tuwe huru.

Baada ya sisi kujenga nyumba yetu, mume wangu aliniambia kuwa anataka azikwe pale.

Baada ya kifo chake nilisema wish ya marehemu ila familia ilipinga. Katika kuepusha shari nilikubali.

Sasa nahisi haya yanatokea kwa sababu sikusikiliza aliyoyataka.

Millard: Unasema umenyamaza kwa mengi. Ni yapi hayo?

JNM: Baada ya Mengi kuumwa Dubai walikuja Regina(mtoto wa kwanza wa marehemu Mengi) na Benjamin

Baada ya mume wangu kufariki moja ya maneno yaliyokuwa yakisemwa ni kuwa mimi ndiye niliyemuua.

Tulikuwa na Balozi wa Tanzania kule na alishauri Benjamin akifika Tanzania azungumzie suala lile kwa ukweli au uongo wake ili “kuclear air” kwa sababu mengi alikuwa mtu wa watu na maneno kama yale ni hatari watu wanaweza hata kuniua

Benjamin alipofika Tanzania hakuzungumza lolote. Ilinikwaza lakini nikapotezea.

Baada ya mazishi wosia wa marehemu ukaletwa ukasomwa tukamaliza. Sikumuona tena Benjamin

Mume wangu alitaja watu 4 wa kusimamia mirathi. Baada ya muda nikasikia Benjamin na mtoto wetu mkubwa wamepinga wosia Mahakamani.

Nilitegemea sisi ni familia hivyo wangekuja tuyazungumze.

Kitu kilichonikwaza ni kwamba lazima unapopinga wosia ueleze sababu; Benjamin ameeleza mambo ambayo kwa jinsi nilivyomjua mume wangu ambaye alifanya kzo hadi mwisho wa maisha yake si ya haki.

Ni maneno ambayo nisingetarajia mtu angeyasema kuhusu mtu aliyefariki ambaye hawezi kujitetea. Sio haki

Millard: Ulitafuta viongozi wa familia?

JNM: Kiongozi wa familia ndiye Benjamin.

Baada ya msiba kwisha niliumwa mguu sikuweza kutembea wiki 3. Katika kipindi hicho waliitisha mkutano wa familia nikawaambia naumwa. Walikutana hivyo hivyo.

Nimewaeleza viongozi wa kanisa. Sina pengine pa kukimbilia.

Millard: Ulisema umechoka, nini umepanga kufanya?

JNM: Nimeamua kuwa nitaongea kama hivi. Wanangu wana umri mdogo sana, miaka 7. Hawakukaa na baba yao kwa muda mrefu. Maneno yaliyoandikwa na uncle wao mahakamani chini ya kiapo ni mabaya na yatawaumiza. Kwa sababu lazima yatakuja kujulikana. Hivyo naongea ili wajue kuwa si ya kweli na mimi kama mama yao nilitumia nafasi yangu kumtetea mume wangu.

Millard: Kesi ya mirathi mahakamani imeisha?

JNM: Haijaisha na mimi wala watoto bado hatujaingia kuwa part ya kesi.

Millard: Kama familia mmekuwa mkipenda sana privacy na kufanya mambo yenu mbali na public eye. Huoni umekosea kwa kuweka tweet ile?

JNM: Mambo yakishaenda mahakamani sio siri tena. Mtu yeyote anaweza kuyaaccess. Familia hukaa na kujadili, mahakama ni last resort.

Millard: Uhusiano wako na watoto wenu wakubwa uko vipi?

JNM: Siwezi kuzungumzia uhusiano wa watoto na baba yao ila mimi nimeishi na Reginald miaka 9. Abdiel alikuwa anakuja mara kwa mara pale nyumbani hivyo nimemzoea. Regina hakuwa anakuja hivyo sikupata namna ya kuzoeana naye.

Millard: Documents zilizovuja mtandaoni zikidaiwa kuwa ndio wosia wa Mengi ambamo hata dada yako ametajwa ni za kweli?

JNM: Mume wangu alikuwa anapenda kusema “Watoto wote ni wangu awe amezaa Jacqueline au Mercy” hivyo alitaka wapate haki sawa. Haki zote walizopata wakubwa kama kusomeshwa na kadhalika alipata wadogo wapate.

Kuhusu Wosia

Nimeulizwa sana na watu private kuhusu wosia. Sijui nini alikuwa anawaza alipoandika wosia ule ila naweza kusema kuhusu maongezi tuliwahi kuwa nayo kama mke na mume.

Alinieleza kuwa baada ya kuachana na mkewe waligawana mali. Sijui ni kwa kiasi gani lakini let us say 50/50. Mkewe alibaki na watoto wawili, hivyo alisema kuwa shares za watoto wakubwa ziko huko ingawa walikuwa na shares zao binafsi. Hata mama yao alipofariki wao ndio warithi. Hivyo wameshapata mgao wao.

Ule wosia uliosambaa mtandaoni ndio wosia halisi ambao tuliufungua.

Wosia unasema share zake zote zilizobakia katika kampuni alizokuwa nazo akiwa kwenye ndoa ya kwanza zigawanywe kati ya mapacha wetu.

Zile za makampuni aliyoanzisha baada ya kutengana na mkewe zigawiwe kwangu na wanetu wawili (Jaden na Ryan).

Millard: Ni kweli umepata asilimia 50 ya mali?

JNM: Hapana

Millard: Lakini inasemekana amekuachia sehemu kubwa sana ya mali zake na kwamba uliinfluence hilo

JNM: Mimi na Reginald hatukuwahi kuzungumzia urithi. Ukiishi na mtu unayempenda, the last thing unataka kuongelea ni yeye kufa. Sikuwahi kumuuliza eti ukifa itakuwaje kwani sikujua yupi kati yetu atatangulia.

Millard: Wakati kesi ya mirathi inaendelea mahakamani, ni vitu gani unasimamia hivi sasa?

JNM: Hakuna hata kitu kimoja ninachosimamia. Vinasimamiwa na watoto wetu wakubwa.

Millard: Kuna maneno yanazunguka kuwa umekataa kufanya usuluhishi. Ni kweli?

JNM: Wakati mume wangu yuko hai sikuwahi kujua kuhusu mgogoro wowote. Baada ya kufariki na wao kwenda mahakamani kuna watu wamenifuata. Wengine ni marafiki wakubwa wa marehemu. Nimekuwa nikisema napenda kupatana ila kabla ya kupatana, yake maneno yaliyozungumzwa kuhusu Reginald akiwa yuko kaburini hawezi kujitetea yafutwe na yaondolewe.

Mume wangu ambaye alijiheshimu, alijijengea jina lake na kufanya kazi miaka yote hadi karibu na kifo chake eti sababu ya mali achafuliwe akiwa hawezi kujitetea? Siwezi kukubali na mtu pekee wa kumtetea ni mimi.

Mali igombewe ila sioni sababu ya kumchafua mume wangu.
Millard: Ukweli wa yaliyotokea Dubai ni upi? Inadaiwa ulimpeleka Mengi kwenye hospitali ambayo si ile anayotibiwa kila mara

JNM: Mume wangu hakuwahi kutibiwa Dubai. Alikuwa na umri ulioenda lakini hakuwa mtu wa kuugua mara kwa mara. Alianguka ghafla tukiwa hotelini na tukaelekezwa na wafanyakazi wa hoteli hospitali ya kumpeleka. Hivyo huo ni uongo!

Millard: Ni mara ya ngapi mlikuwa mnaenda Dubai?

JNM: Mara nyingi tumeenda huko. Hata engagement yetu ilikuwa Dubai. Hata new year 2019 tulikuwa huko.

Millard: Kuna taarifa zilisambaa kuwa ulikuwa na uhusiano na jamaa fulani ambaye ni kijana sana na kwamba huku ulikuwa kwa ajili ya ndoa tu ila moyo wako ulikuwa kwa huyu kijana

JNM: Haya maneno yamesemwa baada ya mume wangu kufariki. Nikabaki najiuliza why yasisemwe akiwa hai kama kweli hao watu waligundua?

Millard: Unamfahamu huyo jamaa?

JNM: Namfahamu. Ni mtu anafahamika mjini.

Millard: Una mawasiliano naye?

JNM: Namfahamu miaka mingi, ni mtu ameishi Tanzania miaka mingi. Alikuwa Darling enzi hizo wanafadhili show za urembo. Sijawahi kuwa kwenye mahusiano naye

Millard: Baada ya uvumi huo alikutafuta?

JNM: Hapana. Hatuna uhusiano wa namna hiyo wa kutafutana.

Millard: Comments za mtandaoni zina effects gani kwako?

JNM: Nilivyoanza uhusiano na mume wangu yalizungumzwa mengi sana. Ila mimi ni public figure huwa napuuza. Kuna mambo yanaumiza.

Nilivyopoteza mume nilipoteza kila kitu. Nilikutana na Reginald wakati baba yangu anaelekea kufariki. Yeye ndo alinizuia nisijiue baada ya baba kufariki. Alikuwa Mume, Baba, Rafiki na kila kitu.

Hivyo maneno haya wakati amefariki sikujali wala kuelewa kwa sababu hakuna maumivu yangezidi yale niliyokuwa nayo. Nilikuja kuyaelewa baadae sana. Nimeamini kuna binadamu wana roho mbaya.

Millard: Umewahi kujiuliza kwanini wakuhusishe na jamaa huyo out of nowhere?

JNM: Nisingependa kujihangaisha na kile kitu. Watu hawana jema, leo hili, kesho lile. Hivyo nimeaccept tu labda ni chuki au kuna sababu nyingine.

Millard: Ikitokea kwenye kesi hujapata kiasi fulani kikubwa cha mali itakudisturb?

JNM: Kinachonidisturb ni namna jina la mume wangu linavyokashifiwa. Kwanza mali yenyewe si kwamba nyumba moja inakatwa katikati, ipo mali ya kutosha sana.

Kinachouma ni kuwa aliyezitafuta anakashifiwa na kuchafuliwa.

Millard: Suala la dada yako kutajwa kwenye mirathi hujalizungumzia

JNM: Mume wangu alitaja wasimamizi 4 wa mirathi ambao wawili ni ndugu na wawili ni wa kwenye kampuni. Dada yangu aliwekwa kama reserve endapo mmoja kati ya waliotajwa atakataa nafasi au kufariki.

Millard: Unasema mumeo alikusaidia usijiue kipindi baba yako amefariki?

JNM: Baba yangu alikuwa kila kitu kwangu, sikuwa na watoto wakati huo. Alipofariki sikutaka kuishi bila yeye. Mume wangu alinisaidia kupita kipindi kile kigumu. Na pia 2012 alinipa watoto. Nawapenda wanangu na wananipa sababu ya kuishi.

Mimi na baba yao tuwapenda sana na tulitaka watimize ndoto zao na watimize ndoto zetu kwao.

Millard: Ni kweli wanasomea nyumbani?

JNM: Hapana. Wanaenda shuleni.

Millard: Nani kimbilio lako katika magumu unayopitia?

JNM: Huwa naongea na dada yangu, sometimes nakaa kimya, sometimes naongea na marafiki. Nina marafiki wanajali sana, hata nisiposema lolote huwa wanakuja kukaa na mimi.

Millard: Nyumba mliyojenga Machame bado una access nayo?

JNM: Ndio. Mume wangu aliniruhusu kusimamia ujenzi. Nilitimiza ndoto zangu katika ile nyumba.

Millard: Ni kweli mzee alikuwa hana pesa akataka muende Zanzibar lakini ukaforce muende Dubai?

JNM: Maisha ya mume na mke ni private lakini nadhani ukiwa maarufu watu watataka kuingia hadi ndani kwenu.

Safari ile ilikuwa kwa ajili ya watoto. Reginald aliwapenda sana watoto. Alitaka kila wakiwa likizo tusafiri. Tulienda Zanzibar ila akahisi hawakuenjoy vilivyo kwani tulikuwa sehemu ya kimya sana. Akasema twende Dubai ili waenjoy zaidi. It was his idea.

Millard: Wewe ni mke wa bilionea. Je, unaenjoy maisha kama watu wanavyodhani?

JNM: Siwezi jua wanadhani nini hivyo siwezi kuzungumzia hilo

Millard: Wanadhani unakula bata siku nzima

JNM: Mimi ni mama hivyo ukiwa mama una majukumu mengi. Napenda kuongea, kucheza na wanangu. Muda wangu mwingi ni kwa ajili yao.

Baada ya hapa walifanya chitchat za hapa na pale.

===== END=====​
 

Raynavero

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
37,147
2,000
Amesema hayo mbele ya mwanahabari Millard Ayo kua hatokaa kwenye meza ya usuluhishi na ndugu wa mume mpk wakae wafute kashfa zao mahakamani walizomkashifu marehemu mume wake kwani hana MTU wa kumtetea zaidi yake yeye kwa kua ameshakufa hatosema tena wala kujitetea.

Ameongelea Mengi lakini kubwa ni kua wamsafishe jina lake na jina lake libaki kama Reginald Mengi na si hvyo ambavyo wao wanamkashifu.

Na pia amesema Mengi ndo alimfanya asijiue baada ya kufiwa na baba yake mwaka2010 maana alikua nae bega kwa bega.

Pia amedai kua kesi itaendelea Tarehe 9 mwezi ujao 2020!!

Haya mambo ndo yameanza upyaa maana naona dada kaamua kujilipua ila msema peke siku zote hushinda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Somoche

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
4,445
2,000
Bi dada atakua anapotoshwa na jamaa mwenye njaa..ambae hatakua na msaada kwake katika hali hii iliyopo.Suala hili angelipeleka kwenye ukoo wakubaliane Kutumia wajanja wenye njaa sioni kama litafanikiwa.

Bi dada lazima aelewe hapa kutaibuka mawakili na wengineo wengi wakifukuzia hela tu awalipe kwasababu ni wanufaika na gogoro hili
 

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
3,944
2,000
Case hii k lyn ana nafasi kubwa sana ya kushinda.. ndio maana anakomaa iamuliwe na mahakama sio na vikao vya ndugu nje ya mahakama..

Hoja za mzee Mengi alichanganyikiwa.. itahitaji ripoti ya hospitali. Hapo ndipo patamu
 

Makiseo

JF-Expert Member
Aug 12, 2015
1,215
2,000
Huyu mzee many naye alibugi kuishi naye
Kumbuka ashaishi na knje tena Akaishi na yule mafi@ wa kibulgaria aliyetimuliwa nchn
Ngj niishie hapa

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu Dada Unaambiwa kwa Muonekano wa Nje unaweza kudhani Malaika.. Wanaomfahamu Wanakwambia ni Mafia hakuna.

Unakumbuka kile kipindi Alienda Kubatiza Watoto Machame? Na Mama Mercy alikuwepo kipindi hicho.Unaambiwa mambo aliyoyafanya Huko hayaelezeki.

Wazee wa Kichagga wakawa Wanaongelea Pembeni tu.. Ila Kumshauri mzee Mengi wakawa Hawawezi kwani yeye ndiyo kashika kwenye Mpini.

Na Haya anayoyapitia Sasa ni Ile Wanaita "KARMA"Hana namna hicho kikombe lazima akinywee tu. Maana hata Kina Regina walikosa Upendo wa Baba yao Punde tu baada ya Jack kuanza kuwa na Mzee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom