Jacob Zuma amwaga pongezi kwa CCM na Mwl Nyerere

Mcheza Karate

JF-Expert Member
Jun 30, 2011
690
350
Wakati chama cha ANC cha Afrika kusini kikisherehea siku yake ya kuzaliwa matukio mawili muhimu kwangu nimeona. Mosi ni Rais wa zamani Thabu Mbeki kuhudhuria sherehe hizo kwa mara ya kwanza tangu aondolewe madarakani mwaka 2007, kitendo kilichomfanya rais Zuma alipokuwa anahutubia amtaje mara mbili kuwa "Mbeki amehudhuria leo". Tukio la pilh ni rais Jacob Zuma kumwaga pongezi kwa chama cha mapinduzi na MWL, NYERERE kwa kuwapa ANC makazi Morogoro wakati wakipigania Uhuru. Hakika nimeamini Nyerere hajafa. Fikra na mchango wake unaonekana. Hili ni somo kwa viongozi wetu wengine kama JK.
 
Hata mimi nimeisikia hii BBC Swahili asubuhi hii!. Thanks Mcheza Karate!
 
Nyerere Julius(nabii hasifiki kwao)ila ukweli Utabaki palepale Hakika ni zaidi ya baba wa Taifa.
 
vipi hajamtaja Sh_mb0 kwa kulisaidia fedha lao kifedha!

Vipi kuhusu kina Skyes manake ni wa Kule Faiza F kama hajatajwa atajisikia vibaya sana!
 
Baba aliyegawa chakula kwa majirani wakati watoto wake wana njaa!

mh! Kijana pana ukweli ndani yake. Uliza mjamaa kauza kwa shekeli ngapi NBC kwa makaburu? Ukipata jibu utajua jamaa alikuwa hamnazo. Halafu wenzao leo hata kumshukuru hamna. Wanamshukuru mwl. tu, atajisikia huzuni sana kwani amejipendekeza kwa mume ambaye hapendi yeye ila dada yake japo alikuwa si mrembo kama yeye.
 
Tulitumia rasilimali nyingi sana kusaidia ukombozi wa Afrika Kusini, matokeo yake wanakuja kutuibia!
 
Wakati chama cha ANC cha Afrika kusini kikisherehea siku yake ya kuzaliwa matukio mawili muhimu kwangu nimeona. Mosi ni Rais wa zamani Thabu Mbeki kuhudhuria sherehe hizo kwa mara ya kwanza tangu aondolewe madarakani mwaka 2007, kitendo kilichomfanya rais Zuma alipokuwa anahutubia amtaje mara mbili kuwa "Mbeki amehudhuria leo". Tukio la pilh ni rais Jacob Zuma kumwaga pongezi kwa chama cha mapinduzi na MWL, NYERERE kwa kuwapa ANC makazi Morogoro wakati wakipigania Uhuru. Hakika nimeamini Nyerere hajafa. Fikra na mchango wake unaonekana. Hili ni somo kwa viongozi wetu wengine kama JK.

Tahadhari hapo kwenye
red; kuna hatari ya "manyang'au" wa kisiasa kuidaka hiyo! Ilikuwa CCM ya Mwl. Nyerere na sio hii ya MAFISADI na wavaa MAGAMBA. Hili ni muhimu mno kuzingatia.
 
Nafarijika kuona Nyerere ana enziwa na kukumbukwa na Afrika japo hapa nchini kuna washenzi wachache wameeanza mkakati wa kumtukanikisha, kumdhihaki na kutaka kutuaminisha alikuwa the worst president ila wanafanya haya kwa malengo yao binafsi, wanafanya haya kwa kuutaka uraisi na Nyerere as good reference in this country alishawakataa na sasa wanataka kufuta hii reference yetu
 
... Tukio la pilh ni rais Jacob Zuma kumwaga pongezi kwa chama cha mapinduzi na MWL, NYERERE kwa kuwapa ANC makazi Morogoro wakati wakipigania Uhuru. Hakika nimeamini Nyerere hajafa. Fikra na mchango wake unaonekana. Hili ni somo kwa viongozi wetu wengine kama JK.

Tahadhari hapo kwenye
red; kuna hatari ya "manyang'au" wa kisiasa kuidaka hiyo! Ilikuwa CCM ya Mwl. Nyerere na sio hii ya MAFISADI na wavaa MAGAMBA. Hili ni muhimu mno kuzingatia.

ASANTE KWA TAHADHARI Dudus, Nyerere is the best president of Tz todate. Hata watu wamfitini lakini vitendo vyake vinamtenga mbali na ubaya usemwao juu yake. Hii haimaanishi hakuwa na mapungufu, hilo ni fungu la wote. Lakini wingi wa mema aloyafanya unamtofautisha na wenzie.
Ilikuwa ccm ya Nyerere, uko sawa kabisa. Na ndo mana walimpoanza kukorofisha na akaona kuwa wanakwenda kinyume na matarajiio ya wananchi yeye mwenyewe akasema NAWEZA KUTOKA, CCM SIO MAMA YANGU.
Ole wetu na viongozi hawa, wana mahali pa kuchukulia mfano lakini wanajifanya hawaoni, wamebaki na mayowe ya "tumuenzi Mwalimu Nyerere"! Wanatuambia mengine na wao wanafanya mengine kabisa. AIBU TUPU!
 
Lakini wadau nimesikia siku zote eti JK hamwiti baba wa taifa ila "MZEE NYERERE" au akionaje anau soo, " BABA WA TAIFA LETU". Kisa hakuwa "the best kwa mwalimu".
 
Back
Top Bottom