Jacob Koda sasa ni askofu jimbo gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jacob Koda sasa ni askofu jimbo gani?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ByaseL, Jun 15, 2009.

 1. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  [​IMG]


  Na Joseph Misango

  ASKOFU Jacques Gaillot wa Ufaransa alijulikana kama Askofu wa Jimbo la Evreux tangu mwaka 1982. Ulaya ilishuhudia ugomvi wake na Vatican wa muda mrefu na ambao haukuwa ukijificha machoni mwa watu.

  Januari 12, 1995 aliwaambia waandishi kwamba kaambiwa na Vatican kuwa jimbo la Evreux si lake tena. Liko wazi likisubiri askofu mwingine. Haikushangaza, kuondolewa kwake Evreux. Kilichoshangaza ni kukamilisha hiyo taarifa yake kwa sahihi iliyoonyesha yeye sasa ni askofu wa jimbo la Parthenia.

  Baadhi wakashangaa Papa John Paul II kumpa askofu huyu jimbo jingine. Je, Papa haoni yaliyotokea Evreux yatajirudia Parthenia?


  Wakaanza kulidadisi kulijua hili jimbo Parthenia atakalohamia Askofu Gaillot. Wakagundua liko katikati ya jangwa la Sahara. Liliteketea karne ya tano kwa kufunikwa na mchanga mkubwa wa jangwani (sand dunes). Kumbe ni nadharia tu, kiuhalisi jimbo hilo halipo. Hivyo, Gaillot ni Askofu wa hiyo Parthenia, lakini kivitendo hana eneo la kutawala wala wanajimbo.


  Sebuleni nina picha kubwa iliyotengenezwa na Baraza la Maaskofu (TEC). Ina ramani ya Tanzania yenye picha ndogo za kila askofu katika jimbo lake. Pia ina picha za mapapa sita, maaskofu wa zamani (Emeritus) na Balozi wa Papa nchini (Askofu Mkuu Joseph Chennoth).


  Marafiki walionitembelea iliwavutia. Mmoja aliyeiona (si mkatoliki) aliniuliza “mbona Dar es Salaam ina maaskofu wawili”? Nikamjibu uwezekano wa maaskofu wengi jimboni. Alipomtazama Balozi wa Papa akaniuliza tena “mbona askofu huyu hana jimbo?”.

  Nikamfafanulia dhana ya majimbo yanayoitwa Titular Diocese na kwamba maaskofu wa majimbo haya wanajulikana kama Titular Bishop akiwemo Balozi wa Papa. Nilijilaumu kutomfafanulia mapema alipouliza Dar es Salaam yenye maaskofu wawili.


  Wakatoliki wenzangu wakaibua mjadala mkali tulioutuliza kwa kurejea vifungu kwenye kitabu chenye Sheria za Kanisa yaani “New Commentary On The Code of Canon Laws” kilichotolewa na “The Canon Law Society of America” na kuchapishwa India mwaka 2003. Sijaelewa kwa nini mjadala wa Titular Bishops huzaa ubishi kidogo lakini kila mmoja ana haki ya kuielewa dhana hiyo si jambo la siri.

  Tumeona hata Ulaya walivyoshtushwa Gaillot kupewa jimbo jingine yaani Parthenia. Walioshangaa ni wale ambao hawakujua kwamba hii Parthenia ni Titular Diocese.
  Je, Titular Diocese au Titular See ni nini? Sijajua niyaiteje kwa kiswahili. Lakini ni majimbo yaliyokuwepo kale kama yalivyo majimbo yetu ya sasa. Ushamiri wake umepotea kwa sababu kadhaa kama vita au kubadili jina. Yako sehemu mbalimbali duniani. Sikuwahi kuyasikia hapa Tanzania. Lakini mitandao imeshatutangazia kuwa Januari mwaka huu tumepata mawili yaani Nachingwea na Rutabo (Rejea: Changes in Ecclesiastical Circumscriptions (2009)). Nachingwea ndiyo iliyobadilika kuwa Lindi kama Rutabo ilivyobadilika kuwa Bukoba. Hivyo, ni kama yamefufuka lakini sasa ni Titular Diocese au Titular See. Yote mawili yako wazi hayajapata Askofu.

  Askofu wenye majimbo tunayoishi kama Mwanza (Mayala), Same (alivyokuwa Koda) huitwa Diocesan Bishop (Askofu wa Jimbo). Wasio na majimbo hujulikana kama Titular Bishop na hivyo hupewa moja ya hizi Titular Diocese au Titular See.


  Hivyo kiuhalisia kila askofu duniani ana jimbo la uaskofu wake. Haipaswi jimbo liwe na maaskofu wawili au awepo askofu asiye na jimbo. Nashauri msomaji upitie kifungu 376 cha sheria za Kanisa kinachobainisha mgawanyo huu (Can. 376). Kuondoka kwa Jacob Koda, kunaifanya Tanzania ya majimbo 31 ibaki na maaskofu 30 wa majimbo.

  Sasa tujadili aina hii ya maaskofu wasio wa majimbo yaani Titular Bishops kuanzia aya ifuatayo. Zamani wote wasiomiliki jimbo waliitwaTitular Bishop wakiwemo waandamizi (Coadjutor) na Bishop Emeritus (wastaafu). Kustaafu, kulimfanya aliyekuwa wa jimbo kuwa Titular Bishop na kupewa Titular Diocese.

  Papa Paul VI alirekebisha kwamba wastaafu au wanaojiuzulu jimboni hawatapewa tena Titular Diocese. Kwamba watambulike kwa majimbo waliyokuwemo (Bishop Emeritus). Wa aina hii ni Lukanima (Arusha), Msarikie (Moshi), Isuja (Dodoma), Nkalanga (Bukoba), Mwanyika (Njombe), Shija (Kahama) na Mwalunyungu (Tunduru-Masasi).

  Pia askofu mwandamizi (Coadjutor Bishop) waliacha kuwa Titular Bishop. Walianza kuitwa kwa majimbo waliyomo. Hawa wana haki ya kurithi jimbo{Sheria: Can. 409(1) na Can. 416}. Mfano ni Polycarp Pengo (Mwandamizi) alivyoirithi Dar es Salaam siku alipostaafu Kadinali Rugambwa.


  Tumejadili wajulikanao kwa majimbo yetu. Sasa tunawajadili (Titular Bishop) wanaofanya kazi kwenye majimbo yetu lakini majimbo ya uaskofu wao (Titular See) yaweza kuwa nchi nyingine tofauti.

  Askofu msaidizi ni aina moja ya Titular Bisshop. Methodius Kilaini wa Dar es Salaam jimbo lake ni Strumnitza yaani Titular Bishop of Strumnitza (Askofu wa Strumnitza). Nadhani ni ile Strumnitza iliyotekwa vitani mara na Bulgaria, Uturuki na Macedonia. Askofu wasaidizi hawa, hawana haki ya kurithi jimbo kama wenzao Coadjutor (waandamizi) { Sheria: Can. 403(1)}.


  Titular Bishop wengine ni Mabalozi wa Papa (Apostolic Nuncios). Majimbo yao mara nyingi huwa majimbo makuu (Titular Archdiocese). Joseph Chennoth aliyepo nchini, jimbo lake huitwa Titular Archdiocese of Milevum. Hivyo anaitwa Askofu Mkuu wa Milevum (Titular Archbishop of Milevum).


  Kuna wanaokuwa Vicars Apostolic. Wanaongoza Apostolic Vicariate (Vikarieti) ambayo haijawa diocese au jimbo (Can. 371(1)). Laurian Rugambwa alianza uaskofu kwa mtindo huu kama Vicar Apostolic wa Kagera-Inferiore (Kagera-Chini). Alikuwa Titular Bishop of Febiana (Askofu wa Febiana). Kagera-Chini lipandishwa hadhi kuwa jimbo la Rutabo. Ndipo Laurian Rugambwa akawa askofu wa jimbo (Deocesan Bishop). Akaachana na ile hadhi ya Askofu wa Febiana iliyomshika kwa siku 468. Febiana aliyoachana nayo ikampata Antonio de Campos, Askofu Msaidizi wa Lisboa (Ureno).


  Titular Bishops wengine wako Vatican kwenye idara za kanisa (Roman Curia). Askofu Mkuu Fortunato Baldelli ni mkuu wa moja ya mahakama kuu za kanisa (Apostolic Penitentiary). Jimbo la uaskofu wake ni Mevania yaani Titular Archbishop of Mevania(Askofu Mkuu wa Mevania).

  Hapo hapo Vatican, mahakama nyingine (Roman Rota) inaongozwa na Askofu Antoni Stankiewicz yaani Titular Bishop of Nova Petra (Askofu wa Nova).


  Titular Bishop wengine ni wale wanaoongoza vikundi (Personal Prelatures) vya kanisa vyenye wafuasi waliosambaa duniani. Askofu Javier Echevarría Rodríguez anaongoza kikundi kiitwacho Opus Dei. Yeye ni Titular Bishop of Cilibia (Askofu wa Cilibi).

  Kanisa liliwahi kutoa uaskofu kwa watawa wa kiume (Territorial abbots) kwenye maeneo waliyokuwa kikundi pekee cha mapadri (Can. 370). Mwaka 1933 Ndanda ilimpata Askofu Joachim Ammann, mkuu wa abasia hiyo akijulikana kama Titular Bishop of Petnelissus (Askofu wa Petnelissus).

  Husemwa kwamba hata makadinali sita (Cardinal Bishops) walioko Vatican , huwekwa katika kundi hili. Kwani kila mmoja ana kanisa jijini Roma (suburbicarian see) kama ishara ya jimbo. Mkuu wa jopo la makadinali duniani (Dean of Cardinals) anaongezewa moja (Ostia) hivyo kuyafanya yawe makanisa saba.


  Tumeona Titular Bishops wengi wamekabidhiwa majukumu. Tulipomjadili Askofu Jacques Gaillot tumeona kuwa kumbe askofu anaweza kuondolewa jimboni, akapewa Titular Diocese. Kwa njia hiyo anabaki kuwa askofu asiye na jukumu lolote.

  Lakini kwa Gaillot ilileta kitu kisichotarajiwa. Badala ya kunyamaza alihamishia maoni yake kwenye mtandao hadi tovuti yake ikaitwa cyber-diocese au jimbo jipya mtandaoni.

  Mjadala kuhusu Jacob Koda huenda haujaisha. Balozi wa Papa keshaeleza kilichomuondoa basi inatosha. Hata hivyo mitandaoni waweza kushuhudia maoni mengi. Pengine kilichomuondoa Koda ni kingine kabisa kana kwamba taarifa ya Balozi Chennoth ilikuwa ni kichwa cha habari na habari kamili wanayo wao.


  Kuwazuia hawa si rahisi maana hatutazuia simu zao kusambaza mawazo yao kona zote wanazotaka. Kama hatutawapuuza basi nadhani hawa tuwakaribishe kwenye mjadala kama makala hii. Ukizingatia makala yangu utagundua cha msingi sasa ni kujua hatima ya Askofu Jacob Koda kulingana na sheria za Kanisa zinazoongoza wakatoliki walio kwenye ushirika na Papa (Communion with the Holy See). Sikujua kama wengi mnajua niliyoyajadili, hasa ile dhana ya Titular Bishop. Ningejua mnajua, makala ningeifupisha kwa maswali matatu tu yafuatayo:

  1: Je Askofu Jacob Koda sasa amekuwa Titular Bishop na kupewa Titular Diocese kama Askofu Jacques Gaillot?

  2: Je, sasa amekuwa Bishop Emeritus (mstaafu) wa jimbo la Same kama ilivyokuwa Askofu Pius Ncube wa Bulawayo mwaka juzi?

  3: Je ameondolewa kabisa utumishini (laicization) ajichagulie shughuli binafsi kama Askofu Fernando Lugo ambaye sasa ni Rais wa Paraguay?

  Nimekomea kwenye haya matatu maana sijaona dalili kwamba labda ametengwa (excommunicated) hata akakosa Titular Diocese kama alivyotengwa Askofu Marcel Lefebvre na wenzake wa SSPX mwaka 1988.
   
 2. Maxence Melo

  Maxence Melo JF Founder Staff Member

  #2
  Apr 21, 2010
  Joined: Feb 10, 2006
  Messages: 2,606
  Likes Received: 1,701
  Trophy Points: 280
  April 21, 2010

  The Vatican has removed from office Bishop Jakob Koda of Same Catholic Diocese in Kilimanjaro region for alleged violation of church moral teachings.

  The Vatican Apostolic Nuncio to Tanzania, Archbishop Joseph Chennoth told the Daily News in Dar es Salaam that Bishop Koda has now been “advised to take time for rest, reflection and personal study”.

  Elaborating

  Following Bishop Koda’s removal, Pope Benedict XVI has appointed Father Rogath Kimaryo to be Apostolic Administrator of the Same Catholic diocese until the diocese gets a new bishop.

  Father Kimaryo, who was until recently the parish priest of Kipawa Parish in Dar es Salaam will be “authorised” tomorrow during Mass at Same Cathedral Church, to be presided over by Cardinal Polycarp Pengo.

  Without elaborating, Archbishop Chennoth said that the Catholic Church normally grants such occasion to its leaders when necessary.

  “We have advised him to leave the Diocese, and Father Kimaryo will lead the See for a short while, until the Holy Father announces (the appointment of) a new bishop,” he said.

  Pope John Paul II nominated Koda as the new bishop of Same in September 1999.

  Father Kimaryo, who is a member of the Holy Ghost Fathers’ congregation, holds a doctorate in Law, from the Rome-based Pontifical Gregorian University.

  An Apostolic Administrator in the Roman Catholic Church is a prelate appointed by the Pope to serve as the ordinary. (CISA)


  Source:
  Daily Nation
   
 3. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #3
  Apr 21, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,564
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  Mmh! Pope at work! Mara nyingi tuhuma za watuhumiwa huwa hazijulikani mpaka hali iwe tete kabisa. Anyway, kama Askofu aliapa kulinda sheria ambzo anajua kabisa hataziweza, then Pope is right. Kama Askofu anaona kuna kitu sio right kinahitaji mabadiliko then alipaswa kutafuta mbinu mbadala. Hakuna anayepambana na R.C akawa salama!
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Hii ni ya mwaka jana jamani only that jana ndo Balozo wa papa huko Tz alihojiwa na media. But msimamizi wa jimbo la Same yuko kazini mwaka na zaidi kwa sasa. Kaka Max, asante kwa thread!
   
 5. N

  Nandoa Member

  #5
  Apr 21, 2010
  Joined: Mar 22, 2009
  Messages: 68
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Huyo askofu ameshajiuzulu uaskofu na Papa ameridhia (nadhani walimweleza afanye hivyo)
   
 6. J

  Jafar JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Vatican sacks Tanzanian bishop Posted: Wednesday, April 21, 2010 3:33 pm
  [​IMG] Email [​IMG] Print [​IMG]
  [​IMG]
  Bishop Koda The Vatican has removed from office Bishop Jacob Koda of Same Catholic Diocese in Kilimanjaro region for alleged violation of church moral teachings.

  The Vatican Apostolic Nuncio to Tanzania Archbishop Joseph Chennoth told the 'Daily News' in Dar es Salaam yesterday that Bishop Koda has now been ‘advised to take time for rest, reflection and personal study.’ Following Bishop Koda’s removal, Archbishop Chennoth said that the Holy Father, Pope Benedict XVI has appointed Father Rogath Kimaryo CSSp to be Apostolic Administrator of the Same Catholic diocese until the diocese gets a new bishop.

  Father Kimaryo, who was until recently the parish priest of Kipawa Parish in Dar Es Salaam will be ‘authorised’ tomorrow during Holy Mass at Same Cathedral Church, to be presided over by Cardinal Polycarp Pengo.

  Archbishop Chennoth will also attend the liturgy. Without elaborating, Archbishop Chennoth said that the Catholic Church normally grants such occasion to its leaders ‘when necessary.’ "We have advised him to leave the Diocese, and Father Kimaryo will lead the See for a short while, until the Holy Father announces (the appointment of) a new bishop" he said.

  Pope John Paul II nominated Koda as the new bishop of Same in September 1999, to succeed Bishop Josaphat Louis Lebulu who had been transferred to Arusha Archdiocese the previous year.Father Kimaryo who is a member of the Holy Ghost Fathers’ congregation holds a doctorate in Law, obtained from the Rome-based Pontifical Gregorian University. He has also worked at the General House of his Order in Rome for six years as Counsellor.

  According to the Catholic teachings, an Apostolic Administrator in the Roman Catholic Church is a prelate appointed by the Pope to serve as the ordinary. He can either be in an area that is not yet a diocese (a stable apostolic administration) or for a diocese that either has no bishop (an apostolic administrator sede vacante) or, in very rare cases, has an incapacitated bishop (apostolic administrator sede plena).

  Strictly in Canon Law, An Apostolic Administrator is equivalent to a diocesan bishop, meaning he has essentially the same authority as a diocesan bishop, serving in their role until a newly chosen diocesan bishop takes possession of the diocese. However, he is restricted by the Canon Law in what he can do to the diocese he temporarily administers. For example, an administrator may not sell real estate owned by the diocese.

  The Daily News has asked the Church to explain to parishioners why their bishop has been removed. "We think we deserve some explanation" a spokesman said.


  Source: CISA
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  Apr 23, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,127
  Trophy Points: 280
  Hii habari mbona kama ya muda mrefu!!!
   
 8. RR

  RR JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2010
  Joined: Mar 17, 2007
  Messages: 6,717
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Ni mwaka jana, i think
   
 9. bht

  bht JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  exactly.......hamna mpya hapa
   
Loading...