Jacob Boniface (Meya CHADEMA): Tunataka kuweka kumbukumbu sawa kabla ya kufanya maamuzi magumu

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Tumeenda kufanya nini JUMUIYA YA UMOJA WA ULAYA NA WABUNGE WA CHADEMA?

Leo tarehe 29 March 2018 kwa pamoja Wajumbe wa kamati Kuu na wabunge wa Chadema tumeweka kumbukumbu sawia ikiwa ni Hatua ya Mwisho ya Utunzaji wa Kumbukumbu za Matukio kabla ya kufanya Hatua ya Mwisho ya kupambania Hadhi,Utu,Haki,Demokrasia na Ubinadamu.

Sisi Siwaoga hata Kidogo,Na Hatuto ogopa kukaa kwenye Nchi yetu na kuendelea kufanya siasa kwa Mujibu wa Katiba na Sheria kama wenzetu wachache wanavyotaka.wala hatukwenda kulialia,au kutia huruma.

Sisi tuna Njia nyingine nyingi ya kupambania Haki,utu na Demokrasia ya Nchi yetu.

Kabla ya Kufanya lolote, leo tumepeleka ushahidi wa Matukio yote kwa Mlolongo,Matukio ya Kuchokozwa Kwa Makusudi na Serikali na Vyombo Vyake Vya Dola.

Nina Imani ya kuwa Mabalozi wametusikia na Wametuelewa kwa Upana zaidi Kwa njia hii kubwa ya kidiplomasia,sababu leo wameona Matukio yote,wameona Wabunge waliofungwa miezi sita na wakashinda rufaa,Wameona wabunge waliofungwa kwa Hila za kukosa Dhamana,Na mwisho wakaona Serikali Yenye Magari zaidi ya Laki 1 imekosa gari ya kuwachukua Mahabusu Segerea sababu ya kumkomoa Mbowe na Wenzie.

Na sasa Ni Imani yangu kuwa Lolote Tutakalo Azimia Katika Mkutano Mkuu na Kamati kuu Chadema dhidi ya Kujilinda na Hali hii na kukomesha Matendo haya dhidivya chama Chetu,Viongozi Wetu na Wanachama wetu,JUMUIYA UMOJA WA ULAYA na Mabalozi wote wa ULAYA watatuelewa vizuri sana.

HAKI UNINUA TAIFA
Hakika Tutashinda.

Boniface Jacob
Mjumbe kamati kuu CHADEMA
 
Kufa ukipigania haki za walio wengi hata Mbinguni utakaribishwa.

Kuna watanzania wenzetu walikufa na kupata vilema katika vita ya Kagera kwa lengo la kuikomboa nchi yetu ili sisi leo hii tuishi tukiwa Taifa huru hivyo sioni tatizo na sisi tukiwa tayari kudhuriwa ili kzazi kijacho kiishi katika misingi ya utu na kuheshimiana.

Tupigane haki na uhuru wetu kwa kutumia njia halali za kikatiba na kisheria wakitudhuru hukumu yao wataipata siku wakitangulia mbele za haki na hapa hapa duniani.

Enough is enough.
 
Ifike mahali sasa mchukue hatua ,Lisu anapigwa risasi ..unasikia Mbowe anasema tunalaani ,anakatwa mapanga Mawazo Mbowe huyo tunalaani ,shamba lake linavamiwa na mkuu wa wilaya ikiwa ni pamoja na Bilcanas ..Mbowe kesho yake tunalaani ,Ben Saanane kapotea Mbowe oh tunalaani ,Lema kakaa mahabusu pamoja na Lijualikali ,Mbowe oh tunalaani

Sugu kafungwa oh tunalaani ,kaokotwa kiongozi wa Chadema Coco beach ,sijui diwani Morogoro kauwawa Mbowe tunalaani

Polisi ikamuua Akwilina sasa kesi ya mauaji anapewa Mbowe

Haya sasa Leo Mbowe kawekwa ndani nani wa kulaani ?

Kulaani hakubadilishi chochote lazima muwe na counter strategy ya kujibu huu upumbavu mnaofanyiwa kwa vitendo
 
Ifike mahali sasa mchukue hatua ,Lisu anapigwa risasi ..unasikia Mbowe anasema tunalaani ,anakatwa mapanga Mawazo Mbowe huyo tunalaani ,shamba lake linavamiwa na mkuu wa wilaya ikiwa ni pamoja na Bilcanas ..Mbowe kesho yake tunalaani ,Ben Saanane kapotea Mbowe oh tunalaani ,Lema kakaa mahabusu pamoja na Lijualikali ,Mbowe oh tunalaani

Sugu kafungwa oh tunalaani ,kaokotwa kiongozi wa Chadema coco beach ,sijui diwani Morogoro kakuuwawa Mbowe tunalaani

Polisi ikamuua Akwilina sasa kesi ya mauaji anapewa Mbowe

Haya sasa Leo Mbowe kawekwa ndani nani wa kulaani ?

Kulaani hakubadilishi chochote lazima muwe na counter strategy ya kujibu huu upumbavu mnaofanyiwa kwa vitendo
Mkuu punguza jazba
 
Tumeenda kufanya nini JUMUIYA YA UMOJA WA ULAYA NA WABUNGE WA CHADEMA?

Leo tarehe 29 March 2018 kwa pamoja Wajumbe wa kamati Kuu na wabunge wa Chadema tumeweka kumbukumbu sawia ikiwa ni Hatua ya Mwisho ya Utunzaji wa Kumbukumbu za Matukio kabla ya kufanya Hatua ya Mwisho ya kupambania Hadhi,Utu,Haki,Demokrasia na Ubinadamu.

Sisi Siwaoga hata Kidogo,Na Hatuto ogopa kukaa kwenye Nchi yetu na kuendelea kufanya siasa kwa Mujibu wa Katiba na Sheria kama wenzetu wachache wanavyotaka.wala hatukwenda kulialia,au kutia huruma.

Sisi tuna Njia nyingine nyingi ya kupambania Haki,utu na Demokrasia ya Nchi yetu.

Kabla ya Kufanya lolote, leo tumepeleka ushahidi wa Matukio yote kwa Mlolongo,Matukio ya Kuchokozwa Kwa Makusudi na Serikali na Vyombo Vyake Vya Dola.

Nina Imani ya kuwa Mabalozi wametusikia na Wametuelewa kwa Upana zaidi Kwa njia hii kubwa ya kidiplomasia,sababu leo wameona Matukio yote,wameona Wabunge waliofungwa miezi sita na wakashinda rufaa,Wameona wabunge waliofungwa kwa Hila za kukosa Dhamana,Na mwisho wakaona Serikali Yenye Magari zaidi ya Laki 1 imekosa gari ya kuwachukua Mahabusu Segerea sababu ya kumkomoa Mbowe na Wenzie.

Na sasa Ni Imani yangu kuwa Lolote Tutakalo Azimia Katika Mkutano Mkuu na Kamati kuu Chadema dhidi ya Kujilinda na Hali hii na kukomesha Matendo haya dhidivya chama Chetu,Viongozi Wetu na Wanachama wetu,JUMUIYA UMOJA WA ULAYA na Mabalozi wote wa ULAYA watatuelewa vizuri sana.

HAKI UNINUA TAIFA
Hakika Tutashinda.

Boniface Jacob
Mjumbe kamati kuu CHADEMA
Pumbavu zako Jacob,si muda mrefu utaanza kuokota makopo,kama akili yenyewe ndo hii ,kutegemea hawala
 
Back
Top Bottom