Jacob Boniface: Mbowe rudisha makambi ya vijana tujilinde

Huyu Jacob hana hadhi wala sura ya kimeya cheo kkama hicho alitakiwa apewe MTU mwenye hadhi.Yeye amajisahau kuwa meya ni MTU mkubwa mtumishi wa watu wote uchama anatakiwa kuweka pembeni.Anadhalilisha sana cheo cha umeya
Kuna wengine wana nyadhifa kuzidi yeye lkn ukiangalia wanayofanya utadhani mkiti wa kijiji.
 
Narudia tena bila kujali wapenzi wa Chadema wanachukuliaje.

Jacob Boniface alipaswa kuwekwa pembeni kwenye active politics kwasababu ya nafasi yake.

Zinatakiwa busara ndogo sana kuona hili kuwa mwenendo wa Meya Jacob kisiasa hatoweza kuchangamana na watu wa serikali kirahisi.

Haya matamko au comments zake mitandaoni alipaswa kuepuka sana kuandika kiharakati au kujibizana sana na wanasiasa. Hii nafasi ya Umeya wa Jacob ni moja ya fursa ambazo Chadema wameshindwa kuzitumia vyema kama mfano.

Mwenzake Isaya Mwita anajua kuishi na kufanya kazi na serikali. Unategemea nini Meya kutoa maoni kama haya alafu apate ushirikiano mzuri kutoka kwa mkurugenzi?Meya Jacob anapaswa kuvua koti la ukada uliopitiliza ili aweze kufanya kazi aliyotumwa na wananchi

Mwenye masikio na asikie mkishupaza shinfo 2020 haiko mbali. Tutawakumbusha mlipoangukia.

Hebu nisaidie ulivyo muelewa Mkuu ,ametoa Maoni yake kama Kada au ametoa Maoni yake kama Meya ?
 
Jacob aache kuwaza mambo ya vikosi, apige Kazi. Wananchi watampima kwa utendaji katika majukumu yake kama Diwani na Meya. Kwa style hii wakihusishwa na matukio wanasema wanaonewa.

Hakuna kikosi ambacho kinaweza kuwa imara kuliko vikosi halali Serikali ya JMT ambavyo vipo kwa mujibu wa sheria.
Kama hivyo vikosi imara vya JMT vikiwa vinaua, vinateka na kutesa watu, wale wanaodhulumiwa hawana haki ya hata ya kuwa na vikosi dhaifu angalao vya kujilinda, na siyo kupambana?
 
huyo mwita mwenyewe 2020 hatoboi labda abadili gia
Siyo Mwita tu bali kwa udikteta unaofanyika sasa hakuna atakayetangazwa mshindi maana JPM alishasema kuwa atashindwa kuelewa mkurugenzi atakayemtangaza mpinzani ameshinda kama atakuwa na akili.

Kwa sasa cha muhimu ni uhai. Kama hupo hai, huo ushindi utaupata ukiwa kaburini?
 
Mimi sisemi kitu, ntapigwa ban maana nahisi jf ni mali ya makamanda.
 
Back
Top Bottom