Jacob Boniface: Mbowe rudisha makambi ya vijana tujilinde

Mku mimi kwa uelewa wangu hii kauli sio nyepesi kumbuka nchi hii ni ya vyama vingi kila chama kina wafuasi wake kwa hiyo ni haki ya chama kuwapa Wanachama wao msimamo wa chama sio dhambi.
Na ukija ktk njia ambayo chama changu ccm kinapitia ktk waraka zilizotoka ktk madhehebu mawili uje tena chadema watoe msimamo wao na vyama vingine. Ndugu yangu hii kitu ni jambo lingine lisilo na jibu la wepesi kama hili.
Mambo sio mazuri yaani nchi haina afya njema nchi kugawanyika imegawanyika kivyama na kiitikadi tutegemee nini ktk hii hoja Meya

Inawezekana wewe huna uzoefu wa siasa za Tanzania.

Matamko ya Maaskofu yamekuwepo tokea utawala wa Mwinyi.

Kwenye utawala wa Kikwete yalikuwa yakitokewa matamko mara kwa mara lakini tunajua kilichotokea baada ya Uchaguzi.

Usishangae ukisikia hao hao Maaskofu wakitoa tena matamko ya kuipongeza serikali.

Hii dhana ya kusema taifa limegawanyika ni hisia tu inayotumika kujaza upepo wa kifikra baadhi ya watu wasiochanganua masuala ya kisiasa ili waingiwe na kiwewe cha kisiasa.

Hizi ni kelele za kutaka kumuondoa Rais Magufuli katika malengo yake.
 
Mtu mwenyewe kajawa mafuta hawezi izunguka ubungo bus stand. Ataweza kweli hizo mbwaimbwai analilia?
Loudest ones are the weakest
Vita vya leo ni vya kisasa si lazima kukutana face to face.
 
Inawezekana wewe huna uzoefu wa siasa za Tanzania.

Matamko ya Maaskofu yamekuwepo tokea utawala wa Mwinyi.

Kwenye utawala wa Kikwete yalikuwa yakitokewa matamko mara kwa mara lakini tunajua kilichotokea baada ya Uchaguzi.

Usishangae ukisikia hao hao Maaskofu wakitoa tena matamko ya kuipongeza serikali.

Hii dhana ya kusema taifa limegawanyika ni hisia tu inayotumika kujaza upepo wa kifikra baadhi ya watu wasiochanganua masuala ya kisiasa ili waingiwe na kiwewe cha kisiasa.

Hizi ni kelele za kutaka kumuondoa Rais Magufuli katika malengo yake.
Ni kweli matamko yamekuwepo tangu zamani lkn hatujawahi kuona rais akiwajibu na kuwabeza maaskofu kama awamu hii.

Kina Mwinyi, Mkapa hata Kikwete walipoona hivyo walikuwa wakiwaita ikulu au sehemu yeyote kuwasikiliza hoja zao lkn si kuwakejeli.
 
Inawezekana wewe huna uzoefu wa siasa za Tanzania.

Matamko ya Maaskofu yamekuwepo tokea utawala wa Mwinyi.

Kwenye utawala wa Kikwete yalikuwa yakitokewa matamko mara kwa mara lakini tunajua kilichotokea baada ya Uchaguzi.

Usishangae ukisikia hao hao Maaskofu wakitoa tena matamko ya kuipongeza serikali.

Hii dhana ya kusema taifa limegawanyika ni hisia tu inayotumika kujaza upepo wa kifikra baadhi ya watu wasiochanganua masuala ya kisiasa ili waingiwe na kiwewe cha kisiasa.

Hizi ni kelele za kutaka kumuondoa Rais Magufuli katika malengo yake.
Mku sio hiki wanachokidai kwani hoja zao na Mange inatofauti gani .
Haya mambo sio mepesi kama unavyochukuli kumbuka vyombo vya habari vya mataifa vimeongelea sana haya mambo tuache kubeza jambo.
Ww unaona ni sawa viongozi wa dini kutoongelea dhamira waumini wao
 
namkubali Sana Major General Boniface Jacob, tunasubiri kuona zile nyarakaka za maaskofu zinafanyiwa kazi? vinginevyo tunaingia msituni mchana kweupeee, kama mbwai na iwe mbwai,

wameonywa, wameshauriwa sana kilichobaki ni vitendo tu.
 
Narudia tena bila kujali wapenzi wa Chadema wanachukuliaje.

Jacob Boniface alipaswa kuwekwa pembeni kwenye active politics kwasababu ya nafasi yake.

Zinatakiwa busara ndogo sana kuona hili kuwa mwenendo wa Meya Jacob kisiasa hatoweza kuchangamana na watu wa serikali kirahisi.

Haya matamko au comments zake mitandaoni alipaswa kuepuka sana kuandika kiharakati au kujibizana sana na wanasiasa. Hii nafasi ya Umeya wa Jacob ni moja ya fursa ambazo Chadema wameshindwa kuzitumia vyema kama mfano.

Mwenzake Isaya Mwita anajua kuishi na kufanya kazi na serikali. Unategemea nini Meya kutoa maoni kama haya alafu apate ushirikiano mzuri kutoka kwa mkurugenzi? Meya Jacob anapaswa kuvua koti la ukada uliopitiliza ili aweze kufanya kazi aliyotumwa na wananchi.

Mwenye masikio na asikie mkishupaza shinfo 2020 haiko mbali. Tutawakumbusha mlipoangukia.
dogo mbona unaonekana uko soft sana, Nina wasiwasi utakuwa una abuse jinsia yako
 
Kauli za kujipa matumaini hewa.

Huyu ni mtalaam wa utumbo wa siasa za mitandao na utoto wakati mwenzake Meya wa Jiji, Isaya Mwita anachapa kazi bila makelele.

Huyu Boniface baada ya kumtesa mlinzi wa Dkt. Slaa na hakukamatwa basi anadhani anaweza kufanya lolote kwa wengine.

Yeye kama anadhani kuna umuhimu wa kuanzisha makambi ya mafunzo ya kigaidi kwa nini asianzishe yeye badala ya kumpa kazi hiyo Mbowe.

Yeye anaepuka madhara ya kufanya maamuzi hayo na anataka Mbowe ayabebe halafu yeye akauze sura mahakamani kama msikiliza kesi.

Ananikumbusha wakati tukiwa watoto na kati yetu wakitaka kupigana ngumi utasikia mmoja anasema anza wewe. Niguse uone.

Halafu Kulinganisha siasa za Tanzania na Afrika Kusini ni kuanika ujinga wake katika masuala ya geopolitics
Mengi ya uliyoyasema ni kweli lakini hili moja umekosea. Siasa za Tanzania kwa sasa zinaweza kulinganishwa na siasa za Africa ya kusini wakati huo na hata sasa hivi. Africa ya kusini ilikuwa huru lakini kulikuwa na ubaguzi wa rangi. Watu waliheshimiwa kulingana na rangi ya ngozi yao. Waafrica walikuwa daraja la chini kabisa, nao haki zao zilikandamizwa na matabaka ya juu(wazungu na wahindi na hata machotara).
Hapa Tanzania hakuna ubaguzi wa rangi lakini kuna ubaguzi; kuna tabaka la watawala na tabaka la watawaliwa. Kuna miungu watu na watu. Unaposikia watu wanaanza kujisema kuwa hata wakifa watawatawala hata malaika! Unaposikia mtu anasema Rais ni malaika wa Mungu. Unaposikia kuwa kuna watu wakunyosha wengine na watu wa kunyoshwa. Inapothibitika kuwa wanyoshaji wanatoka chama tofauti cha wanyoshwaji! Nionavyo mimi, ubaguzi umetamalaki, ukandamizaji umekithiri na ubabe umepindukia.

Katika hali kama hii kwa nini utawala wetu usionekane wa kibaguzi? Kwanini watu wa kunyoshwa wasijitetee kuwa wanaumizwa?
 
Kauli za kujipa matumaini hewa.

Huyu ni mtalaam wa utumbo wa siasa za mitandao na utoto wakati mwenzake Meya wa Jiji, Isaya Mwita anachapa kazi bila makelele.

Huyu Boniface baada ya kumtesa mlinzi wa Dkt. Slaa na hakukamatwa basi anadhani anaweza kufanya lolote kwa wengine.

Yeye kama anadhani kuna umuhimu wa kuanzisha makambi ya mafunzo ya kigaidi kwa nini asianzishe yeye badala ya kumpa kazi hiyo Mbowe.

Yeye anaepuka madhara ya kufanya maamuzi hayo na anataka Mbowe ayabebe halafu yeye akauze sura mahakamani kama msikiliza kesi.

Ananikumbusha wakati tukiwa watoto na kati yetu wakitaka kupigana ngumi utasikia mmoja anasema anza wewe. Niguse uone.

Halafu Kulinganisha siasa za Tanzania na Afrika Kusini ni kuanika ujinga wake katika masuala ya geopolitics
Hivi Bado wamemuwekea mamake wema walinzi kule sinza au wamewaondoa?
 
Asalaam Mh. Mwenyekiti wangu

Baada ya salaam naomba kukupa hongera kwa hekaheka za hapa na pale huku pia nikikutia moyo usonge mbele kuendelea kupanga safu na vikosi vyako vizuri kwa sababu mambo yameiva mkuu. Kwetu huku kwa watu wa Pwani kuna msemo usemao
*"kurukaruka kwa maharage ndiyo kuiva kwake"*

Mhe. Mwenyekiti wangu, Mungu atupe nini zaidi ya haya yanayoendelea sasa? Siasa imekuwa nyepesi kuliko miaka yote 25 mliyoanzisha vuguvugu la mabadiliko nchini. Siku hizi wasomi, wafanya biashara, viongozi wa dini, wasanii na hata mabishoo nao wanapiga siasa vizuri kuliko hata baadhi ya waanzilishi na waasisi wa siasa za mabadiliko.

Dalili ni njema sana na matunda ya kazi za watangulizi wote wa mageuzi, kuanzia waliokimbia upande wetu mpaka tulionao leo. Mimi mmoja wa wapiganaji (askari) wako wa miguu, nakuhakikishia mambo mazuri sana mtaani.

Je Mh. Mwenyekiti umeliona teke la farasi anayekufa? Kwa kule majuu wanaita *"the last kick of the dying horse"*

Kwa sasa CCM na serikali yake hawana tena jipya na wameacha kufanya siasa tena. Ndiyo maana husikii mashambulizi kwetu kama zamani ooh mara siasa za ukanda, mara udini, mara kununua wapinzani zaidi ya yule BWANA YULE....siyo wajinga walishajua haisaidii tena na muda umekwenda sana na wameanza kuachwa nao.

Teke la farasi anayekufa baya sana Mh. Mwenyekiti. Huwa lina nguvu sana. Huweza kukusababishia kifo. Huwa ndiyo karata yake ya mwisho ya kupambania uhai wake. Bahati nzuri ni kwamba huwa pia ni dalili ya kwamba amezidiwa na hana mbinu nyingine tena kabla ya kusalimu amri ya kifo. *Ndiyo farasi anakufa hivyo*

CCM ndiyo kinahitimisha utawala wake wa miaka arobaini na ushee tangu kianzishwe na kinajua kinaelekea kufa ama kufutika kabisa.

Jambo pekee wanalodhania litawaokoa na kifo cha chama chao na serikali yao ni kuua, kuteka na kupoteza wapinzani na wakosoaji wa serikali yao. Ili kupunguza kupingwa kila kona ama kutia watu uoga.

Kumbe jambo ambalo farasi anayekufa hakuwa anajua ni kwamba, wakosoaji kwenye nchi si nyinyi peke peke yenu kama zamani bali moto wa fikra za mabadiliko ulishawaka nchi nzima. Sisi tunaoishi na watu huku mitaani tunaona.

Mh. Mwenyekiti kila tawala ya kidhalimu inapokaribia kutoweka inatumia mbinu hizo. Majirani zetu Afrika Kusini chini ya makaburu walikutana na hali hii walipokuwa wanawaondoa makaburu madarakani. Waliuwawa, waliteswa na wengine walipotezwa hata maiti zao hazikuonekana kabisa.

Lakini hawakurudi nyuma bali walianzisha makambi ya vijana na kauli mbiu ya "UMKHONTO WE SIZWE" kulinda wanachama wa ANC viongozi wake na wananchi wanyonge dhidi ya makaburu. Ikawa 'teka tuwateke, poteza tuwapoteze na vunja tukuvunje'.

Kila ngazi ya chama chao ANC palikuwa na BLACK BOOK ya kusajili majina na anuani za watesi wao kwenye likitabu la kumbukumbu......wapo wananchi wetu huku chini wanaanza kushauri kuwa hilo hata sisi tunaweza kulifanya.

Juzi mmoja akaniuliza kwanini Mh. Mwenyekiti usiitishe vikao vya chama na tuazimie na tutangazie wanachama wetu wote na wapenzi wa mabadiliko hali ya hatari, ili tujihami wote? Tuhesabu kondoo wako zizini. Wasipotee zaidi ya hao waliopotea. Tusilalamike kuumizwa wakati na sisi tunacho cha kufanya. Hili pekee ndilo litakalofanya tuwe salama na tuheshimiane ikibidi kukaa chini meza moja kwa mazungumzo ya kuamua mstakabali mwema wa pamoja wa nchi yetu, Mama Tanzania.

Tangaza hari ya hatari kwa wanachama wako na wafuasi wote, kisha mikoa na wilaya za kichama zikae chini kutoa vijana wa kike na kiume kila upande. Tupewe mafunzo ya tahadhari na kujihami dhidi ya vikundi vya kifedhuli na nina imani vijana tutakupa ushirikiano mkubwa sana,
sababu wakosoaji na wapinzani wa serikali hii hatuna mpango wa ku retreat au kuacha kabisa kuikosoa na kuipinga kwa namna ilivyopoteza malengo na muelekeo ambao Watanzania walitarajia.

Haitakuwa mara ya kwanza kwa chama kufanya hivyo na haitakuwa mara ya mwisho kwa wewe kulaumiwa kwa kuongoza vikao vya chama kufanya maamuzi ya kulinda hadhi na utu wa wanachama wetu na jamii nzima ya Watanzania.

Tunashauri ufanye hima... hima Mh. Mwenyekiti wetu, vijana wako tumalizie kazi ambayo wewe na Wazee wetu wengine mmeisimamia kwa miaka yote 25 kwa ajili ya MABADILIKO YA KWELI NA UHURU WA KWELI ndani ya nchi yetu Tanzania.

Na BONIFACE JACOB
MJUMBE KAMATI KUU
SENIOR COUNCILOR UBUNGO

Jacob aache kuwaza mambo ya vikosi, apige Kazi. Wananchi watampima kwa utendaji katika majukumu yake kama Diwani na Meya. Kwa style hii wakihusishwa na matukio wanasema wanaonewa.

Hakuna kikosi ambacho kinaweza kuwa imara kuliko vikosi halali Serikali ya JMT ambavyo vipo kwa mujibu wa sheria.
 
Anahofia usalama wake na sio kuchaguliwa tena maana kama ni kura atapata tu.
 
Narudia tena bila kujali wapenzi wa Chadema wanachukuliaje.

Jacob Boniface alipaswa kuwekwa pembeni kwenye active politics kwasababu ya nafasi yake.

Zinatakiwa busara ndogo sana kuona hili kuwa mwenendo wa Meya Jacob kisiasa hatoweza kuchangamana na watu wa serikali kirahisi.

Haya matamko au comments zake mitandaoni alipaswa kuepuka sana kuandika kiharakati au kujibizana sana na wanasiasa. Hii nafasi ya Umeya wa Jacob ni moja ya fursa ambazo Chadema wameshindwa kuzitumia vyema kama mfano.

Mwenzake Isaya Mwita anajua kuishi na kufanya kazi na serikali. Unategemea nini Meya kutoa maoni kama haya alafu apate ushirikiano mzuri kutoka kwa mkurugenzi? Meya Jacob anapaswa kuvua koti la ukada uliopitiliza ili aweze kufanya kazi aliyotumwa na wananchi.

Mwenye masikio na asikie mkishupaza shinfo 2020 haiko mbali. Tutawakumbusha mlipoangukia.
huyo mwita mwenyewe 2020 hatoboi labda abadili gia
 
Huyu jamaa ni miongoni mwa watu 10 hatari waliotajwa na Cyprian Musiba tumpuuze tuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!¡!!!
 
Narudia tena bila kujali wapenzi wa Chadema wanachukuliaje.

Jacob Boniface alipaswa kuwekwa pembeni kwenye active politics kwasababu ya nafasi yake.

Zinatakiwa busara ndogo sana kuona hili kuwa mwenendo wa Meya Jacob kisiasa hatoweza kuchangamana na watu wa serikali kirahisi.

Haya matamko au comments zake mitandaoni alipaswa kuepuka sana kuandika kiharakati au kujibizana sana na wanasiasa. Hii nafasi ya Umeya wa Jacob ni moja ya fursa ambazo Chadema wameshindwa kuzitumia vyema kama mfano.

Mwenzake Isaya Mwita anajua kuishi na kufanya kazi na serikali. Unategemea nini Meya kutoa maoni kama haya alafu apate ushirikiano mzuri kutoka kwa mkurugenzi? Meya Jacob anapaswa kuvua koti la ukada uliopitiliza ili aweze kufanya kazi aliyotumwa na wananchi.

Mwenye masikio na asikie mkishupaza shinfo 2020 haiko mbali. Tutawakumbusha mlipoangukia.

Nionyeshe ni meya gani w aupinzani anafanya kazi na srekali na amefanikiwa na amefanikiw akwenye lipi zaidi ya kupiga picha na kusifiwa ?
 
Kauli za kujipa matumaini hewa.

Huyu ni mtalaam wa utumbo wa siasa za mitandao na utoto wakati mwenzake Meya wa Jiji, Isaya Mwita anachapa kazi bila makelele.

Huyu Boniface baada ya kumtesa mlinzi wa Dkt. Slaa na hakukamatwa basi anadhani anaweza kufanya lolote kwa wengine.

Yeye kama anadhani kuna umuhimu wa kuanzisha makambi ya mafunzo ya kigaidi kwa nini asianzishe yeye badala ya kumpa kazi hiyo Mbowe.

Yeye anaepuka madhara ya kufanya maamuzi hayo na anataka Mbowe ayabebe halafu yeye akauze sura mahakamani kama msikiliza kesi.

Ananikumbusha wakati tukiwa watoto na kati yetu wakitaka kupigana ngumi utasikia mmoja anasema anza wewe. Niguse uone.

Halafu Kulinganisha siasa za Tanzania na Afrika Kusini ni kuanika ujinga wake katika masuala ya geopolitics
Kiazi
 
Huyu Jacob hana hadhi wala sura ya kimeya cheo kkama hicho alitakiwa apewe MTU mwenye hadhi.Yeye amajisahau kuwa meya ni MTU mkubwa mtumishi wa watu wote uchama anatakiwa kuweka pembeni.Anadhalilisha sana cheo cha umeya
 
Asalaam Mh. Mwenyekiti wangu

Baada ya salaam naomba kukupa hongera kwa hekaheka za hapa na pale huku pia nikikutia moyo usonge mbele kuendelea kupanga safu na vikosi vyako vizuri kwa sababu mambo yameiva mkuu. Kwetu huku kwa watu wa Pwani kuna msemo usemao
*"kurukaruka kwa maharage ndiyo kuiva kwake"*

Mhe. Mwenyekiti wangu, Mungu atupe nini zaidi ya haya yanayoendelea sasa? Siasa imekuwa nyepesi kuliko miaka yote 25 mliyoanzisha vuguvugu la mabadiliko nchini. Siku hizi wasomi, wafanya biashara, viongozi wa dini, wasanii na hata mabishoo nao wanapiga siasa vizuri kuliko hata baadhi ya waanzilishi na waasisi wa siasa za mabadiliko.

Dalili ni njema sana na matunda ya kazi za watangulizi wote wa mageuzi, kuanzia waliokimbia upande wetu mpaka tulionao leo. Mimi mmoja wa wapiganaji (askari) wako wa miguu, nakuhakikishia mambo mazuri sana mtaani.

Je Mh. Mwenyekiti umeliona teke la farasi anayekufa? Kwa kule majuu wanaita *"the last kick of the dying horse"*

Kwa sasa CCM na serikali yake hawana tena jipya na wameacha kufanya siasa tena. Ndiyo maana husikii mashambulizi kwetu kama zamani ooh mara siasa za ukanda, mara udini, mara kununua wapinzani zaidi ya yule BWANA YULE....siyo wajinga walishajua haisaidii tena na muda umekwenda sana na wameanza kuachwa nao.

Teke la farasi anayekufa baya sana Mh. Mwenyekiti. Huwa lina nguvu sana. Huweza kukusababishia kifo. Huwa ndiyo karata yake ya mwisho ya kupambania uhai wake. Bahati nzuri ni kwamba huwa pia ni dalili ya kwamba amezidiwa na hana mbinu nyingine tena kabla ya kusalimu amri ya kifo. *Ndiyo farasi anakufa hivyo*

CCM ndiyo kinahitimisha utawala wake wa miaka arobaini na ushee tangu kianzishwe na kinajua kinaelekea kufa ama kufutika kabisa.

Jambo pekee wanalodhania litawaokoa na kifo cha chama chao na serikali yao ni kuua, kuteka na kupoteza wapinzani na wakosoaji wa serikali yao. Ili kupunguza kupingwa kila kona ama kutia watu uoga.

Kumbe jambo ambalo farasi anayekufa hakuwa anajua ni kwamba, wakosoaji kwenye nchi si nyinyi peke peke yenu kama zamani bali moto wa fikra za mabadiliko ulishawaka nchi nzima. Sisi tunaoishi na watu huku mitaani tunaona.

Mh. Mwenyekiti kila tawala ya kidhalimu inapokaribia kutoweka inatumia mbinu hizo. Majirani zetu Afrika Kusini chini ya makaburu walikutana na hali hii walipokuwa wanawaondoa makaburu madarakani. Waliuwawa, waliteswa na wengine walipotezwa hata maiti zao hazikuonekana kabisa.

Lakini hawakurudi nyuma bali walianzisha makambi ya vijana na kauli mbiu ya "UMKHONTO WE SIZWE" kulinda wanachama wa ANC viongozi wake na wananchi wanyonge dhidi ya makaburu. Ikawa 'teka tuwateke, poteza tuwapoteze na vunja tukuvunje'.

Kila ngazi ya chama chao ANC palikuwa na BLACK BOOK ya kusajili majina na anuani za watesi wao kwenye likitabu la kumbukumbu......wapo wananchi wetu huku chini wanaanza kushauri kuwa hilo hata sisi tunaweza kulifanya.

Juzi mmoja akaniuliza kwanini Mh. Mwenyekiti usiitishe vikao vya chama na tuazimie na tutangazie wanachama wetu wote na wapenzi wa mabadiliko hali ya hatari, ili tujihami wote? Tuhesabu kondoo wako zizini. Wasipotee zaidi ya hao waliopotea. Tusilalamike kuumizwa wakati na sisi tunacho cha kufanya. Hili pekee ndilo litakalofanya tuwe salama na tuheshimiane ikibidi kukaa chini meza moja kwa mazungumzo ya kuamua mstakabali mwema wa pamoja wa nchi yetu, Mama Tanzania.

Tangaza hari ya hatari kwa wanachama wako na wafuasi wote, kisha mikoa na wilaya za kichama zikae chini kutoa vijana wa kike na kiume kila upande. Tupewe mafunzo ya tahadhari na kujihami dhidi ya vikundi vya kifedhuli na nina imani vijana tutakupa ushirikiano mkubwa sana,
sababu wakosoaji na wapinzani wa serikali hii hatuna mpango wa ku retreat au kuacha kabisa kuikosoa na kuipinga kwa namna ilivyopoteza malengo na muelekeo ambao Watanzania walitarajia.

Haitakuwa mara ya kwanza kwa chama kufanya hivyo na haitakuwa mara ya mwisho kwa wewe kulaumiwa kwa kuongoza vikao vya chama kufanya maamuzi ya kulinda hadhi na utu wa wanachama wetu na jamii nzima ya Watanzania.

Tunashauri ufanye hima... hima Mh. Mwenyekiti wetu, vijana wako tumalizie kazi ambayo wewe na Wazee wetu wengine mmeisimamia kwa miaka yote 25 kwa ajili ya MABADILIKO YA KWELI NA UHURU WA KWELI ndani ya nchi yetu Tanzania.

Na BONIFACE JACOB
MJUMBE KAMATI KUU
SENIOR COUNCILOR UBUNGO
Ovyoo kabisa. Umeongea pumba mtupu
 
Back
Top Bottom