Jackson Mvangila Makwetta: Tofauti 10 Kati yake na Mafisadi

galiya

JF-Expert Member
Oct 29, 2012
302
131
J.M. Makweta alizaliwa 15.6.1943 na amefariki 17.11.2012 wodi ya Mwaisela, hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo na figo. Nawapa pole sana wafiwa wote.

Mwaka 1975 akiwa Mwalimu IDM Mzumbe aligombea Ubunge Njombe Kaskazini na mwanafunzi wake chuoni hapo A. Makinda aliyekua machachali sana chuoni hapo akagombea Ubunge Njombe Kusini na wote wakashinda. Huo ndo ulikua ni mwanzo wa harakati za sias za marehemu J.M. Makweta.Alikua Mbunge kwa miaka 35 (1975-2010). Pia alikuwa Waziri katika Wizara mbalimbali eg Ofisi ya Waziri Mkuu, Elimu, Kilimo, Jeshi la Kujenga taifa na pia Mawasiliano.Binafsi nimejifunza mambo mengi toka marehemu Makweta kama ifuatavyo;

1. MCHAPAKAZI HODARI
Makweta alikua ni mchapakazi sana na kazini alikua akiingia saa moja na mara nyingi kutoka usiku wa manane. Aidha sehemu zote alizofanya kazi alipendwa mno na wafanyakazi. Makweta ni tofauti na viongozi wengi mfano PM mmoja ambae ana uchu sana wa kutaka kwenda Ikulu wakati akiwa PM, alikua akitoka kazini saa 9.30 na kwenda nyumbani kwaajili ya kuanza kupanga dili za rushwa!Ukikuta yumo ofisni baada ya muda wa kazi basi ujue kuna dili inachongwa! Kutokana na uhodari wake na uzoefu wake, 1995 wengi walimtabiria Makweta au P. Kimiti kuwa Waziri Mkuu lakini Mkapa akamuibua Sumaye.

2. KUTOBAGUA WAGENI OFISINI
Daima Makweta hakua na ubaguzi kwani aliona binadamu wote ni sawa. Ofisini kwake ilikua ni "First come, first served". Ni tofauti na ofisi za viongozi wengi ambapo si jambo la ajabu mtu ukafika saa moja lakini kibopa au mhindi akaja saa nne akatangulia yeye. Kwa Makweta hilo lilikua ni mwiko.

3. HAKUWA FISADI
Makweta licha ya kupata nafasi nyingi za ccm na serikalini hakupata hata siku moja kua na fikra za kujitajirisha kama kua na jumba kama la Ubalozi wa Afrika ya Kusini etc. Viongozi wengi wanapopata nafasi serikalini basi wao kitu pekee wakiwazacho ni dili na rushwa mf Waziri mmoja wa Ardhi 1993-95 kazi yake kubwa ilikua ni kuuza open spaces kwa matajiri pamoja na maeneo mengine nyeti kwa wahindi na hivyo kupata utajiri mkubwa! Inashangaza watu kuuliza kiongozi huyu kapataje utajiri huu wakati hata Baba wa Taifa alisema kwa umri wake mdogo kwa nchi kama yetu asingekua na utajiri huo. Wapambe wake daima hudai eti kaupata kutokana na kuuza ngombe wa urithi!

4.KANISANI
Makweta daima alikua akitoa sadaka kama wakristu wengine kwa kufuata utaratibu uliowekwa. Kuna bwana mmoja mwenye uchu wa kwenda Ikulu anaogopwa hadi kanisani kwake maeneo ya posta ambako baada ya waumini wengine kutoa sadaka yeye na familia yake hupeleka sadaka kwenye vikapu kwa padr huku waumini wengine wakiwa wamekaai!

5. NYUMBA YA KAWAIDA
Kijijini kwake Njombe, Makweta aliishi nyumba ya kawaida na maisha ya kawaida sana. Hata hapa Dsm kule Boko Makweta aliishi na Wagogo na kuongea nao kama vile hakuwahi kua na cheo kikubwa serikalini! Aliishi maisha sawa na aliowaongoza na kuutendea haki ushauri uliotolewa na Nyerere 7.7.1985 "Politicians lifestyles should never be far removed from the electorate". Huyu ni tofauti na baadhi ya viongozi wanaoutaka Urais na wana Majumba karibu kila mkoa. Tumeona wakati Uncle Hashim Lundenga na Mamiss TZ majuzi walivyomtembelea Kigogo mmoja Monduli akiwa ndani ya "Kasri lake la kufa mtu huku wanavijiji wakiwa na nyumba za mbavu za mbwa!

6.MBUNIFU HODARI
Katika kila wizara alikopita alibuni jambo jipya na zuri ambalo linakumbukwa hadi leo mfano Mitihani ya kidato cha pili. Sio kama wengine eti walibuni njia tatu za kupita asb na jioni matokeo yake ni kuzidisha foleni na kuongeza ajali!

7. KUWAENDELEZA WATU WAKE
Alifanya kazi kubwa kuwaendeleza watu wa jimbo lake. Aliinua elimu, alijenga barabara, umeme, maji RTC etc . Hii ni tofauti na wabunge wengine eg wale wenye uchu wa Urais lakini majimbo yao yako dhoful hali mf idadi ya Wamasai wanaoikimbia Monduli kuja mijini kutafuta kazi imekua ikiongezeka kwa kasi sana. Wamasai wengi sasa wamekua ni wasusi na walinzi!!! Hii ni aibu kubwa kwa "Mtu Mzima". Aidha lindi la umaskini linazidi kuongezeka na wafugaji wanazidi kuwa na hali mbaya! Hivi hizo hela zenu chafu mnazozigawa misikitin na makanisan kwanini msiwaendeleze hawa Wamasai??? Hivi mkishindwa 2015 mtaendelea kutoa hizi hela makanisani na miskitini kweli?

8. ALIICHUKIA SANA RUSHWA
Makweta daima alikua kipenda sana kuitaja Ahadi ya 5 ya Mwanatanu, 1965 "Cheo ni dhamana sitatoa wala kupokea rushwa. Vitendo vyake vilidhihirisha pasipo shaka kwamba aliamini kile anachokisema. Utashangaa kuna Mheshimiwa mmoja bila woga wala aibu akiwa Ujerumani kutibiwa nae alijitutumua eti nae alidai anachukia sana rushwa ila akamsifia Hosea kwa utendaji wake mzuri na eti pccb iendelezwe!Ndio lazma ampongeze Hosea si alimsafisha tuhuma za Richmondul eti uchunguzi haujabaini lolote baya!si Hosea huyuhuyu ameshindwa kufanya lolote chaguzi za NEC ambazo rushwa ilikua ikigawiwa vyooni hadi utu wa mwanadamu hauthamini?? Makweta aliona fahari kushindwa kuliko kutoa rushwa! Akiongea na Mwananchi 20.8. 2010 alisema rushwa ilitawala sana kura za maoni ccm njombe. Mfanyabiashara D. Sanga aka Jah People alihonga sana usiku na mchana na kuwatumia wafuasi wake wamtukane Makweta majukwaani.Deo Sanga ndiye pia aliyehonga mno Uenyekiti wa ccm mkoa wa Iringa na kumshinda P. Mangula ambae nae alilalamika mno matumizi makubwa ya rushwa.

9.HAKUTOA MAAMUZI YA KIDIKETA
Makweta daima alikua ni mtu mwenye kutumia busara wakati wa kufanya maamuzi. Kwake yeye kila jambo alilitolea uamuzi mara moja na hakupenda kulaza kazi-viporo. Kabla ya kufanya maamuzi alifikiri kwa kina na kisha kutoa uamuzi. Yeye ni tofauti na wengine ambao kwa kupenda sifa za kijinga hata wakiwa kwenye majukwaa ya siasa hufukuzilia mbali viongozi bila hata ya kusikia upande wao unasemaje. Viongozi hawa wakipewa nchi hawatakua na tofauti na Idd Amini ambae naye alikua akitoa maamuzi ya kipumbavu kama hayo!

10. HAKUWA MBINAFSI
Katika maisha yake yote hakuwa mbinafsi. yeye mara zote alipenda kugawana na wenzake na pia kushauri ili wengine nao waweze kufaidika

Great thinkers, the ball is now in your court!
 
RIP JACKSON Makweta daima tutakukumbuka, ubarikiwe na tutazidi kukuombea ili ufike Mbinguni kwa baba.
 
Mzee kudos kwa kuchambua legacy ya mzee wetu Makweta ambaye binafsi namkumbuka alipotembelea shuleni kwetu mwaka 1983 na nakumbuka alivyoingia darasani, wakati ule akiwa waziri wa elimu na akiwa na naibu wake Nalaila Kiula na kutufundisha biology na baada ya hapo kupiga stori na sisi. Hakika yule alikuwa anatoa servant leadership. Nimependa pia ulivyoua ndege wawili kwa jiwe moja kwa kutoa contrast na hili janga la taifa tulilonalo sasa hivi na ambalo kwake yeye hajali kama kiongozi anatakiwa kuwa na miiko. Miiko pekee anayoitambua yeye ni ile inayompa fursa ya kuhandisi njia za kujipatia utajiri na kuwafakirisha anaowania kuwaongoza. Hakika Makweta anastahili kuenziwa na kila mpenda haki na hasa katika kipindi hiki nchi inapoelekea kudidimizwa na wenye tamaa.
 
Uchambuzi wako umekuwa mzuri sana, japo umenichosha kitu kimoja tu! inaonekana kama umeandika kwa malengo mengine zaidi ya kumpraise mzee wetu (RIP Makweta). Mi siyo muumini wa uchambuzi wa majitaka, ingawa pia siyo mfuasi wa lowasa, lakini inaonekana wazi kabisa umeandika ukitaka kuonesha side effect ya lowasa
Maskini mtakuwa nao siku zote, na haiwezekani wote tukaishi maisha sasa
"we differ because we vary"
 
BHIKOLA

Nashukuru kwa maoni yako kwamba "uchambuzi wangu umekua mzuri sana". Lazma tutambue kwamba ingawa Mwanasiasa huyu katutoka inabid kuangalia tunajifunza nini toka kwake. Nakumbuka kuna mnywa gongo mmoja alifariki Mwenge miezi mitatu iliyopita. Huyu mtu ambaye alikua ni tena na kibaka hakua anasali na mapadri wakagoma kabisa kusalisha misa ya kumwombea. Kutokana na hali hiyo padri wa kanisa katoliki la Mwenge alihubiri kwa kirefu mafunzo tunayopata kwa kifo kile. Ndio maana katika uzi huu nami nimeweka mafunzo ambayo tunayapata toka kwa Marehemu Mzee wetu J.M. Makweta
 
Galiya nashukuru kwa uchambuzi wako, lakini nafikiri hukuwa unamfahamu vizuri huyu mzee. Ni kweli anaweza akawa alikuwa sio fisadi kiivo, lakini swala la kusaidia watu wa jimbo lake si kweli kama alisaidia ni kidogo sana lulinganisha na na muda aliokaa kama kiongozi. Pia alikuwa mbinafsi sana na mtu wa kujivuna, alidiriki kusema katika jimo lake akuna mtu anayeweza kuliongoza kama mbunge labda mtoto wake aliyekuwa akisoma Uingereza amalize shule ngio aje kuchukua nafasi yake. Hua sisahau, R.I.P J.M
 
Huyo mwingine ambaye anatenda na kufanya tofati na Makweta ni Lowassa nini?

Sifa nyingine kubwa ya Makweta ni MSIKIVU, yeye ndiye aliyeidhinisha posho ya wanafunzi wa mwaka wa mwisho, kwenye semester ya mwisho (kipindi kile cha LIKIZO) ili waweze kumudu gharama za maisha wakiwa shuleni (Chuo kikuu). Hii aliifanya mwaka 1996 akiwa waziri wa elimu ya Juu, Sayansi na teknolojia (kama nakumbuka vyema).
 
POPIEXO

Una ushahidi wa hicho ukisemacho? We unaonekana una chuki binafsi na marehemu eti ni mtoto wake tu ndo atakuja kuongoza!!! Kwa sisi tuliomfahamu vzr hawezi kutoa kauli kama hiyo. Muulize yeyote aliyefanya nae kazi. JIPANGE
 
Sifa hizi zinamstahili Makweta. Usafi wake ulimfanya Mkapa ashindwe kumteua kwenye awamu yake ya mwisho. Angalia alivyokuwa tofauti na wanaNjombe wenzake akina Spika Makinda, Philemon Luhanjo, akina Yona Kevela, fisadimtoto bosi wa NHC,.....
 
Mimi nafikiri ungesma tu TOFAUTI KATI YA J.MAKWETA NA E. LOWASA,maana content nzima ya post hiyo imemlenga mtu mmoja na si wengi kama inavyoonyesha kwenye tittle "mafisadi".
 
J.M. Makweta alizaliwa 15.6.1943 na amefariki 17.11.2012 wodi ya Mwaisela, hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo na figo. Nawapa pole sana wafiwa wote.

Mwaka 1975 akiwa Mwalimu IDM Mzumbe aligombea Ubunge Njombe Kaskazini na mwanafunzi wake chuoni hapo A. Makinda aliyekua machachali sana chuoni hapo akagombea Ubunge Njombe Kusini na wote wakashinda. Huo ndo ulikua ni mwanzo wa harakati za sias za marehemu J.M. Makweta.Alikua Mbunge kwa miaka 35 (1975-2010). Pia alikuwa Waziri katika Wizara mbalimbali eg Ofisi ya Waziri Mkuu, Elimu, Kilimo, Jeshi la Kujenga taifa na pia Mawasiliano.Binafsi nimejifunza mambo mengi toka marehemu Makweta kama ifuatavyo;

1. MCHAPAKAZI HODARI
Makweta alikua ni mchapakazi sana na kazini alikua akiingia saa moja na mara nyingi kutoka usiku wa manane. Aidha sehemu zote alizofanya kazi alipendwa mno na wafanyakazi. Makweta ni tofauti na viongozi wengi mfano PM mmoja ambae ana uchu sana wa kutaka kwenda Ikulu wakati akiwa PM, alikua akitoka kazini saa 9.30 na kwenda nyumbani kwaajili ya kuanza kupanga dili za rushwa!Ukikuta yumo ofisni baada ya muda wa kazi basi ujue kuna dili inachongwa! Kutokana na uhodari wake na uzoefu wake, 1995 wengi walimtabiria Makweta au P. Kimiti kuwa Waziri Mkuu lakini Mkapa akamuibua Sumaye.

2. KUTOBAGUA WAGENI OFISINI
Daima Makweta hakua na ubaguzi kwani aliona binadamu wote ni sawa. Ofisini kwake ilikua ni "First come, first served". Ni tofauti na ofisi za viongozi wengi ambapo si jambo la ajabu mtu ukafika saa moja lakini kibopa au mhindi akaja saa nne akatangulia yeye. Kwa Makweta hilo lilikua ni mwiko.

3. HAKUWA FISADI
Makweta licha ya kupata nafasi nyingi za ccm na serikalini hakupata hata siku moja kua na fikra za kujitajirisha kama kua na jumba kama la Ubalozi wa Afrika ya Kusini etc. Viongozi wengi wanapopata nafasi serikalini basi wao kitu pekee wakiwazacho ni dili na rushwa mf Waziri mmoja wa Ardhi 1993-95 kazi yake kubwa ilikua ni kuuza open spaces kwa matajiri pamoja na maeneo mengine nyeti kwa wahindi na hivyo kupata utajiri mkubwa! Inashangaza watu kuuliza kiongozi huyu kapataje utajiri huu wakati hata Baba wa Taifa alisema kwa umri wake mdogo kwa nchi kama yetu asingekua na utajiri huo. Wapambe wake daima hudai eti kaupata kutokana na kuuza ngombe wa urithi!

4.KANISANI
Makweta daima alikua akitoa sadaka kama wakristu wengine kwa kufuata utaratibu uliowekwa. Kuna bwana mmoja mwenye uchu wa kwenda Ikulu anaogopwa hadi kanisani kwake maeneo ya posta ambako baada ya waumini wengine kutoa sadaka yeye na familia yake hupeleka sadaka kwenye vikapu kwa padr huku waumini wengine wakiwa wamekaai!

5. NYUMBA YA KAWAIDA
Kijijini kwake Njombe, Makweta aliishi nyumba ya kawaida na maisha ya kawaida sana. Hata hapa Dsm kule Boko Makweta aliishi na Wagogo na kuongea nao kama vile hakuwahi kua na cheo kikubwa serikalini! Aliishi maisha sawa na aliowaongoza na kuutendea haki ushauri uliotolewa na Nyerere 7.7.1985 "Politicians lifestyles should never be far removed from the electorate". Huyu ni tofauti na baadhi ya viongozi wanaoutaka Urais na wana Majumba karibu kila mkoa. Tumeona wakati Uncle Hashim Lundenga na Mamiss TZ majuzi walivyomtembelea Kigogo mmoja Monduli akiwa ndani ya "Kasri lake la kufa mtu huku wanavijiji wakiwa na nyumba za mbavu za mbwa!

6.MBUNIFU HODARI
Katika kila wizara alikopita alibuni jambo jipya na zuri ambalo linakumbukwa hadi leo mfano Mitihani ya kidato cha pili. Sio kama wengine eti walibuni njia tatu za kupita asb na jioni matokeo yake ni kuzidisha foleni na kuongeza ajali!

7. KUWAENDELEZA WATU WAKE
Alifanya kazi kubwa kuwaendeleza watu wa jimbo lake. Aliinua elimu, alijenga barabara, umeme, maji RTC etc . Hii ni tofauti na wabunge wengine eg wale wenye uchu wa Urais lakini majimbo yao yako dhoful hali mf idadi ya Wamasai wanaoikimbia Monduli kuja mijini kutafuta kazi imekua ikiongezeka kwa kasi sana. Wamasai wengi sasa wamekua ni wasusi na walinzi!!! Hii ni aibu kubwa kwa "Mtu Mzima". Aidha lindi la umaskini linazidi kuongezeka na wafugaji wanazidi kuwa na hali mbaya! Hivi hizo hela zenu chafu mnazozigawa misikitin na makanisan kwanini msiwaendeleze hawa Wamasai??? Hivi mkishindwa 2015 mtaendelea kutoa hizi hela makanisani na miskitini kweli?

8. ALIICHUKIA SANA RUSHWA
Makweta daima alikua kipenda sana kuitaja Ahadi ya 5 ya Mwanatanu, 1965 "Cheo ni dhamana sitatoa wala kupokea rushwa. Vitendo vyake vilidhihirisha pasipo shaka kwamba aliamini kile anachokisema. Utashangaa kuna Mheshimiwa mmoja bila woga wala aibu akiwa Ujerumani kutibiwa nae alijitutumua eti nae alidai anachukia sana rushwa ila akamsifia Hosea kwa utendaji wake mzuri na eti pccb iendelezwe!Ndio lazma ampongeze Hosea si alimsafisha tuhuma za Richmondul eti uchunguzi haujabaini lolote baya!si Hosea huyuhuyu ameshindwa kufanya lolote chaguzi za NEC ambazo rushwa ilikua ikigawiwa vyooni hadi utu wa mwanadamu hauthamini?? Makweta aliona fahari kushindwa kuliko kutoa rushwa! Akiongea na Mwananchi 20.8. 2010 alisema rushwa ilitawala sana kura za maoni ccm njombe. Mfanyabiashara D. Sanga aka Jah People alihonga sana usiku na mchana na kuwatumia wafuasi wake wamtukane Makweta majukwaani.Deo Sanga ndiye pia aliyehonga mno Uenyekiti wa ccm mkoa wa Iringa na kumshinda P. Mangula ambae nae alilalamika mno matumizi makubwa ya rushwa.

9.HAKUTOA MAAMUZI YA KIDIKETA
Makweta daima alikua ni mtu mwenye kutumia busara wakati wa kufanya maamuzi. Kwake yeye kila jambo alilitolea uamuzi mara moja na hakupenda kulaza kazi-viporo. Kabla ya kufanya maamuzi alifikiri kwa kina na kisha kutoa uamuzi. Yeye ni tofauti na wengine ambao kwa kupenda sifa za kijinga hata wakiwa kwenye majukwaa ya siasa hufukuzilia mbali viongozi bila hata ya kusikia upande wao unasemaje. Viongozi hawa wakipewa nchi hawatakua na tofauti na Idd Amini ambae naye alikua akitoa maamuzi ya kipumbavu kama hayo!

10. HAKUWA MBINAFSI
Katika maisha yake yote hakuwa mbinafsi. yeye mara zote alipenda kugawana na wenzake na pia kushauri ili wengine nao waweze kufaidika

Great thinkers, the ball is now in your court!

Hakuwa na tabia ya kupendelea watu wa kwao, Kama walivyofanya wanyalukolo miaka ya karibuni
 
Galiya nashukuru kwa uchambuzi wako, lakini nafikiri hukuwa unamfahamu vizuri huyu mzee. Ni kweli anaweza akawa alikuwa sio fisadi kiivo, lakini swala la kusaidia watu wa jimbo lake si kweli kama alisaidia ni kidogo sana lulinganisha na na muda aliokaa kama kiongozi. Pia alikuwa mbinafsi sana na mtu wa kujivuna, alidiriki kusema katika jimo lake akuna mtu anayeweza kuliongoza kama mbunge labda mtoto wake aliyekuwa akisoma Uingereza amalize shule ngio aje kuchukua nafasi yake. Hua sisahau, R.I.P J.M

Ingawa posting nzima inaelemea kumshambulia Lowasa na CCM nzima.Ila pia ukiangalia suala la kusaidia watu ninegomba utuletee maelezo kuhusu hao watu alioshindwa wasaiidia.kama ni watu waliokuwa wakitaka awape hela cash za k utosh maliza shida zao,ni wazi ingekuwa ngumu kwake.Hasa kwa watu waliopoenda mtu kuwa na sifa, na kujituma tafuta kitu na yeye kusaidia kumpa mawazo, hela za kulipia ada na si kumpati amtu upendeleo.
 
Unaweza kuwa na hoja Galiya, but I think it's a bit too little and a bit too late.

Mzee Makweta, RIP, angepaswa kufanya zaidi kwa nchi hii hasa hapa mwishoni. Mimi naamini mtu yeyote mwenye nia njema na maslahi mapana hawezi kukaa CCM ya sasa. Kwanza hakuna nafasi ya kutoa maoni kwa uhuru na wala huwezi kushiriki kukemea vitendo vya ufisadi (i.e. utamaduni wa CCM) na wigo wao wa demokrasia ni finyu mno.

Marehemu naweza kumfananisha na akina Mzee Joseph Butiku & Salim Ahmed Salim etc. To me as long as they remain inactive but safely there, then indirectly they're part of the big scum, the big lie. Sio lazima waende CDM, NCCR au CUF. At least waunde au wajiunge na movements/harakati za kiukombozi. Just get something done rather than periodic hot words. Becuase the stinking Tanzania is now sinking!

"Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi" Yakobo 4;17
 
BIJOU umesema "hakuna na tabia ya kupendelea watu wa kwao kama wafanyavyo wananylukolo miaka ya hivi karibuni" Je ni wanyalukolo gani hao? Tiririka
 
RONALD REAGAN

Umesema Makweta au mtu mwingine yeyote hawezi kua mtu mzuri eti tu kwa vile yuko CCM...Hii ni ajabu sana. Hivi CHADEMA ndiko waliko malaika? Mbona visa na vituko vyao wengi tunavifahamu? Wengine walikua na skandali lukuki wakiwa mashuleni, vyuoni na hata mitaani na wanachpsubiri ni kupata madaraka ya nchi tu ndo mtajua jinsi walivyokua mafisadi. Hivi hamuoni jinsi migogoro isiyoisha katika hivyo vyama kuhusu ruzuku?

Hivi wazee kama Mzee I. Kaduma ambae amejitolea sana kwa nchi hii na kuelezea miiko hata kwenye vitabu bado mtamwita fisadi kwa vile tu yuko ccm??
 
NAKAPANYA

Mi ningetegemea ueleze ni jinsi gani ulivyomfahamu mzee huyu ukilinganisha na WENYE UCHU WA KWENDA IKULU INGAWA HATA BABA WA TAIFA ALIISHAWAKATAA NA WATANZANIA WAMECHOSHWA NA UFISADI WAO!
 
BIJOU umesema "hakuna na tabia ya kupendelea watu wa kwao kama wafanyavyo wananylukolo miaka ya hivi karibuni" Je ni wanyalukolo gani hao? Tiririka

Angalia post ya Wildcard hapo juu!!!!
 
Sifa hizo Mzee Makweta nastahili kupewa, ila ulipochemka ni kila pointi ulikuwa unamlinganisha na Lowassa. Nchi hii ni zaidi ya Lowassa, iko mifisadi mingi sana mingine. Lowassa kaondoka serikalini 2008, nchi imesongambela au imerudi nyuma? Sina nia ya kumtetea Lowassa kwamba sio fisadi ila nilitaka tumtofasutishe makweta na viongozi wote ambao ni mafisadi akiwemo JK, Membe, Sitta, Kinana, RA, Chenge e.t.c
 
Back
Top Bottom