J.M. Makweta alizaliwa 15.6.1943 na amefariki 17.11.2012 wodi ya Mwaisela, hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo na figo. Nawapa pole sana wafiwa wote.
Mwaka 1975 akiwa Mwalimu IDM Mzumbe aligombea Ubunge Njombe Kaskazini na mwanafunzi wake chuoni hapo A. Makinda aliyekua machachali sana chuoni hapo akagombea Ubunge Njombe Kusini na wote wakashinda. Huo ndo ulikua ni mwanzo wa harakati za sias za marehemu J.M. Makweta.Alikua Mbunge kwa miaka 35 (1975-2010). Pia alikuwa Waziri katika Wizara mbalimbali eg Ofisi ya Waziri Mkuu, Elimu, Kilimo, Jeshi la Kujenga taifa na pia Mawasiliano.Binafsi nimejifunza mambo mengi toka marehemu Makweta kama ifuatavyo;
1. MCHAPAKAZI HODARI
Makweta alikua ni mchapakazi sana na kazini alikua akiingia saa moja na mara nyingi kutoka usiku wa manane. Aidha sehemu zote alizofanya kazi alipendwa mno na wafanyakazi. Makweta ni tofauti na viongozi wengi mfano PM mmoja ambae ana uchu sana wa kutaka kwenda Ikulu wakati akiwa PM, alikua akitoka kazini saa 9.30 na kwenda nyumbani kwaajili ya kuanza kupanga dili za rushwa!Ukikuta yumo ofisni baada ya muda wa kazi basi ujue kuna dili inachongwa! Kutokana na uhodari wake na uzoefu wake, 1995 wengi walimtabiria Makweta au P. Kimiti kuwa Waziri Mkuu lakini Mkapa akamuibua Sumaye.
2. KUTOBAGUA WAGENI OFISINI
Daima Makweta hakua na ubaguzi kwani aliona binadamu wote ni sawa. Ofisini kwake ilikua ni "First come, first served". Ni tofauti na ofisi za viongozi wengi ambapo si jambo la ajabu mtu ukafika saa moja lakini kibopa au mhindi akaja saa nne akatangulia yeye. Kwa Makweta hilo lilikua ni mwiko.
3. HAKUWA FISADI
Makweta licha ya kupata nafasi nyingi za ccm na serikalini hakupata hata siku moja kua na fikra za kujitajirisha kama kua na jumba kama la Ubalozi wa Afrika ya Kusini etc. Viongozi wengi wanapopata nafasi serikalini basi wao kitu pekee wakiwazacho ni dili na rushwa mf Waziri mmoja wa Ardhi 1993-95 kazi yake kubwa ilikua ni kuuza open spaces kwa matajiri pamoja na maeneo mengine nyeti kwa wahindi na hivyo kupata utajiri mkubwa! Inashangaza watu kuuliza kiongozi huyu kapataje utajiri huu wakati hata Baba wa Taifa alisema kwa umri wake mdogo kwa nchi kama yetu asingekua na utajiri huo. Wapambe wake daima hudai eti kaupata kutokana na kuuza ngombe wa urithi!
4.KANISANI
Makweta daima alikua akitoa sadaka kama wakristu wengine kwa kufuata utaratibu uliowekwa. Kuna bwana mmoja mwenye uchu wa kwenda Ikulu anaogopwa hadi kanisani kwake maeneo ya posta ambako baada ya waumini wengine kutoa sadaka yeye na familia yake hupeleka sadaka kwenye vikapu kwa padr huku waumini wengine wakiwa wamekaai!
5. NYUMBA YA KAWAIDA
Kijijini kwake Njombe, Makweta aliishi nyumba ya kawaida na maisha ya kawaida sana. Hata hapa Dsm kule Boko Makweta aliishi na Wagogo na kuongea nao kama vile hakuwahi kua na cheo kikubwa serikalini! Aliishi maisha sawa na aliowaongoza na kuutendea haki ushauri uliotolewa na Nyerere 7.7.1985 "Politicians lifestyles should never be far removed from the electorate". Huyu ni tofauti na baadhi ya viongozi wanaoutaka Urais na wana Majumba karibu kila mkoa. Tumeona wakati Uncle Hashim Lundenga na Mamiss TZ majuzi walivyomtembelea Kigogo mmoja Monduli akiwa ndani ya "Kasri lake la kufa mtu huku wanavijiji wakiwa na nyumba za mbavu za mbwa!
6.MBUNIFU HODARI
Katika kila wizara alikopita alibuni jambo jipya na zuri ambalo linakumbukwa hadi leo mfano Mitihani ya kidato cha pili. Sio kama wengine eti walibuni njia tatu za kupita asb na jioni matokeo yake ni kuzidisha foleni na kuongeza ajali!
7. KUWAENDELEZA WATU WAKE
Alifanya kazi kubwa kuwaendeleza watu wa jimbo lake. Aliinua elimu, alijenga barabara, umeme, maji RTC etc . Hii ni tofauti na wabunge wengine eg wale wenye uchu wa Urais lakini majimbo yao yako dhoful hali mf idadi ya Wamasai wanaoikimbia Monduli kuja mijini kutafuta kazi imekua ikiongezeka kwa kasi sana. Wamasai wengi sasa wamekua ni wasusi na walinzi!!! Hii ni aibu kubwa kwa "Mtu Mzima". Aidha lindi la umaskini linazidi kuongezeka na wafugaji wanazidi kuwa na hali mbaya! Hivi hizo hela zenu chafu mnazozigawa misikitin na makanisan kwanini msiwaendeleze hawa Wamasai??? Hivi mkishindwa 2015 mtaendelea kutoa hizi hela makanisani na miskitini kweli?
8. ALIICHUKIA SANA RUSHWA
Makweta daima alikua kipenda sana kuitaja Ahadi ya 5 ya Mwanatanu, 1965 "Cheo ni dhamana sitatoa wala kupokea rushwa. Vitendo vyake vilidhihirisha pasipo shaka kwamba aliamini kile anachokisema. Utashangaa kuna Mheshimiwa mmoja bila woga wala aibu akiwa Ujerumani kutibiwa nae alijitutumua eti nae alidai anachukia sana rushwa ila akamsifia Hosea kwa utendaji wake mzuri na eti pccb iendelezwe!Ndio lazma ampongeze Hosea si alimsafisha tuhuma za Richmondul eti uchunguzi haujabaini lolote baya!si Hosea huyuhuyu ameshindwa kufanya lolote chaguzi za NEC ambazo rushwa ilikua ikigawiwa vyooni hadi utu wa mwanadamu hauthamini?? Makweta aliona fahari kushindwa kuliko kutoa rushwa! Akiongea na Mwananchi 20.8. 2010 alisema rushwa ilitawala sana kura za maoni ccm njombe. Mfanyabiashara D. Sanga aka Jah People alihonga sana usiku na mchana na kuwatumia wafuasi wake wamtukane Makweta majukwaani.Deo Sanga ndiye pia aliyehonga mno Uenyekiti wa ccm mkoa wa Iringa na kumshinda P. Mangula ambae nae alilalamika mno matumizi makubwa ya rushwa.
9.HAKUTOA MAAMUZI YA KIDIKETA
Makweta daima alikua ni mtu mwenye kutumia busara wakati wa kufanya maamuzi. Kwake yeye kila jambo alilitolea uamuzi mara moja na hakupenda kulaza kazi-viporo. Kabla ya kufanya maamuzi alifikiri kwa kina na kisha kutoa uamuzi. Yeye ni tofauti na wengine ambao kwa kupenda sifa za kijinga hata wakiwa kwenye majukwaa ya siasa hufukuzilia mbali viongozi bila hata ya kusikia upande wao unasemaje. Viongozi hawa wakipewa nchi hawatakua na tofauti na Idd Amini ambae naye alikua akitoa maamuzi ya kipumbavu kama hayo!
10. HAKUWA MBINAFSI
Katika maisha yake yote hakuwa mbinafsi. yeye mara zote alipenda kugawana na wenzake na pia kushauri ili wengine nao waweze kufaidika
Great thinkers, the ball is now in your court!