Jackson Mvangila Makwetta: Tofauti 10 Kati yake na Mafisadi

POPIEXO

Una ushahidi wa hicho ukisemacho? We unaonekana una chuki binafsi na marehemu eti ni mtoto wake tu ndo atakuja kuongoza!!! Kwa sisi tuliomfahamu vzr hawezi kutoa kauli kama hiyo. Muulize yeyote aliyefanya nae kazi. JIPANGE
Alitoa kauli hiyo na nilikuwepo kwenye huo mkutano. Binafsi nachukulia kama vijembe vya kisiasa kwa sababu alikuwa anapambana na Jah People mwenye elimu ya darasa la saba. Hata hivyo Mzee Makweta ni kiongozi bora wa kitaifa kuliko wote waliowahi kuzaliwa Njombe
 
wengine vilaza wa somo la siasa enzi hizo tulikuwa angalau tunaambulia swali moja la waziri wa Elimu ni nani?? enzi hizo jawabu lilikuwa ni moja JACKSON MAKWETA. RIP MAKWETA na Mungu aipe faraja familia nzima.
 
POLITIK

Mkuu umenikumbusha mbali. Nakumbuka mitihani ya primary wakati ule ilikua inauliza mf Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo Mijini ni.... Unajibu Thabita Siwale..wale ndo walikua viongozi wazalendo na wenye kuipenda nchi sio kama hawa akina nanii wakipewa Wizara ya Ardhi kazi yao kuwauzia wahindi kwa rushwa!
 
Galiya nashukuru kwa uchambuzi wako, lakini nafikiri hukuwa unamfahamu vizuri huyu mzee. Ni kweli anaweza akawa alikuwa sio fisadi kiivo, lakini swala la kusaidia watu wa jimbo lake si kweli kama alisaidia ni kidogo sana lulinganisha na na muda aliokaa kama kiongozi. Pia alikuwa mbinafsi sana na mtu wa kujivuna, alidiriki kusema katika jimo lake akuna mtu anayeweza kuliongoza kama mbunge labda mtoto wake aliyekuwa akisoma Uingereza amalize shule ngio aje kuchukua nafasi yake. Hua sisahau, R.I.P J.M

Be corrected. Mzee Makwetta alibahatika kupata watoto watatu, mmoja wa kiume ambaye ni marehemu na wawili wa kike amabo wameolewa sasa hivi. Huyo wa kiume (RIP) hakuwahi kufika Chuo na ninavyojua mimi hawa wa kike hawajawahi kusoma Uingereza. Mzee Makwetta hakuwa mtu wa hivyo.

We all know alikuwa akipambana na changamoto za maisha kama watu wengine na watu walikuwa wakimuuliza " Hivi wewe ni waziri kweli?"

Nyumba yake ya Boko ameingia wakati bado hata haijaisha vizuri na ile ya Njombe Hagafilo ni ndogo mno na ya kawaida sana. Matibabu yake yalikuwa ni Lugalo Military Hospital.

Uadilifu wake wote huo ulifanya awe out of tune. Its sad kuona watu wanamlaumu kwamba ameacha familia yake kwenye shida.
 
We need to learn a lot from this one of the great son of our beloved country! Alikua mfano mzuri sana wa kuigwa hasa kwenye suala la uadilifu (corruption free mind). Nakumbuka wakati wa utawala wa Ben, J.M. alipostaafu ulifika wakati wa kuondoka kwenye nyumba ya serikali.

Mzee J. M. akajikuta hana kwa kwenda kwani nyumba yake ya Boko ilikua ndio kwanza inaanza kujengwa. Kwa kiburi cha uadilifu aliokua nao (ingawa haikua sahihi kisheria na kanuni) alikataa kuondoka kwenye nyumba kwa maelezo kuwa bado hana nyumba hapa Dar na kwa vile kalitumikia Taifa kwa uaminifu hana kwa kwenda zaidi ya kubaki kwenye nyumba ya serikali hadi amalize kujenga nyumba yake!!

Wahusika walipolipeleka jambo hili mbele inasemekana official permission ilitolewa ili mzee J.M. alipewa muda zaidi kuendelea kukaa hapo ili aweze kumalizia nyumba yake. Waweza kutafsiri kuwa alikua mzembe kutokua na nyumba au pia kuwa alivunja sheria na kanuni kukataa ku-vaccate nyumba ya serikali...lakini mimi nimepata fundisho moja kuwa alikua na KIBURI KINACHOTOKANA NA UADILIFU NA UAMINIFU - the J.K. Nyerere style!
 
We need to learn a lot from this one of the great son of our beloved country! Alikua mfano mzuri sana wa kuigwa hasa kwenye suala la uadilifu (corruption free mind). Nakumbuka wakati wa utawala wa Ben, J.M. alipostaafu ulifika wakati wa kuondoka kwenye nyumba ya serikali.

Mzee J. M. akajikuta hana kwa kwenda kwani nyumba yake ya Boko ilikua ndio kwanza inaanza kujengwa. Kwa kiburi cha uadilifu aliokua nao (ingawa haikua sahihi kisheria na kanuni) alikataa kuondoka kwenye nyumba kwa maelezo kuwa bado hana nyumba hapa Dar na kwa vile kalitumikia Taifa kwa uaminifu hana kwa kwenda zaidi ya kubaki kwenye nyumba ya serikali hadi amalize kujenga nyumba yake!!

Wahusika walipolipeleka jambo hili mbele inasemekana official permission ilitolewa ili mzee J.M. alipewa muda zaidi kuendelea kukaa hapo ili aweze kumalizia nyumba yake. Waweza kutafsiri kuwa alikua mzembe kutokua na nyumba au pia kuwa alivunja sheria na kanuni kukataa ku-vaccate nyumba ya serikali...lakini mimi nimepata fundisho moja kuwa alikua na KIBURI KINACHOTOKANA NA UADILIFU NA UAMINIFU - the J.K. Nyerere style!

Hakuwa na mipangilio mizuri na ndio maana hakuweza kulisaidia jimbo lake la njombe. Kwanza lazima tufahamu kutokujenga nyumba sio kiashilia cha uadilifu au kujenga nyumba sio kiashilia cha ufisadi. Kushindwa kuandaa maisha yako ya badae wewe kama wewe ni uzembe mkubwa, unataka kusema mshahara wake alikuwa anapeleka wapi? Anagaia maskini? Tuache kutoa sifa za kijinga.
 
RIP JACKSON Makweta daima tutakukumbuka, ubarikiwe na tutazidi kukuombea ili ufike Mbinguni kwa baba.
Rip makweta haya manyangau ya siku hizi yasingekubali fia Muhimbili maana yanaleta ubichololo hadi kwenye kifo
 
Galiya nashukuru kwa uchambuzi wako, lakini nafikiri hukuwa unamfahamu vizuri huyu mzee. Ni kweli anaweza akawa alikuwa sio fisadi kiivo, lakini swala la kusaidia watu wa jimbo lake si kweli kama alisaidia ni kidogo sana lulinganisha na na muda aliokaa kama kiongozi. Pia alikuwa mbinafsi sana na mtu wa kujivuna, alidiriki kusema katika jimo lake akuna mtu anayeweza kuliongoza kama mbunge labda mtoto wake aliyekuwa akisoma Uingereza amalize shule ngio aje kuchukua nafasi yake. Hua sisahau, R.I.P J.M
Kwa wale wanaoifahamu njombe kabla ya mwaka 80 na sasa wanaelewa vema mchango wa Mzee Makwetta. Nakumbuka alivyoanzisha taasisi za kiuchumi kama mabenki, simu,posta, umeme,kilimo,kampeni za ujenzi wa nyumba bora, lami ya makambako-njombe-songea,shule n.k. RIP Jackson
 
sioni tatizo la mchambuzu maana wanaccm wanajijua mafisadi kiongozi wao ni nani! eaulize waliogombea nafasi mbalimbali watakwambia aliywaliza nani
 
Nilizaliwa na kuwa na ufahamu wewe ulikuwa mbunge.
Nilisoma shule ya msingi,uliendelea kuwa mbunge.
Nilihitimu elimu ya sekondari ukawa bado mbunge.
Nilikwenda kusoma chuo majuu,narudi wewe bado mbunge.
Nikaoa na kupata watoto,bado wewe ukawa mbunge wao,yaani mimi mke,watoto,wazazi wangu na bibi yangu.
Ndipo nafsi yangu ikaona si busara wewe kuwa kiongozi wa milele.Nilikupinga mwaka 2000,ukanishinda,nikarudia tena 2005,ukanishinda katika mazingira magumu sana.2010 nikaingia kwenye njia unayopitia nikakushinda lakini haikunitosha kuwa mbunge wala diwani.Kisa,fisadi mwingine akaingilia mchezo nikadhulumiwa haki.Njia pekee nikaamua kurudi nyumbani nilikolelewa yaani CDM.
Juzi kabla ya kuanza safari ya milele ulinipa maneno ya mwisho uliposema,"si lazima uwe mbunge ili uwasaidie wabena na wakinga na makabila yote yaNjombe" Kisha katika hali ya kutafakarisha ulimtuma kijana wako wa kazi ukamwelekeza anitembeze katika maktaba yako nzuri ya vitabu mbalimbali na ukaniagiza nikuandalie wasomi na watu wote wenye mapenzi mema na mkoa wa Njombe ili uongee nao.Siku moja kabla ya kuja kukuona nilikukuta karibu na Benki ya NBC NJOMBE ukiwa na na familia yako na mhudumu wa afya mmoja ukielekea Ikonda Hospital kwaajili ya matibabu.Sikumbjili baadaye tulijulishwa kuwa umekimbizwa Lugalo hospital na hatimaye Muhimbili.Jumamosi ya tarehe 17.11.2012
nilijulishwa na mtu wa karibu kuwa Mungu alimtuma Malaika kuja kukuchukua na kwamba hupo pamoja nasi.Nililia kidogo lakini baadaye nilifarijika kwa imani kuwa sikuwa na ushahidi juu ya maovu ya dhahiri uliyotenda hapa duniani.Nikasema amina,Bwana alitoa na Bwana amepungukiwa na waziri wa elimu kule mbinguni kwenye eneo ambalo watanzania huwa wanapumzikia wakiitwa.:A S cry::A S cry:Lala Makweta,lala kwa amani,ila ukifika mwambie Mungu juu ya uovu unaofanywa na chama cha magamba hapa Tanzania.Kama ukikutana na Nyerere,mwambie akiweza arudi mara moja ili aje awambie hawa jamaa kuwa wanachezea nchi yetu.Kwamba wameuza karibu kila kitu katika nchi hii.Mwambie kuwa kila mtanzania kwa sasa amekata tamaa ya kuishi na kwamba kila mtanzania sasa anaheshimu simu za mchina kuliko hata kazi aliyoajiriwa.Kwamba hata manurse kama wakipigiwa cmu huacha mgonjwa na kuongea kwa cmu zaidi ya dk 20 bila kujali kama mgonjwa anahitaji msaada.
 
RIP Makweta. Ulikuwa waziri wangu mzuri wa elimu. Ulichapa kazi na kujitenga na ufisadi. Nenda na pumzika salama Jake Makweta.
 
J.M. Makweta alizaliwa 15.6.1943 na amefariki 17.11.2012 wodi ya Mwaisela, hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo na figo. Nawapa pole sana wafiwa wote.

Mwaka 1975 akiwa Mwalimu IDM Mzumbe aligombea Ubunge Njombe Kaskazini na mwanafunzi wake chuoni hapo A. Makinda aliyekua machachali sana chuoni hapo akagombea Ubunge Njombe Kusini na wote wakashinda. Huo ndo ulikua ni mwanzo wa harakati za sias za marehemu J.M. Makweta.Alikua Mbunge kwa miaka 35 (1975-2010). Pia alikuwa Waziri katika Wizara mbalimbali eg Ofisi ya Waziri Mkuu, Elimu, Kilimo, Jeshi la Kujenga taifa na pia Mawasiliano.Binafsi nimejifunza mambo mengi toka marehemu Makweta kama ifuatavyo;

1. MCHAPAKAZI HODARI
Makweta alikua ni mchapakazi sana na kazini alikua akiingia saa moja na mara nyingi kutoka usiku wa manane. Aidha sehemu zote alizofanya kazi alipendwa mno na wafanyakazi. Makweta ni tofauti na viongozi wengi mfano PM mmoja ambae ana uchu sana wa kutaka kwenda Ikulu wakati akiwa PM, alikua akitoka kazini saa 9.30 na kwenda nyumbani kwaajili ya kuanza kupanga dili za rushwa!Ukikuta yumo ofisni baada ya muda wa kazi basi ujue kuna dili inachongwa! Kutokana na uhodari wake na uzoefu wake, 1995 wengi walimtabiria Makweta au P. Kimiti kuwa Waziri Mkuu lakini Mkapa akamuibua Sumaye.

2. KUTOBAGUA WAGENI OFISINI
Daima Makweta hakua na ubaguzi kwani aliona binadamu wote ni sawa. Ofisini kwake ilikua ni "First come, first served". Ni tofauti na ofisi za viongozi wengi ambapo si jambo la ajabu mtu ukafika saa moja lakini kibopa au mhindi akaja saa nne akatangulia yeye. Kwa Makweta hilo lilikua ni mwiko.

3. HAKUWA FISADI
Makweta licha ya kupata nafasi nyingi za ccm na serikalini hakupata hata siku moja kua na fikra za kujitajirisha kama kua na jumba kama la Ubalozi wa Afrika ya Kusini etc. Viongozi wengi wanapopata nafasi serikalini basi wao kitu pekee wakiwazacho ni dili na rushwa mf Waziri mmoja wa Ardhi 1993-95 kazi yake kubwa ilikua ni kuuza open spaces kwa matajiri pamoja na maeneo mengine nyeti kwa wahindi na hivyo kupata utajiri mkubwa! Inashangaza watu kuuliza kiongozi huyu kapataje utajiri huu wakati hata Baba wa Taifa alisema kwa umri wake mdogo kwa nchi kama yetu asingekua na utajiri huo. Wapambe wake daima hudai eti kaupata kutokana na kuuza ngombe wa urithi!

4.KANISANI
Makweta daima alikua akitoa sadaka kama wakristu wengine kwa kufuata utaratibu uliowekwa. Kuna bwana mmoja mwenye uchu wa kwenda Ikulu anaogopwa hadi kanisani kwake maeneo ya posta ambako baada ya waumini wengine kutoa sadaka yeye na familia yake hupeleka sadaka kwenye vikapu kwa padr huku waumini wengine wakiwa wamekaai!

5. NYUMBA YA KAWAIDA
Kijijini kwake Njombe, Makweta aliishi nyumba ya kawaida na maisha ya kawaida sana. Hata hapa Dsm kule Boko Makweta aliishi na Wagogo na kuongea nao kama vile hakuwahi kua na cheo kikubwa serikalini! Aliishi maisha sawa na aliowaongoza na kuutendea haki ushauri uliotolewa na Nyerere 7.7.1985 "Politicians lifestyles should never be far removed from the electorate". Huyu ni tofauti na baadhi ya viongozi wanaoutaka Urais na wana Majumba karibu kila mkoa. Tumeona wakati Uncle Hashim Lundenga na Mamiss TZ majuzi walivyomtembelea Kigogo mmoja Monduli akiwa ndani ya "Kasri lake la kufa mtu huku wanavijiji wakiwa na nyumba za mbavu za mbwa!

6.MBUNIFU HODARI
Katika kila wizara alikopita alibuni jambo jipya na zuri ambalo linakumbukwa hadi leo mfano Mitihani ya kidato cha pili. Sio kama wengine eti walibuni njia tatu za kupita asb na jioni matokeo yake ni kuzidisha foleni na kuongeza ajali!

7. KUWAENDELEZA WATU WAKE
Alifanya kazi kubwa kuwaendeleza watu wa jimbo lake. Aliinua elimu, alijenga barabara, umeme, maji RTC etc . Hii ni tofauti na wabunge wengine eg wale wenye uchu wa Urais lakini majimbo yao yako dhoful hali mf idadi ya Wamasai wanaoikimbia Monduli kuja mijini kutafuta kazi imekua ikiongezeka kwa kasi sana. Wamasai wengi sasa wamekua ni wasusi na walinzi!!! Hii ni aibu kubwa kwa "Mtu Mzima". Aidha lindi la umaskini linazidi kuongezeka na wafugaji wanazidi kuwa na hali mbaya! Hivi hizo hela zenu chafu mnazozigawa misikitin na makanisan kwanini msiwaendeleze hawa Wamasai??? Hivi mkishindwa 2015 mtaendelea kutoa hizi hela makanisani na miskitini kweli?

8. ALIICHUKIA SANA RUSHWA
Makweta daima alikua kipenda sana kuitaja Ahadi ya 5 ya Mwanatanu, 1965 "Cheo ni dhamana sitatoa wala kupokea rushwa. Vitendo vyake vilidhihirisha pasipo shaka kwamba aliamini kile anachokisema. Utashangaa kuna Mheshimiwa mmoja bila woga wala aibu akiwa Ujerumani kutibiwa nae alijitutumua eti nae alidai anachukia sana rushwa ila akamsifia Hosea kwa utendaji wake mzuri na eti pccb iendelezwe!Ndio lazma ampongeze Hosea si alimsafisha tuhuma za Richmondul eti uchunguzi haujabaini lolote baya!si Hosea huyuhuyu ameshindwa kufanya lolote chaguzi za NEC ambazo rushwa ilikua ikigawiwa vyooni hadi utu wa mwanadamu hauthamini?? Makweta aliona fahari kushindwa kuliko kutoa rushwa! Akiongea na Mwananchi 20.8. 2010 alisema rushwa ilitawala sana kura za maoni ccm njombe. Mfanyabiashara D. Sanga aka Jah People alihonga sana usiku na mchana na kuwatumia wafuasi wake wamtukane Makweta majukwaani.Deo Sanga ndiye pia aliyehonga mno Uenyekiti wa ccm mkoa wa Iringa na kumshinda P. Mangula ambae nae alilalamika mno matumizi makubwa ya rushwa.

9.HAKUTOA MAAMUZI YA KIDIKETA
Makweta daima alikua ni mtu mwenye kutumia busara wakati wa kufanya maamuzi. Kwake yeye kila jambo alilitolea uamuzi mara moja na hakupenda kulaza kazi-viporo. Kabla ya kufanya maamuzi alifikiri kwa kina na kisha kutoa uamuzi. Yeye ni tofauti na wengine ambao kwa kupenda sifa za kijinga hata wakiwa kwenye majukwaa ya siasa hufukuzilia mbali viongozi bila hata ya kusikia upande wao unasemaje. Viongozi hawa wakipewa nchi hawatakua na tofauti na Idd Amini ambae naye alikua akitoa maamuzi ya kipumbavu kama hayo!

10. HAKUWA MBINAFSI
Katika maisha yake yote hakuwa mbinafsi. yeye mara zote alipenda kugawana na wen..........


















Pamoja na kushukuru kwa mtazamo chanya juu ya mzee wetu Makweta,bado hujatenda haki juu ya Anna Makinda kuwa Mbunge Njombe kusini kuanzia 1975.Nakukumbusha kuwa jimbo la Njombe kusini lilizaliwa 1990 na mbunge wake wa kwanza ni Dr.dr.H.Ngunangwa(Jembe).Anna alikuwa mbunge wa kuteuliwa tangu mwaka huo.Njombbe alianza ubunge 1995.
 
Back
Top Bottom