Ni aliyekuwa mbunge wa huko Njombe na waziri katika serikali ya awamu ya kwanza na ya pili Mhe. Jackson Makwetta amefariki dunia jioni ya leo.
Alazwe pema peponi
Chanzo: Ndugu wa karibu na marehemu.
=======
Fahamu zaidi kuhusu Jackson Makweta
Waziri wa Elimu wa Serikali ya Awamu ya Kwanza Mh Jackson Makweta. Pia aliwahi kuwa waziri wa maji nishati na madini katika awamu ya pili. Aliandika rekodi kwa kushikilia ubunge jimbo la Njombe kaskazini kuanzia mwaka 1975 hadi mwaka 2010 alipong'olewa na Deo Sanga
Mwaka 1982, Tume ya Rais ya Elimu iliyojulikana kama “Tume ya Makweta” ilitoa mapendekezo kuhusu uboreshaji wa mfumo wa elimu na mitaala. Utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya Makweta na utafiti wa TET ulichukua muda mrefu kutokana na mdororo wa kiuchumi wa dunia, ukata ambao pia uliiathiri Tanzania
Ripoti ya Makweta ya 1982 iliyopendekeza kutumia Lugha ya Kiswahili kama Lugha ya Kufundishia masomo yote tangu elimu ya wali hadi Chuo Kikuu huku Kiingereza kikifundishwa vizuri kama somo kwenye Taasisi ya Lugha za Kigeni (Institute of Foreign Languages) na matawi yake nchi nzima
Jackson Makweta alifariki novemba 17, 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MHE. MAKWETTA AFARIKI DUNIA
SERIKALI inasikitika kutangaza kifo cha Bw. Jackson Makwetta kilichotokea leo saa 11 jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ya jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa.
Msiba uko nyumbani kwake Boko kwa Wagogo. Taarifa zaidi kuhusu mipango ya mazishi zitatolewa baadaye.
Bw. Makweta aliwahi kuwa Waziri katika wizara mbalimbali zikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu kama Waziri wa Nchi, Elimu, Kilimo na Utumishi.
Pia amekuwa Mbunge kwa zaidi ya miaka 35.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
DODOMA.
JUMAMOSI, NOVEMBA 17, 2012.