TANZIA Jackson Makwetta (Mbunge na Waziri wa zamani) afariki dunia

kaeso

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
551
96
Ni aliyekuwa mbunge wa huko Njombe na waziri katika serikali ya awamu ya kwanza na ya pili Mhe. Jackson Makwetta amefariki dunia jioni ya leo.

Alazwe pema peponi

Chanzo: Ndugu wa karibu na marehemu.


=======

Fahamu zaidi kuhusu Jackson Makweta


Waziri wa Elimu wa Serikali ya Awamu ya Kwanza Mh Jackson Makweta. Pia aliwahi kuwa waziri wa maji nishati na madini katika awamu ya pili. Aliandika rekodi kwa kushikilia ubunge jimbo la Njombe kaskazini kuanzia mwaka 1975 hadi mwaka 2010 alipong'olewa na Deo Sanga

Mwaka 1982, Tume ya Rais ya Elimu iliyojulikana kama “Tume ya Makweta” ilitoa mapendekezo kuhusu uboreshaji wa mfumo wa elimu na mitaala. Utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya Makweta na utafiti wa TET ulichukua muda mrefu kutokana na mdororo wa kiuchumi wa dunia, ukata ambao pia uliiathiri Tanzania

Ripoti ya Makweta ya 1982 iliyopendekeza kutumia Lugha ya Kiswahili kama Lugha ya Kufundishia masomo yote tangu elimu ya wali hadi Chuo Kikuu huku Kiingereza kikifundishwa vizuri kama somo kwenye Taasisi ya Lugha za Kigeni (Institute of Foreign Languages) na matawi yake nchi nzima

Jackson Makweta alifariki novemba 17, 2012


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MHE. MAKWETTA AFARIKI DUNIA

SERIKALI inasikitika kutangaza kifo cha Bw. Jackson Makwetta kilichotokea leo saa 11 jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ya jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa.

Msiba uko nyumbani kwake Boko kwa Wagogo. Taarifa zaidi kuhusu mipango ya mazishi zitatolewa baadaye.

Bw. Makweta aliwahi kuwa Waziri katika wizara mbalimbali zikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu kama Waziri wa Nchi, Elimu, Kilimo na Utumishi.

Pia amekuwa Mbunge kwa zaidi ya miaka 35.



IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
DODOMA.
JUMAMOSI, NOVEMBA 17, 2012.
 
Mzee huyu alikuwa ni miongoni mwa viongozi wachache wa CCM waliotumikia taifa lao kwa uadilifu na kwa uzalendo wa hali ya juu, akiwa waziri wa serikali kwa miaka 25 mfululizo (1975 - 2000), lakini hakuna mahali alitumia vibaya madaraka yake kwani inasemekana kwamba hata nyumba ya kuishi nje kidogo ya jiji la Dar-es-salaam alijengewa na wanae kabla ya kustaafu na hata hivyo haikukamilika ipasavyo; na katika kipindi karibia chote cha ustaafu wake alikuwa anaishi kwao kijijini;

Lakini kwa vile serikali yetu ya CCM haijali watu kama hawa, msiba wake utaendeshwa kinafiki tu; Misiba yenye kupewa uzito ni ile ya viongozi wasiokuwa wazalendo ambao utashi wao unapimwa kwa utajiri wao; Lakini ipo siku yote haya yatabadilika;

Poleni wafiwa; Mwenyezi mungu amlaze mahali pema peponi Mzee wetu Makweta, Amen;
 
This is sad. He Jakson Makweta was a rare "brand". I once introduced myself to him and when he wondered who was I? I told him he need not wonder as I new him from when I was a kid and am proud of his services as a senior citizen of this country. We had a good laugh. Unfortunately it was during the time that he was sidelined for the reasons that Mkapa and Sumaye know better.
 
R.I.P Great Man MAKWETA
Ni aliyekuwa mbunge wa huko Njombe na waziri katika serikali ya awamu ya kwanza na ya pili Mhe. Jackson Makwetta amefariki dunia jioni ya leo.

Alazwe pema peponi

Chanzo: Ndugu wa karibu na marehemu.
 
1.Explain the objectives of Makwata commission.

Mungu amlaze mahali pema kwa kazi kubwa aliyoifanya kwa taifa hili.

Kwa wale wanaosoma/waliosoma shahada/stashahada za elimu wanaelewa mapendekezo aliyoyafanya kwenye tume yake kuhusu maswala ya elimu na uboreshaji wake kwa ujumla.

Mungu amlaze mahali alipo mpangia. Ameen.
 
R. I. P Makweta umelitumikia taifa lakini mchango wako haujatambulika mpaka wameshindwa kukupeleka lndia.
 
Kijijini kwetu tunamkumbuka sana kwa jinsi alivyopigana kiume mpaka tukapata barabara na RTC enzi hizo akiwa mbunge wa njombe ( Ludew,Makete,Wanging`ombe zilikuwa bado kumegwa). Kweli watu wazuri wanakufa yanabaki manung`ayembe yanayotuhangaisha.

Kwa njombe, alipigania elimu sana kupitia NDDT, shule zikafunguliwa kwa wingi. Mungu amekupenda zaidi.

RIP MAKWETA.
 
hawa ndo wangestahili hata kuzawadiwa v8 kwa utumishi wao badala yake eti Shimbo ndo anapewa v8 ...Mungu amtangulie.amen
 
Waziri wa Zamani
katika Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania,Jackso n Makweta
amefariki dunia jioni katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
 
Back
Top Bottom