BUBERWA D.
JF-Expert Member
- Apr 22, 2011
- 2,293
- 1,170
ripoti yake ya maboresho ya elimu mpaka sasa haijafanyiwa kazi. ndo maana kafa.R.I.P
R I P J MakwettaNi aliyekuwa mbunge wa huko Njombe na waziri katika serikali ya awamu ya kwanza na ya pili Mhe. Jackson Makwetta amefariki dunia jioni ya leo.
Alazwe pema peponi
Chanzo: Ndugu wa karibu na marehemu.
Tujifunze kuthamini watu wakiwa Hai,sifa zote hizi na kumbukumbu ya mazuri yake mngeyasema enzi za uhai wake ili hata watoto waliozaliwa enzi za Mwinyi waijue historia ya viongozi waliopita na kutaka kujua wanafanya nini kwa sasa.
)
Mzee huyu alikuwa ni miongoni mwa viongozi wachache wa CCM waliotumikia taifa lao kwa uadilifu na kwa uzalendo wa hali ya juu, akiwa waziri wa serikali kwa miaka 25 mfululizo (1975 - 2000), lakini hakuna mahali alitumia vibaya madaraka yake kwani inasemekana kwamba hata nyumba ya kuishi nje kidogo ya jiji la Dar-es-salaam alijengewa na wanae kabla ya kustaafu na hata hivyo haikukamilika ipasavyo; na katika kipindi karibia chote cha ustaafu wake alikuwa anaishi kwao kijijini;
Lakini kwa vile serikali yetu ya CCM haijali watu kama hawa, msiba wake utaendeshwa kinafiki tu; Misiba yenye kupewa uzito ni ile ya viongozi wasiokuwa wazalendo ambao utashi wao unapimwa kwa utajiri wao; Lakini ipo siku yote haya yatabadilika;
Poleni wafiwa; Mwenyezi mungu amlaze mahali pema peponi Mzee wetu Makweta, Amen;
Alifanya kazi kubwa sana katika kujenga mji wa Makambako kwani wanaokumbuka Makambako ya miaka ya 80 na 70 ukilinganisha na ya sasa huwezi kuamini.Kijijini kwetu tunamkumbuka sana kwa jinsi alivyopigana kiume mpaka tukapata barabara na RTC enzi hizo akiwa mbunge wa njombe ( Ludew,Makete,Wanging`ombe zilikuwa bado kumegwa). Kweli watu wazuri wanakufa yanabaki manung`ayembe yanayotuhangaisha.
Kwa njombe, alipigania elimu sana kupitia NDDT, shule zikafunguliwa kwa wingi. Mungu amekupenda zaidi.
RIP MAKWETA.
Mzee huyu alikuwa ni miongoni mwa viongozi wachache wa CCM waliotumikia taifa lao kwa uadilifu na kwa uzalendo wa hali ya juu, akiwa waziri wa serikali kwa miaka 25 mfululizo (1975 - 2000), lakini hakuna mahali alitumia vibaya madaraka yake kwani inasemekana kwamba hata nyumba ya kuishi nje kidogo ya jiji la Dar-es-salaam alijengewa na wanae kabla ya kustaafu na hata hivyo haikukamilika ipasavyo; na katika kipindi karibia chote cha ustaafu wake alikuwa anaishi kwao kijijini;
Lakini kwa vile serikali yetu ya CCM haijali watu kama hawa, msiba wake utaendeshwa kinafiki tu; Misiba yenye kupewa uzito ni ile ya viongozi wasiokuwa wazalendo ambao utashi wao unapimwa kwa utajiri wao; Lakini ipo siku yote haya yatabadilika;
Poleni wafiwa; Mwenyezi mungu amlaze mahali pema peponi Mzee wetu Makweta, Amen;
GT tuwe wa kweli na taarifa tunazozitoa.
Je unajua nini wananchi wake wa jimbo lake waliamua kumuondoa kwa kumnyima Kura katika kura za maoni na kushindwa na kijana Mdogo Sanga?
Mola aiweke pahala panapo stahiki Roho ya jackson Makweta.
Je unajua kuwa DEO SANGA (JAH PEOPLE) alitumia nguvu ya pesa kuwaangusha MAKWETTA ubunge na MANGULA uenyekiti wa CCM mkoa? Au ndio kuishi mbali unasahau kwenu? Na huyu Sanga sio bwana mdogo kama unavyotaka tuamini.