Christopher Wallace
JF-Expert Member
- Dec 8, 2015
- 1,410
- 3,548
Kuna wakati tuliaminishwa na Waingereza pamoja na Media zao kuwa Wachezaji vijana wanaocheza kwenye nafasi ya Kiungo, Jack Wilshere wa Arsenal na Tom Cleverley wa Man Utd Kipindi hiko kuwa ni World Class Players yaani Wachezaji wa daraja la juu ambao wangeweza kucheza timu yoyote ile Ulimwenguni.
Ilifika kipindi wakawa wanawapambanisha kati ya Wilshere na Cleverley ni nani zaidi? Hata Kocha wa zamani wa Man Utd aliwahi kukaririwa akisema Cleverley ni "Scholes Mpya" na akafikia kumuweka nje Rooney kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Man Utd dhidi ya Real Madrid ili acheze Cleverley. Vijana hao wakaaminiwa zaidi hadi kwenye timu yao ya taifa wakawa ni sehemu ya kikosi cha kwanza cha timu ya taifa ya England.
Wachezaji wenzao vijana ambao walichipukia nao kwasasa ni matured ni kama akina Toni Kroos wa Real Madrid, Draxler wa PSG nk
Miaka imesogea, leo hii Wilshere yupo Bournemouth kwa mkopo tena akipigania namba huku Cleverley akiwa Watford kwa mkopo akitokea Everton, Je nini kiliwasibu vijana hawa ambao walichipukia vizuri sana lakini kwasasa hali zao uwanjani zikiwa hoi bin taabani?
Karibuni wanajukwaa kwa Mjadala...