Jack Warner ajiuzulu kama naibu mkuu wa FIFA

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,985
20,263
Naibu rais wa shirikisho la soka ulimwenguni FIFA Jack Warner, ambaye aliangaziwa zaidi katika madai ya hivi karibuni ya rushwa katika shirikisho hilo, amejiuzulu wadhifa wake. Hayo yamethibitishwa hii leo na shirikisho hilo. Warner aliyekuwa kiongozi mwenye ushawishi mkubwa wa shirikisho la soka la eneo la Karibik, Amerika ya kaskazini na ya kati - CONCACAF, aliachishwa kazi kwa muda mwezi jana kufuatia madai kuwa alishirikiana na mkuu wa shirikisho la soka barani Asia Mohammed bin Hammam kununua kura katika jaribio la kumwondoa uongozini kiongozi wa sasa wa FIFA Sepp Blatter katika uchaguzi wa rais uliofanywa mapema mwezi huu.
 
Back
Top Bottom