Jack Grealish asaini mkataba mpya wa miaka mitano nwa kuendelea kusalia kuichezea Aston Villa

Last Seen

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
223
549
Nahodha wa klabu ya Aston Villa ya nchini Uingereza Jack Grealish amesaini mkataba mpya wa miaka mitano na klabu yake ya Aston Villa utakaomfanya asalie klabuni hapo Hadi mwaka 2025.

Jack Amekuwa mshambuliaji hatari katika msimu huu wa ligi kuu ya Uingereza, na ndio mchezaji anayeongoza kuchezewa madhambi zaidi "fouls".

Kabla ya mkataba huu mshambuliaji huyu mwenye umri wa miaka 24 alihusishwa kujiunga na klabu ya Barcelona ya uhispania pamoja na klabu ya Manchester United.

======

Aston Villa Football Club is delighted to announce Club Captain Jack Grealish has signed a new five-year contract.

The 25-year-old’s new deal will see him remain at Villa Park until 2025.

Jack has been with his hometown club since he was eight-years-old and made his claret and blue debut at the end of the 2013/14 season. He remained with Villa despite relegation in 2016 and was pivotal in our return to the top-flight last year.

In our first season back in the Premier League, Jack was instrumental in the team’s survival and was capped by England for the first time earlier this month.

CEO Christian Purslow said: “Jack is an emblem of our Owner’s vision for Aston Villa. He joined our Club as a local boy aged six and has developed into one of the country’s finest players finally becoming a full England international last week.

“We are determined to build a top team around him and are delighted that he is extending his contract and committing himself to the club he loves.”

Jack Grealish said: “I am delighted to make this commitment to Villa. It is my club, my home and I am very happy here. The owners have made it very clear to me how ambitious they are and how they want to build Aston Villa. There are exciting times ahead and I am very glad to be part of it.”

avfcofficial___CFJ8xlksKKr___.jpg

Source: Aston Villa official site
 
Mbona wabongo humchukia sana huyu jamaa
Wabongo wengi wanamchukia sana Grealish kwa sababu wanaamini kwamba anamnyima pass Mbwana Samatta! Hata hapa mtaani alikuwa anachukiwa sana yule mwamba. Lakini ukweli mchungu ni kwamba Jack Grealish ni mchakarikaji sana na umri bado unaruhusu lakini Mbwana Samatta hana kiwango cha kutosheleza kucheza EPL.

Mwanzo nilikuwa siifuatilii Aston Villa wala kumfahamu mchezaji yeyote pale zaidi ya kusikia tu kuna kijana wetu pale. Lakini baada ya kusikia sana mitaani ...ooohh kuna na.10 anamnyima pass Samatta... Nikaamua kuifuatilia Aston Villa baada ya corona ili nione huyu anayemnyima pass Samatta wetu ni nani?! Nikawaambia na wadau tushirikiane kuwafuatilia wote wawili ili waache kumbebesha lawama za bure yule chalii.

Hadi msimu unaisha nilijiridhisha pasi na shaka kwamba Grealish ni mchakarikaji sana kiasi kwamba ni halali yake hata kupewa unahodha. Na wadau wa kitaa walikubali pia na kuacha kumlaumu, tulikubaliana kijana wetu uwezo hautoshelezi kumshindanisha na Grealish, yaani amemuacha mbali sana!

Mchezaji anayechezewa rafu nyingi zaidi hawezi kuwa boya. Namkubali sana yule mdau, ananikumbusha upambanaji wa Hazard pale darajani na alivyokuwa anaburuzwa chini kila wakati. Kwakuwa kabaki nitaendelea kuifuatilia Aston Villa.
 
Aston villa wanamkubali uyo jamaa ila sioni anachofanyaa uwanjani
Amewabakisha kwenye ligi kuu. Upambanaji wake umewaokoa kushuka daraja. Aston Villa nzima, kuanzia wamiliki hadi waokota mipira na mashabiki wote wanalijua hilo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom