J2K Ingizo jipya katika Bongo flava apanga kuing'arisha Mkuranga

KAMBOTA

Senior Member
Joined
Mar 21, 2011
Messages
176
Points
0

KAMBOTA

Senior Member
Joined Mar 21, 2011
176 0
Na Nova Kambota , 27 Nov 2012
J2K.jpg

Kijana anayechipukia katika miondoko ya bongo flava kutoka pande za Mkuranga anayekwenda kwa jina la Juma Thabit a.k.a J2K ameibuka na kudai kuwa sasa amejipanga vikali kuonyesha kipaji chake katika mziki huo wenye mashabiki wengi vijana.

Akipiga stori kutoka maskani yake yaliyoko Mkuranga J2K amefafanua kwa kirefu azma yake ya kuhakikisha kuwa anaachia vibao vikali vitakavyoteka hisia za mashabiki wake na anga la muziki kwa ujumla.

Tayari mpaka sasa mkali huyo amesharekodi vibao kadhaa kama vile wameshindwa, Nenda salama na nyinginezo katika studio ya Chapa Two records sambama na HD record zote za Tabata jijini Dar es salaam.

J2K pia ameomba sapoti ya wadau wa mziki hususani mapromota ili kumsaidia kuingiza sokoni albamu yake aliyodai ina vibao vikali na vyenye ujumbe mzito!

Kwa mawasiliano zaidi na J2K waweza kuwasiliana naye kupitia namba 0652 907711
 

Forum statistics

Threads 1,392,816
Members 528,722
Posts 34,118,751
Top