J. Makamba:- Mgao wa umeme kuwepo 2012 hadi 2013 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

J. Makamba:- Mgao wa umeme kuwepo 2012 hadi 2013

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwitaz, Apr 9, 2012.

 1. mwitaz

  mwitaz JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 314
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  wana JF,
  Umeme una manufaa makubwa kwa maisha ya kila siku kwa binadamu na endapo kukawa na ukosefu au mgawo wa umeme, kutakuwa na madhara makubwa kwa kuwa umeme unatumika viwandani, hospitalini, barabarani na majumbani kwa matumizi ya majokofu ya kupoozea vinywaji, vyakula ili visioze, mwangaza, kupiga pasi, kusaga unga, kukata nyama na shughuli nyinginezo..

  Mgawo wa umeme unatabiriwa na Mh. J. Makamba katika mtandao wa www.twitter.com alimwandikia Michael Dalali hivi "JMakamba @MichaelDalali Mwaka 2011,
  nilisema
  kwamba suluhu
  ya umeme
  haiwezi
  kufikiwa kabla ya 2013. Kauli
  yangu inabaki
  pale pale.
  Mgawo wa umeme 2012 & 2013"

  Kauli hii ya mwana CCM inatuambia Wananchi tujiandae kuka giza, kutokutazama Tv, kutokupiga pasi, kutokutengeneza juisi za matunda, kukosa maji kwa kuwa mashine za maji haziwezi kusukuma maji bila umeme na hìvyo basi tusinywe maji na tusiende Msalani kwa kuwa hatuna maji, vyakula kuoza kwa kuwa majokofu hayawezi kufanya kazi bila umeme na matatizo mengineyo mengi yatakayosabishwa na mgawo wa umeme.

  Kwa nguvu zangu zote naomba nichukuwe nafasi hii kuwajuza wananchi kuwa CCM wameshindwa kuongoza Taifa letu na ndio maana walishindwa si kuandaa mazingira bali hata nakufua umeme kwa takribani miaka kumi iliyoisha. Na dawa ya ugonjwa huu itapatikana katika msemo 'BIDÍI YETU ITAINGIZA CHADEMA MADARAKANI' ambalo pia ni kundi katika mtandao wa www.facebook.com

  Pamoja tunaweza kujenga Taifa letu kuwa imara na la kutamanika na nchi zingine kama tutajitahidi kuondoa CCM madarakani kwa kutumia nguvu ya kitambulisho cha kupiga kura ifikapo mwaka 2015.
  Nawasilisha
   
 2. M

  Masabaja Senior Member

  #2
  Apr 9, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 139
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kaka hili suala la umeme kwa CCM halina umuhimu wowote hata huyo makamba hana nia ya dhati ya kulitatua hili tatizo ila kujitafutia umaarufu binafsi. Ushauri wangu kwa watanzania ni kuwa toka 2006 alipoingia huyu mkubwa JK wakaanza kulichezea hili jambo mpaka tumefika hapa. Nashauri kama kweli tunahitaji umeme ondoa CCM madarakani period.
   
Loading...