J. Makamba kukatwa na Magufuli 2025 kama Lowassa alivyokatwa na J. Kikwete 2015

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,486
Hakika ndani ya CCM ukionekana una uchu na uraisi, ni lazima ukatwe tu kwa maslahi mapana ya chama.

2025 huenda ikawa zamu ya kijana ninayemwona ana nia ya hali na mali ya kupokea kijiti ambaye ni January Yusuph Makamba.

Kuna dalili akiendelea na spidi hiyo ya kutaka kutimiza ndoto zake, Mwenyekiti wa CCM akakata jina lake kama Jakaya alivyokata lile la Lowasa. Ninyi mnasemaje wenye maono kama mimi?
 
Hakika ndani ya CCM ukionekana una uchu na uraisi, ni lazima ukatwe tu kwa maslahi mapana ya chama. 2025 huenda ikawa zamu ya kijana ninayemwona ana nia ya hali na mali ya kupokea kijiti ambaye ni January Yusuph Makamba. Kuna dalili akiendelea na spidi hiyo ya kutaka kutimiza ndoto zake, Mwenyekiti wa CCM akakata jina lake kama Jakaya alivyokata lile la Lowasa. Ninyi mnasemaje wenye maono kama mimi?
Wafu wakizikana siye tunapita tu
 
Ngosha mwisho wake kuongoza 2020 kama ZZK alivyosema.

Akiendelea na style hii ya uongozi. Kutumbua vipele na kuacha majipu.
 
Ngosha mwisho wake kuongoza 2020 kama ZZK alivyosema.

Akiendelea na style hii ya uongozi. Kutumbua vipele na kuacha majipu.
Ngosha anatoboa bila kizuizi labda Watanzania wahamishwe wote waletwe wengine, na kama Lowasa atakuwa threat kwakwe basi mahakama ya mafisadi itafanya yake then baada ya uchaguzi itamsafisha
 
Ngosha mwisho wake kuongoza 2020 kama ZZK alivyosema.

Akiendelea na style hii ya uongozi. Kutumbua vipele na kuacha majipu.
jipu kuu is loading, ngoja leo tufuatilie habari tutajua. Kama bilioni 15 ni vipele basi tutajie jipu.
 
Akileta pyeee pyeee CCM hawangalii kima usoni.kata pangua kanyaga mbele dadadeki.
 
Hakika ndani ya CCM ukionekana una uchu na uraisi, ni lazima ukatwe tu kwa maslahi mapana ya chama. 2025 huenda ikawa zamu ya kijana ninayemwona ana nia ya hali na mali ya kupokea kijiti ambaye ni January Yusuph
Makamba. Kuna dalili akiendelea na spidi hiyo ya kutaka kutimiza ndoto zake, Mwenyekiti wa CCM akakata jina lake kama Jakaya
alivyokata lile la Lowasa. Ninyi
mnasemaje wenye maono kama mimi?

Lete viashiria kadhaa vya yeye kuwa na uchu wa ukuu wa kaya, na ni kwann awe hivyo kama ni kweli unabashiri vizuri kama ugonjwa kifua kikuu wa joshua wa kijijini kwetu two pipe
 
Wameshasema CCM inaangalia maslahi ya chama na sio mtu binafsi.Alafu sasa JM anaonekana hajishughulishi kabisa yupo tuuuuu.

.
 
Hakika ndani ya CCM ukionekana una uchu na uraisi, ni lazima ukatwe tu kwa maslahi mapana ya chama. 2025 huenda ikawa zamu ya kijana ninayemwona ana nia ya hali na mali ya kupokea kijiti ambaye ni January Yusuph Makamba. Kuna dalili akiendelea na spidi hiyo ya kutaka kutimiza ndoto zake, Mwenyekiti wa CCM akakata jina lake kama Jakaya alivyokata lile la Lowasa. Ninyi mnasemaje wenye maono kama mimi?
omba uzima kwanza 2025 mbali sana Bwa shehe
 
Reli ya Kati wanaanza kujenga linI?
Mradi wa umeme Kinyerezi III utaanza lini kuzalisha umeme?
Mradi wa mwendokasi utaanza lini kuelekea Mbagala na Tegeta? Je Gongomboto hadi Pugu?
 
Mgombea wa CCM 2025 huenda akawa Mwigulu Nchemba au Engineer Yusuph Masauni. January Makamba hatokuwa Rais wa Tanzania na yeye kishalitambua hilo
Japokuwa ni kijana anaefaa kurithi mikoba ya Comrade Kanali Abdul rahman Omar Kinana kuanzia Uenyekiti wa Kampeni za CCM na baadae Ukatibu Mkuu wa CCM
 
hahaha Masauni ndo nani tena? Niwe team Masauni.
 
Kila siku mnahubiri ya ccm , hivi ya chama chenu chagadema huwa mnafuatilia saa ngapi??.
 
hahaha Masauni ndo nani tena? Niwe team Masauni.
Masauni ni Engineer na tunajua ubaguzi wa kitaaluma ulivyotamalaki kwny Awamu hii, Kazi zote Muhimu za Nchi yetu wamepewa Ma Engineer.
Ikitokea ikatumika Utamaduni wa Kubadilishana kidini Masauni ana kidhi kigezo
Ikitokea tukatazama Upande wa Pili wa Muungano nao kupewa fursa basi ana kigezo hicho
Ikitokea kukulia ndani ya chama ni kigezo basi Masauni kishawahi kuwa Chairman wa UV CCM japo majungu yalimtoa
Ikitokea Sifa ni kuwa below 60 wakati unagombea basi sifa hiyo anayo
 
Back
Top Bottom