J.K "Yanayoendelea Dodoma: nayajua, nayafuatiliana natoa uamuzi mgumu punde tu, tulieni watanzania"

dalalitz

JF-Expert Member
Sep 6, 2013
2,750
2,000
J.K bila shaka anafahamu shauku na hamu ya watanzania kutaka kupata japo neno moja kutoka kwake.
Lakini, kwakuwa yeye ni mtendaji zaidi ameamua kuliweka hilo katika maneno machache tu.

[Mwisho wa hotuba yake pale uwanja wa ndege]

Raisi amesema: "Kuhusu yanayoendelea Dodoma sina ninalolijua".


Jiulize tu maswali haya:

1.Hajaulizwa swali lolote na mtu yeyote kwanini aseme hivyo?
-Raisi wa inchi asijue kinachoendelea inchini mwake?- Haiwezekani.

2. Alivyoiendesha hotuba yake.

Aliyoyaongea yote, Hata nusu saa ingetosha kuyaongea na akaondoka zake lakini badala yake alitumia muda mwingi kurudiaridia vitu vilevile na ile ni 'delaying tactic',
anazo hesabu zake na bila shaka ambazo zinaendana na kile kinachoendelea Dodoma.

3. Body language. facial expression&composure

Rais alikuwa ametulia, hana wasiwasi na asie na papara.
Hii inatuambia kuwa kila kitu kiko sawa,
Huwezi kuwa na janga linaloweza kupelekea kulazimika pengine hata kulivunja baraza la mawaziri lako,
Huna ukijuacho halafu ukabaki kuleta hadithi za madaktari wa marekani.

Nimeipenda taarifa yake hii,
Ila nikiri imeniharibia shauku yangu ya kutaka kuona ambacho kingejiri Dodoma. 

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,611
1,250
Unajua alikuwa ICU sasa huko unakuwa huambiwi mambo ya hatari au habari za aina hiyo zinaweza kumsababishia sindikizo la moyo ,kuna kale ka ugonjwa kanachowapata mawaziri wabunge ,siju i wanauita shinikizo mfano wa hivyo ,so naamini alikuwa haambiwi ,unafikiri angeliambiwa wakati yuko kwenye Operation Ondoa Tezi angeponah ?
 

pinno

JF-Expert Member
Jan 17, 2013
1,216
2,000
Huyu jamaa anawajua Watanzania na anajua namna ya kuwatalawa
 

MANI

Platinum Member
Feb 22, 2010
7,289
2,000
Unajua alikuwa ICU sasa huko unakuwa huambiwi mambo ya hatari au habari za aina hiyo zinaweza kumsababishia sindikizo la moyo ,kuna kale ka ugonjwa kanachowapata mawaziri wabunge ,siju i wanauita shinikizo mfano wa hivyo ,so naamini alikuwa haambiwi ,unafikiri angeliambiwa wakati yuko kwenye Operation Ondoa Tezi angeponah ?
Mpwa wangu Elli hebu pita na huku.
 
Last edited by a moderator:

nabiidaniel

JF-Expert Member
Feb 25, 2014
764
1,000
Kichwa cha habari: Yanayoendelea Dodoma nayajua.

Habari yenyewe: Yanayoendelea Dodoma siyajui.

Hivi hapa ndio elimu yetu ilipofikia?
 

Mkomawatu

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
263
250
mimi sishangai hotuba yake kuwa hivyo, alishatumia masaa kadhaa uwanja wa uhuru akizungumzia viatu vya Mandela
 

Maseto

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
894
500
Ni lazima akina Wasira wamemdokeza kabla ya kukubaliana na maazimio yale.Nilisema hapa kwamba hawa CCM wanasubiri msimamo wa JK atakapotua saa tisa
 

Abunuas

JF-Expert Member
Apr 8, 2011
8,726
1,500
nitamshangaa sana huyu jamaa kama hatawafukuza hawa wezi wa hela za umma tena kwa kutumia viroba, magunia na mabox.
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
39,521
2,000
Binafsi niliweka uzi specific kuhusu hiyo kauli ila thread yangu ikaungwanisha ni ile ya Chabruma ambayo ilijaribu kuiboresha kauli ya JK kwa kuiongezea maneno ili kumfichia aibu Kikwete.

Ninachokikumbuka ni kuwa alichomekea mwishoni kabsa mwa hotuba yake kwa kusema na hapa namnukuu "Siongelei ya Dodoma, siyajui vizuri, nikiyajua nitayaongelea".Hii kauli iliniboa sana.
 
Last edited by a moderator:

stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
21,630
2,000
watu wana mihemko, tulizeni bolu bhana, atasema tu , nadhani wengi walitegemea akifika tu airport atangaze so and so, hawapo so and so itakua hivi, sidhani kama nchi inaendeshwa kwa staili ya kuzima moto, inahitaji utulivu na umakini mkubwa kuhandle situations kama hizo.
 

SaidSabke

JF-Expert Member
Sep 28, 2006
2,072
1,500
watu wana mihemko, tulizeni bolu bhana, atasema tu , nadhani wengi walitegemea akifika tu airport atangaze so and so, hawapo so and so itakua hivi, sidhani kama nchi inaendeshwa kwa staili ya kuzima moto, inahitaji utulivu na umakini mkubwa kuhandle situations kama hizo.
Ni kweli ni lazima atulie aelezwe atafute ushauri na apate undani wa suala lenyewe ndipo afanye uamuzi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom