J.K., Laigwenan Lowassa ni mtu muhimu kwako, asikudanganye mtu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

J.K., Laigwenan Lowassa ni mtu muhimu kwako, asikudanganye mtu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Royals, Nov 27, 2011.

 1. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #1
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mtukufu Rais wetu. Mlipopanda ndege mwaka 1995 kwenda Dodoma kurudisha fomu ya wewe kuomba uteuliwe kuwa mgombea urais, mlionekana bado ni vijana. Sababu ilikuwa ni wote wewe pamoja na Laigwenan mlikiwa na nguvu ya ujana na morari mkubwa wa kufanya kazi kwa ajili ya kulijenga taifa letu.

  Bahati nzuri Mungu aliye mwaminifu akawahifadhi nyoye wamili na akahifadhi kiti chako hadi baada ya miaka kumi, ukakipata kiti kile. Na kwa bahati nzuri ukamchagua mwenzako Laigwenan kuwa waziri mkuu. Mtendaji mkuu wa Serikali yako.

  Miaka mitano yako ya kwanza ilikuwa na matumaini makubwa sana kwa watanzania katika kipindi kile ambacho Laigwenan alikuwa mtendaji mkuu wa serikali yako. Nakumbuka mambo mengi yaliyokuwa yanakwenda kwa kasi ya kupaa. Nitaje harakati mlizozianzisha za kila kata kujenga sekondari, harakati za kuzalisha waalimu ili kukidhi ikama ya walimu katika mashule hayo mapya. Nitaje alivokuwa akiwashupalia shingo Wamisri waliokuwa wanaupigia kelele mradi wa kutoa maji ziwa Victoria na kuyaleta Shinyanga na Kahama na mengine mengi ambayo yanajulikana wazi aliyoyafanya kwa ajili ya Serikali yako na yetu.

  Mheshimiwa, potelea mbali kwa yaliyotokea iwe ni kweli au si kweli lakini ukweli unabaki pale pale kwamba Mungu anakufamu vizuri sana wewe binafsi. Anajua yale ambayo unayaweza kama wewe na anajua yale ambayo kwa hakika huyawezi wewe mwenyewe. Laigwenan alikuwa kama Haruni kwako. Kufanya yale ambayo wewe huyawezi na kuyasema yale ambayo huyawezi. Kwa kipindi hicho serikali yako ilikuwa ngunguri kama ilivokuwa serkali ya mtangulizi wako mheshiwa wa Mambo? wananchi wakaitikia kwa sauti kuu yenye afya Poaaaaaaa. Mzee Mkapa.

  Mheshimiwa, ninachojua kila safari na hasa ndefu zina kujikwaa kwingi. Si neno yaliyopita lakini bado kuna kazi kubwa iliyo mbele yako na mbele ya serkali ya chama cha Mapindizi. Kuleta maisha bora kwa kila mtanzania. Nikukumbushe jambo zuri ulilolifanya kwa busara kubwa sana. Ulipoona kasi ya ujenzi wa barabara nchini hauendi kwa kasi ulioitaka ulifanya maamuzi mazuri kama afanyayo kocha mzuri wakati wa mechi. Ukamtoa. Magufuli alikokuwa anachezea na kumpa achezee upande aliouzoea na unaomfaa, mambo yakaenda na yanaenda vizuri.

  Haya yaliyotokea ni mambo ambayo lazima uangetokea, ndivo uongozi wa wengi ulivo. Ni kama ajali iliyotokea kwenye mechi mchezaji mzuri akawa benchi. Hata kama akipa majeraha ya kumlaza muda mrefu namna gani, mchezaji mzuri hujaribiwa kwenye mechi hasa pale timu inapoelemewa. Mimi bado nadhani na ninamwamini Lowasa ni mtu muhimu sana kwako. Fikiri mwenyewe.
   
 2. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #2
  Nov 27, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Too little too late!

  Mngemalizana huko NEC.
   
 3. nzehe

  nzehe Member

  #3
  Nov 27, 2011
  Joined: Dec 6, 2009
  Messages: 94
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  Kwa hiyo nchi nzima hakuna mchapa kazi,ni Lowassa tu?
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Nov 28, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,529
  Trophy Points: 280
  Ni wengi wanamdhania Lowassa kuwa ni Mmasai hivyo kustahili hata hiyo hadhi ya Lwaigwenan. Ukweli Lowassa sio Mmasai na Monduli sio kwao!.

  Muda muafaka ukiwadia, nitawaeleza Lowasa alizaliwa wapi, kwao halisi ni wapi na alifikaje Monduli, alibadilisha vipi kabila toka kabila lake la asili na kugeuka Mmasai na alifanya juhudi gani hadi kuukwaa huo u-Laingwenan!.
   
 5. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #5
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mgomo wa walimu unaofanyika nchi nzima ni ushahidi kuwa unahitaji mtu wa kukusaidia kuongoza nchi. Kwa vile haya yanayotokea sasa hayakuwepo wakati wa Lowasa je, huoni ni vizuri kumrudishia jamaa huyu mikoba yake ili akufae wakati huu mgumu?
   
 6. d

  dguyana JF-Expert Member

  #6
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 426
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tokea mgomo wa walimu uanze sijamsiki JK hewani. Samahan jamani hivi tuna Raisi au?
   
 7. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #7
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ana ziara ya Monduli na Ngorongoro kutoa fidia ya ng'ombe waliokufa mwaka juzi.
   
 8. W

  Wenger JF-Expert Member

  #8
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 448
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 60
  Nadhani ni muhimu kwako wewe mcumia tumbo
   
 9. S

  Starn JF-Expert Member

  #9
  Aug 1, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 400
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Naomba ufute kauli yako ya kumuita raisi mtukufu. ni kipi kilichokufanya mpaka ukamuita mtukufu?
   
 10. m

  markj JF-Expert Member

  #10
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  kwani ye mwalimu? ingekuwa mgomo wa marais duniani ungemsikia!
   
 11. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #11
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  kwani wewe ni mchumia mgongo?
   
 12. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #12
  Aug 1, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hon. Edward N. Lowassa For Presidency 2015.
   
 13. m

  msenda Member

  #13
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  Lowassa rais ajaye
   
 14. Wachovu

  Wachovu JF-Expert Member

  #14
  Aug 1, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 1,197
  Likes Received: 388
  Trophy Points: 180
  Hakuna cha lowassa hapa, huu utawala ndio unaishia. Dola lolote likianza kuanguka viashilia huwa dhairi , migomo kila pahala na mabaraha yanaikumba nchi
   
 15. b

  beyanga Senior Member

  #15
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ​peleka hoja zako ccm hazina mshiko hapa
   
 16. K

  Kakubilo Kasota Senior Member

  #16
  Aug 1, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye bold na red, angalia mkubwa, watakuja wenyewe na kusema, huyu alikuwa anawachukia Waislam ndo maana alipinga ule mkataba wa Wamisri!
   
 17. Young Tanzanian

  Young Tanzanian JF-Expert Member

  #17
  Aug 1, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,740
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  PASCO Ur wrong tunajadili uwezo na tahmini ya lowasa si alizaliwa wap apo ndio waafrka tunapochanganya mambo kwan utendaji na kuzaliwa wapwap na wap jaman elimu itukomboe unaanza propaganda za kna N.N huku JF...Kiukweli tunajua waliommaliza lowasa bni wanamtandao kwa kuhofia threat yake ktk siasa za urais 2105 lakn kama kipokpo tu ni nan aliyeamin kuwa sumaye aliyekuwa PM ataukosa urais...mm naamn moja ya aliyefanikisha ili kwa asilimia 100 ni lowasa yule ni mzee wa mikakati na option B msidhan amelala 2015 mtona mm napta tu
   
 18. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #18
  Aug 1, 2012
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Acha raisi,hata serikali hatuna,it's all rubbish.
   
 19. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #19
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  watu wasubiri 2015 we bado unazugumzia mambo ya zamani
   
 20. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #20
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  sijakuelewa vizuri
   
Loading...