J.K ameridhia CHADEMA Kuchukua nchi kabla ya 2015 kwa udhaifu huu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

J.K ameridhia CHADEMA Kuchukua nchi kabla ya 2015 kwa udhaifu huu...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by simon james, Apr 27, 2012.

 1. s

  simon james JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 283
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa udhaifu huu wa J.k ni dhahiri kuwa CHADEMA imeshaikamata dola kabla ya 2015. Ni dhahiri na mwenye tafakuri hana haja ya kuuliza zaidi kwani waswahili husema mwenye macho haambiwi Tazama. Sina haja ya kurejea matukio mengi yaliyopita ila mambo tunayo ya sadiki hivi sasa yanaonyesha kuwa CHADEMA ndiyo inayo ongoza nchi. Ikumbukwe CC Ya CHADEMA ilipo tangaza kufanya maandamano nchi nzima mapema 2010 baada ya uchaguzi mkuu kushinikiza uandikwaji wa Katiba mpya ndipo J.K akaridhia na kutangaza kuanza mchakato wa katiba mpya. Hata hivyo baada ya mswada wa mabadiliko ya katiba kupitishwa na wabunge wa CCM Nakusainiwa na J.K licha ya mapungufu yaliyofanya CDM Kususia na hatimaye kutangaza kuwa CHADEMA watazunguka nchi nzima ndipo J.K Aliridhia mswada urejee tena Bungeni kwa mara ya kwanza. Hivijuzi baada ya CHADEMA kutangaza kuitisha kamati kuu ya dharura kutoa tamko kali kuhusu ufisadi ulioelezwa na CAG J.K Amekuwa mwoga na kuitisha Cc ya Chama Chake ijumaa kabla ya CC ya CHADEMA Jumamosi tar 28/04/2012 kwakuogopa kimbunga kinachokuja amekubali kusuka baraza la mawaziri.Hongera sana CHADEMA kwa kuuonyesha Uma wawa Tz kuwa sera na hoja zenu zinatekelezeka. Zungukeni sasa vijijini kuweka matawi kwani mnakubalika. Na mshauri J.K asilisuke baraza la mawaziri bali alinyoe kabisa ili nywele ziote upya
   
 2. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Huyo ndiye Rais anayehitajika siyo wale wanaokurupuka. Wasiojua maana ya utawala wa sheria walishang'aka kuwa Rais ameshindwa kuwawajibisha mawaziri wake. Ilikuwa ni lazima baraza libadilishwe na wala siyo habari ya wanasiasa, Rais anafanya kazi kufuata ripori za wataalam na siyo wana siasa. Hongera yake JK kwa kuchukua maamuzi mazito kama hayo kwani inaonesha ni jinsi gani anavyoshikiana kwa kwa karibu na vyombo alivyoviunda kumsaidia kazi
   
 3. v

  vngenge JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 366
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Achanganye na mawaziri toka vyama vya upinzani kwani yy pia huwa anaamini kwamba wote tunajenga nyumba moja hivyo hakuna haja ya kugombea fito
   
 4. Ciphertext

  Ciphertext Senior Member

  #4
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 161
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nguvu ya umma haishindwi kamwe.
   
 5. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Tatizo haliko kwa mawaziri tu, bali hata rubani ni mbovu. Hivyo hata akichanganya kutoka upinzani haitasaidia, jahazi litendelea kwenda mrama kwa kuwa rubani ni bomu tu.
   
 6. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  Huu woga sometimes unamsaidia huyu mtu. Ninaamini jamaa angeliamua kukomaa asingefika 2015. Ila kwa woga huu anaweza kutoboa '15.
  .
   
 7. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #7
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mkuu jaribu kuweka paragraphs habari yako isomeke vizuri.
   
 8. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,463
  Likes Received: 10,672
  Trophy Points: 280
  this is the best option available.kama katiba inaridhia.

  KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
   
 9. s

  simon james JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 283
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekuelewa kamanda
   
 10. m

  manyani Member

  #10
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nionavyo Rubani sio mbovu ila amechoka na ndege hiii na sasa mtizamo wake ni kuona kuwa ndege inabadilishwa kabisa na rubani makini anachukua usukani.... chochote anachochelea kufanya kwa mtizamo wangu ni kwa kufanikisha ndege mpya na rubani mpya anapatikana. ndio maana kila wasio upande wake wakitoa hoja mwishowe rubani huyu hukubaliana nazo.. atakumbukwa kwa kuwa amekuwa daraja ma mabadiliko.
   
 11. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #11
  Apr 27, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  NAKUKUBALI pia si lazima atishiwe na Upinzani kwani kuna kipindi NCCR kilitingisha Nchi na majimbo yote ya Dar yakachukuliwa na wapinzani lakini si kwamba ndio serikali iliyokuwa madarakani ilichanganya na Wabunge wa Upinzani katika Baraza la Mawaziri
  Chama chochote kikipata ridhaa ya kuongoza hakitakosa misukosuko km hii ndio kusema kila saa Bunge litakuwa likimshinikiza Rais akubaliane na matakwa yake (fukuza Jairo, fukuza Lumbanga, fukuza Mponda, fukuza Nkya, fukuza Ngeleja, Pinda, Mkulo mwishowe na Kikwete sasa niutawala gani huo
  Tuheshimu Mihimili iliyoko (Serikali, Bunge na Mahakama) kwani haiingiliani ndio maana kuna Uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge / ambapo mwenye Mamlaka ya kulivunja Bunge ni Rais pekee na wakarudi majimboni kuomba kura upya
  Bunge litatunga Sheria na kuifuatilia Serikali kiutendaji km itatetereka
  Mahakama yenyewe itatoa Hukumu kwa wabunge wote katika makosa yote isipokuwa kwa Rais km atashtakiwa kwa makosa ya jinai
  Du kwaherini maana naona kila siku kampeni hadi kieleweke je/ kisipoeleweka na 2015 imefika tujifiche wapi?
   
 12. Alonick Antony

  Alonick Antony Member

  #12
  Apr 27, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera chadema!
   
 13. s

  simon james JF-Expert Member

  #13
  Apr 28, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 283
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwendo mdundo CDM
   
 14. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #14
  Apr 28, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Ilivyo ni kwamba:

  CCM ni Chama inayotawala na
  CHADEMA ni Chama inayoongoza Tanzania.
   
 15. s

  simon james JF-Expert Member

  #15
  Apr 28, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 283
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabsa
   
 16. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #16
  Apr 28, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  vinega bwana hamuishi vituko,yani muikamate dola kwa wabunge 48 tu mlionao bungeni...!
   
 17. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #17
  Apr 28, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,381
  Likes Received: 22,253
  Trophy Points: 280
  Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake

  Chadema tumenyenyekea sana kwa wananchi sasa tunakwezwa.
   
 18. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #18
  Apr 28, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwani riport ngapi za kitaalamu zimeandikwa na hakufuata? na hili la kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu ndo imewavuruga kabisa na wala si za ripoti za kitaalamu. Huyo CAG kila mwaka anawapelekea riport na wala hawachukui hatua zozote? Ripoti ziko nyingi za kitaalamu na wala hazifuati ila hii ya sasa kwa vile wapinzani wamelivzalia njuga hana jinsi. Wewe ni mnafiki tu na unamaana ni wale wanaojikomba ili wapate vyeo. Hongereni CDM kwa kazi nzuri mnayofanya mpaka hawa jamaa wa CCM wanachanganyikiwa sasa. Cha kushangaza utaona kaingiza tena vilaza kama kawaida yake. Miaka yote yeye kazi yake ni kuunda baraza tu, makatibu wa wizara ni walewale unategemea patakuwa na mabadiliko gani hapo?
   
 19. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #19
  Apr 28, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  nimewahi kusoma kitabu kimoja kinaitwa 'The Power of an Example' na kinaeleza jinsi wengi tunavyoshindwa kuelewa kwa sababu ya kutokuwa na mifano ya hali halisi iliyopo.

  Leo katika 'pitapita' nimeona haka kapicha ambako kanaweza kuelezea what is so called 'NGUVU YA UMMA", ipo na inaishi.
  Na jinsi kamati kuu ya ccm walivyotoa tamko wanasahau kuwa wao ni kama udongo tu lakini mbegu ziko chini na zitaota tu, watake wasitake!
  nguvu ya umma.jpg .
   
 20. s

  simon james JF-Expert Member

  #20
  Apr 28, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 283
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli Mungu anatulipa fadhila
   
Loading...