Iyumbu, Dodoma: Rais Magufuli aagiza ardhi iliyotengwa na Serikali ili kuzika Viongozi kurudishwa kwa wananchi. Asema yeye atazikwa Chato

likandambwasada

JF-Expert Member
May 27, 2015
5,402
6,072
Baada ya Mh. Rais kuzindua tawi la benki ya CRDB la LAPF Dom, sasa TBC1 wako live katika sherehe za uzinduzi wa mradi wa nyumba za makazi wa Iyumbu, Dodoma.

Anazindua nyumba 150 za mradi wa Shirika la nyumba la Taifa (NHC) zilizopo Iyumbu, kata ya Iyumbu Mkoani Dodoma.


==========================================

UPDATES

=> Tumeshahamia Dodoma na kama kuna mtu anafikiri tunatania ajue hilo,Tarehe 15 Makamu wa Rais anahamia hapa,mimi mwakani nahamia hapa,Dodoma ndio makao makuu lazima tuhamie.

=> Ninafahamu NHC kuna mgogoro, wapo watu wanaotaka ukurugenzi, wanawatumia mpaka wajumbe wa Bodi, wapo wanaotumiwa na wasiasa,nazungumza ukweli ili tulimalize tatizo, kaeni mtathmini wapi kuna tatizo.

=> Serikali yoyote iliyopo madarakani kazi yake ni kutengeneza ajira, nanyi mmeweza kutengeneza ajira hizo.

=> Jengeni nyumba kila mahali,lakini angalieni matumizi yenu ya pesa, ninafahamu cost ya nyumba, mimi nimekaa kwenye ujenzi.

=> Sheria Namba 1 ya mwaka 2006 ilipitisha Dodoma kuwa eneo la kuzikiwa viongozi, mimi nikifa nizikwe kwetu Chato alikozikwa baba yangu, hii ardhi ya makaburi tutawarudishia wananchi wenyewe.

=> Tulipitisha sheria kutenga eneo Dodoma la kuzikia viongozi, Mimi nikifa nitazikwa kwetu Chato, nina uhakika hakuna kiongozi atakayetaka kuzikwa hapa, watataka kuzikwa kwao, ile sheria tuliipitisha nikiwa bado sijawa Rais.

Pia Rais Magufuli atangaza Eka 129 za ardhi iliyopo Iyumbu, Dodoma ambazo Serilkali ilikusudia zitumike kwa ajili ya kuzika viongozi zimerudishwa kwa wananchi,

MAGUFULI: Mimi nimeshasema nikifa mimi, nazikwa nyumbani kule alikozikwa baba, Chato. Wakati napitishwa sikujua kama nitakuwa Rais, nilikuwa nasema wale, hao marais wakifa tutawazika huko Dodoma, sasa nimeingia mule nikashangaa, na mimi niende nikazikwe kwa wagogo?

Yaani nije nizikwe kabisa hapa kwa wagogo halafu waanze kuchezea hapo na fisi zao! Lakini nikajaribu kuuliza na wengine, marais wastaafu sitaki kuwataja majina, nakasema wewe ukifa tutakupeleka Dodoma? Akasema hapana, mimi nataka nikifa nikazikwe mahali fulani alikozaliwa, kwa hiyo nikajua hii, hakuna mtu atakaetaka kuzikwa hapa, labda Malecela na mheshimiwa spika hapa kama atataka lakini nina uhakika na yeye atataka azikwe Mvumi na mwingine Kongwa.

Sasa mtabaki hapa mtazika nani na wakati ardhi mmeikatalia, nimeshatoa maagizo hiyo sheria tuibadilishe, wakati tunasubiri hiyo sheria tuibadilishe, natamka hapa, hii ardhi tunawarudishia wananchi wenyewe. Maamuzi mengine huwa ni ya ajabu.


 
Habari wakuu,

Baada ya mh. Rais kuzindua tawi la benki ya CRDB la LAPF Dom, sasa TBC1 wako live katika sherehe za uzinduzi wa mradi wa nyumba za makazi wa Iyumbu, Dodoma. Nyumba hizi zimejengwa na NHC na zinatarajiwa kuzinduliwa na mh Rais John Pombe Magufuli hivi punde.

Stay tuned
[HASHTAG]#hapakazitu[/HASHTAG]
WEKA NA TUPICHA MKUU-MAMBO YATANOGA
 
Habari wakuu,

Baada ya mh. Rais kuzindua tawi la benki ya CRDB la LAPF Dom, sasa TBC1 wako live katika sherehe za uzinduzi wa mradi wa nyumba za makazi wa Iyumbu, Dodoma. Nyumba hizi zimejengwa na NHC na zinatarajiwa kuzinduliwa na mh Rais John Pombe Magufuli hivi punde.

Stay tuned
[HASHTAG]#hapakazitu[/HASHTAG]
Hiyo TBC Hawana vipindi vingine vyenye tija kwa taifa?
 
Nimemshangaa Mrisho Mpoto anasifia hadi anapitiliza na anaweka na uongo tupo Iyumbu hapa anaimba anasema kwa uzalendo wa MH SANA anajenga flyover kutoka DAR hadi MWANZA aisee huu unafiki wa watanzania ni wakiwango cha 100G maana kwa kujua watu wanapenda sifa basi wanasifia hadi uongo.
Ukweli utakuweka huru wakati wote.
 
Nimemshangaa huyu jamaa anasifia hadi anapitiliza na anaweka na uongo tupo iyumbu hapa anaimba anasema kwa uzalendo wa MH SANA anajenga flyover kutoka DAR hadi MWANZA aisee huu unafiki wa watanzania ni wakiwango cha 100G maana kwa kujua watu wanapenda sifa basi wanasifia hadi uongo.
Ukweli utakuweka huru wakati wote.
Anajikomba ......eti na yeye ni mzalendo ......:p
 
Naye apumzike bwana so kila kamradi unaenda kuzindua wakati mawaziri wapo..
Uje unizindulie na choo changu cha kulipia hapa kitaa..
Naunga mkono Rais kuzinduwa nyumba hizi.

Lakini azikaguwe na awaulize bei za hizo nyumba ninaamini atazimia.

Tunamsubiri azinduwe na zile za Pspf kule Buyuni Chanika, ule ni wizi na ujambazi wanafanyiwa Watanzania, nyumba ya millioni 20 Mtanzania anakamuliwa millioni 80, na ukikopa riba inafika millioni 200.

Mheshimiwa Rais ukiweza kuwashughulikia hawa wahuni na mimi niandalie kadi ya kujiunga na ccm ya Magufuli.
 
Back
Top Bottom