Iwepo tume ya kuratibu ada za shule binafsi. Kuna shule kila mwaka ada wanapandisha asilimia kubwa na hakuna mabadiliko shuleni

ommytk

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
482
1,053
Wadau Mimi nashauri Serikali iangalie kuunda tume ya pamoja na shule za binafsi kuhusu suala la ada. Kuna shule zinapandisha ada kila kukicha yaani kila mwaka aisee na kwa kiwango kikubwa bila sababu.

Unajua ada inapanda labda kuna mazingira shule au walimu watabadilika hakuna inabaki pale pale hii serikali inabidi kumulika kwa jicho angavu
 
Hizi shule nyingi ni biashara, zinaendeshwa kwa malipo ya Ada, bila ada, hakuna mishahara. Hakuna haja ya tume, wizara ipo, tatizo watendaji wamelala, miongozo haifwatwi.

Unalipa millioni 2,mtoto anapewa andazi moja na chai ya rangi Kama breakfast!
 
Unajikuta una pakulalamika basi unaumia tu kimya kimya
Hizi shule nyingi ni biashara,zinaendeshwa kwa malipo ya Ada,bila ada,hakuna mishahara,
Hakuna haja ya tume,wizara ipo,tatizo watendaji wamelala,miongozo haifwatwi.
Unalipa millioni 2,mtoto anapewa andazi moja na chai ya rangi Kama breakfast!
 
Shule wazipe grade tu yaani kuna shule class a hizo ada ni kuanzia kiasi kadhaa mpk kadhaa na kuna class b yaani mpk class f uko.
 
Wadau Mimi nashauri Serikali iangalie kuunda tume ya pamoja na shule za binafsi kuhusu suala la ada. Kuna shule zinapandisha ada kila kukicha yaani kila mwaka aisee na kwa kiwango kikubwa bila sababu.

Unajua ada inapanda labda kuna mazingira shule au walimu watabadilika hakuna inabaki pale pale hii serikali inabidi kumulika kwa jicho angavu
January fever inatusumbua wengi sana.

Bora Magu anavyopambana kuboresha public schools tuachane na hizi zinazotupa wazimu
 
Wadau Mimi nashauri Serikali iangalie kuunda tume ya pamoja na shule za binafsi kuhusu suala la ada. Kuna shule zinapandisha ada kila kukicha yaani kila mwaka aisee na kwa kiwango kikubwa bila sababu.

Unajua ada inapanda labda kuna mazingira shule au walimu watabadilika hakuna inabaki pale pale hii serikali inabidi kumulika kwa jicho angavu
Shule za umma zipo na mtoto wako kapangiwa shule ya umma kwanini unang'ang'ania ya binafsi? Shule binafsi kuna ADA na GHARAMA za matumizi ya mwanao. Shule nyingi toka Magufuli ameingia madarakani hajapandisha ADA. Kinachopanda na GHARAMA za matumizi ya mtoto, mfano Godoro, ndoo, jembe, kijiko, sahani, uniform. Wewe umeambiwa mtoto aende na ndoo (ambazo nyumbani unazo) au atapatiwa shuleni; unaamua asibebe mzigo anakwenda kulipishwa TZS 5,000 na ndoo umeacha nyumbani.
 
Umeongea kwa hasira sana. Ila binafsi naona ungenyamaza ili wenye watoto wao huko waseme.
 
Hata mimi nina watoto shule binafsi. Mmoja wa Form I nimempeleka jana wawili wa Form III na Form V wanaondoka Jumamosi. Hakuna ada iliyopandishwa toka Magufuli aingie madarakani kwa shule wanakosoma watoto wangu. Kinachoongezeka kwenye malipo ni mahitaji mbalimbali ya mtoto ambayo hata kama mzazi angenunua peke yake huenda bei ingekuwa juu. Kuna shule mmoja nimempeleka mtoto wa marehemu kaka yangu Blancket tulilokuwa nalo lilikataliwa na badala yake tukauzia lingine pale shule kwa TZS 15,000 ambayo ni bei nafuu kuliko tunavyouziwa huku mijini.
 
Kwa kuponda shule za serikali hamjambo.

Acheni kulia lia nyie matajiri, lipeni ada.

Nashauri wamiliki wa shule waongeze laki 2 kila muhula
 
Back
Top Bottom