Iweje mkullo asifie mandhari na hadhi ukumbi bot - twin towers za mseminari liyumba!!

FDR.Jr

JF-Expert Member
Jun 17, 2008
1,359
353
leo nimetumia muda mwingi kusikiliza na kuangalia forum ya imf na africa ktk econimic crisis ya dunia.

Nimeshangazwa sana mkuu wangu mkulo ku high light kuwa africa inasonga mbele na kuipa dunia mfano ni sehemu forum inapofanyika!!!

Mkuu wa imf naye akafagalia sana hilo.

Ninatafakari sana nchi kujifagilia product iliyozaliwa na mradi ambao pccb wanatuambia mseminari na wenzake wamemega salio kiaina, nchi iko mahakamani ikinung'unika dhidi ya liyumba!!!!!

Tutajidili mantiki ya mh. Mkulo, karibuni
 
Sitaingia kwa mengine, lakini kama alikuwa anajisifu kuwepo ukumbi mzuri waliotumia, na huo ukumi ndio tulipigwa changa la macho kwa kuibiwa hakuna kosa. Kuibiwa tulishaibiwa, lakini bado ukumbi ulijengwa kwa fedha zetu walipa kodi. Hivyo lazima tutambe nao kwa kuwa ni wetu, japo tuliibiwa.
 
leo nimetumia muda mwingi kusikiliza na kuangalia forum ya imf na africa ktk econimic crisis ya dunia.

Nimeshangazwa sana mkuu wangu mkulo ku high light kuwa africa inasonga mbele na kuipa dunia mfano ni sehemu forum inapofanyika!!!

Mkuu wa imf naye akafagalia sana hilo.

Ninatafakari sana nchi kujifagilia product iliyozaliwa na mradi ambao pccb wanatuambia mseminari na wenzake wamemega salio kiaina, nchi iko mahakamani ikinung'unika dhidi ya liyumba!!!!!

Tutajidili mantiki ya mh. Mkulo, karibuni

Naona mada yako haijakaa vyema. Ulichotaka kijadiliwe hujakiweka wazi, kwani maneno ya mkulo kuwa kasifia mandhari ya ukumbi inaonekana tu kwenye kichwa cha habari. Lakini pia kama ukumbi ni mzuri sioni sababu ya kuusema ni mbaya kwa kuwa mafisadi waliiba kupitia huo mradi. Ni mfano binti akibakwa na akamzaa binti mzuri, ukatae kuwa sio mzuri kwa kuwa tu ni tokeo la ubakaji.

Halafu pia suala la mseminari hapa sijui linakuja je, kwani mie nikimuelezea Mustafa kama "Mmadrasa" nitakuwa nimeleta vionjo vingine ambavyo vitafanya mada ipoteze mwelekeo. Nadhani taasisi mtu aliyosomea au anayoamini katika misingi ya imani yake usiwe msingi wa hoja!
 
Mkuu Nono Binafsi napenda sana kutumia wasifu wa awali mtu yeyote ambaye nimebahatika kumfahamu, hivyo kwangu Liyumba atadumu kuwa Mseminari na zaidi msingi wa hoja haufungamani na imani za watu lakini tafsiri na tafakuri ni uwanja huru kwa kila mwana jf kujifungua kimawazo. Ndiyo maana nimekushukuru kwanza na nimeona haja kukupa fursa kutafakari hoja yangu kwa kila kona itakayofaa isipokuwa utangulizi huu wa sasa. twende kazini mkuu
 
Ukumbi mzuri ndio lakini hata kama wageni watausifia tujue tu kuwa huko pembeni wanatucheka kuwa priorities zetu haziko sahihi!! Utatumiaje mabilioni ya shilingi kujenga hizo towers wakati wanao hawana madawati wala vitabu mashuleni; watoto wanasoma madarasa ya mbavu za mbwa; secondari za YEBO YEBO hazina walimu na juu ya yote serikali hiyo hiyo inashindwa kuwafadhili wanafunzi wetu kwenye vyuo vyetu vikuu?
 
Last edited:
Back
Top Bottom