Iwapo Watanzania wataamua 2025 twende na Mwanamke, mnaonaje tukiwashauri CHADEMA wasimamishe Mwanamke? Maana Mwanaume kushindwa na Mwanamke ni aibu!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,578
Wanabodi,

Nimekutana bandiko hili humu JF Mnyukano Chadema ,mbunge Aida amkataa Lisu
Gazeti la jamhuri la leo limekuja na taarifa inayoelezea majibizano ya Tundu Lisu na mbunge wa Nkasi kupitia Chadema mh Aida khenani, Tundu Lisu amenukuliwa akisema kuwa chadema haiutambui ubunge wa Aida Khenani licha ya kuwa alichaguliwa kwa kura za kishindo na wananchi wa Nkasi kaskazini.
Mh Khenani amemtaka Lisu kutulia na kuendelea kulelewa Ubelgiji kwani hana uwezo wa kusema hatambui ubunge wa mtu fulani kwani hana maamuzi ya mwisho ndani ya chama.View attachment 2576465
Ushauri wa bure Chadema, iwapo Watanzania kwa kauli moja wataamua 2025 twende na Mwanamke kama nilivyo shauri hapa, Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!

Mnaonaje kama tukiwashauri Chadema, kwenye urais asimamishwe Mhe. Aida Khenani ambaye ndie mbunge pekee wa Chadema aliyepata ridhaa ya Watanzania, na leo ndio kwa mara yangu ya kwanza kumsikia akichangia Bungeni, hili ni jembe la ukweli!, anajua kujenga hoja na anachangia very independently sio kichawa chawa!, kwasababu hajaingia Bungeni, kwa hisani ya mtu yoyote!.

Leo wakati wabunge wengi wakichangia kichawa chawa kumpongeza Rais Samia kuresha demokrasia na mikutano ya hadhara mbunge huyu aliuliza ni nani na wa chama gani aliyefifisha demokrasia?.
(kuhusu kuruhusu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, hata mimi nilipongeza na kusema lazima kuhoji!. Anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga. Kuzuiwa bila kifungu, kuruhusu bila Kifungu. Ni hisani ya Rais Samia. Haki kuhisaniwa hadi lini? )

Maadam sasa tayari Makamo Mwenyekiti wa Chadema ameisha anza kukwaruzana na jembe hili, then Chadema isimamishe mgombea Mwanamke mwingine yeyote, maana wakimsimamisha mgombea mwanaume, atapata aibu sana, kwasababu Kiafrika mwanaume kushindwa na Mwanamke ni aibu sana!.

Iwapo Watanzania Wataamua 2025 Twende na Mwanamke, hii maana yake ni Watanzania wanakwenda kuchagua rais Mwanamke, hivyo vyama vyote vyenye akili timamu, vitasimamisha wagombea wanawake washindane, wanawake kwa wanawake, Mwanamke akimshinda Mwanamke mwenzake imekaa vizuri na Mwanamke akishindwa na Mwanamke kwenye siasa, iko poa, sio aibu!.
Mnaonaje tukiwashauri Chadema uchaguzi wa 2025 nao waende na mgombea mwanamke?.

Hivyo kuelekea 2025, iwapo sauti hii Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke sio ya kweli, then mnaonaje kama tukiwashauri Chadema nao wasimamishe mgombea mwanamke?.

Angalizo
Sisi binadamu ni kama wanyama, kuna wanyama wakati na wanyama wapole, wanyama wala nyama ni wanyama wakali na hawaliwi, wanyama wala majani ni wanyama wapole na wanaliwa.

Vivyo hivyo kwa makabila yetu yako makabila wakali na makabila wapole. Makabila ya wakulima ni wala mazao ni wapole na makabila ya wafugaji ni wala nyama ni wakali.

Na kwenye mifumo ya utawala, kuna makabila ya patriach system au patrilinea na matriarch system au matrilinier. Makabila ya wafugaji ni dominant tribes, kwao mwanaume ndio kila kitu, kwa makabila haya kushindwa na Mwanamke ni aibu ya mwaka! Kwa makabila matrilinier ni makabila ya wakulima, kwao Mwanamke ndio kila kitu hivyo kwao kwa mwanaume kushindwa na Mwanamke ni poa tuu sio aibu.

Kufuatia mimi ni kutokea dominant tribe la Wasukuma, naomba bandiko hili lisije kupata negative connotation kuwa mimi ni Sukuma Gang!, hatuwaamini wanawake, hatuwathamini wanawake, naomba kuwaambia, wengi wamemjua Samia baada ya kuukwaa urais wa JMT, angalieni watu tulianza lini na Samia New Cabinet: Baadhi ya Majina ni Haya Hapa!

Na kuhusu kuzungumzia rais Mwanamke Siku ya Wanawake Duniani: Je, tuna Wanawake wenye sifa za Presidential Material?

Hata Samia kuwa rais, angalia ni kina nani walimtabiria Pascal Mayalla alitabiri mwaka 2017 kuwa Samia atakuwa Rais wa JMT baada ya 2020 na nikashauri Baada ya Marais 5 Wanaumez, Samia ndiye Kifungua Mimba 'cha Rais Mwanamke!. Mnaonaje Akifuatiwa na Marais Wanawake 5 Ndipo Aje Tena Rais Mwanaume?.

Nisije kunyooshewa kidole kuhusu uwezo wa wanawake, nimeusema wazi Je, kuna kazi za kike na za kiume? Fupa hili lililowashinda wanaume wanne, mwanamke mmoja ataliweza?

Nimezungumzia akili za wanawake Wanawake Wana Akili Kuliko Wanaume? Hata kwenye Siasa na Uongozi, Wanawake Wameonyesha Uwezo Kuliko Wanaume

Nimezungumzia uwezo wa wanawake Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani: Je Wajua Kuna Wanawake Wana Uwezo Mkubwa Kuliko Wanaume ila Wamekuwa Wanabaniwa!. Hata Huyo Kuonyesha Uwezo na ...

Paskali
 
.
20230329_225233.jpg
 
Back
Top Bottom