iwapo watachukua nchi...... CHADEMA kuendesha nchi kwa maombi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

iwapo watachukua nchi...... CHADEMA kuendesha nchi kwa maombi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by in and out, Jul 10, 2011.

 1. i

  in and out Member

  #1
  Jul 10, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  chama cha democrasia na maendeleo (chadema)kimesema, endapo kitapewa ridhaa na wanainchi ya kuunda serikali ktk uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, kitahakikisha kinaanzisha utaratibu wa kufanya maombi maalum kwa taifa ili mungu aweze kufanikisha ndoto ya watanzania ya kuwa na maisha bora. Ahadi hiyo ilitolewa jumapili iliyopita na mwenyekiti wa CHADEMA mheshimiwa Freeman mbowe, alipokuwa mgeni rasmi katika hafla maalum ya uzinduzi wa kitabu cha kuhamasisha maendeleo ya watanzania kilicho andikwa na mtume john nengala Lobulu. katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye kanisa la Maranatha Christian Center lililopo kinondoni, jijini Dar es salam na kuhudhuriwa na watu wa kada mbalimbali , mbowe ambaye ni mbunge wa hai, mkoani kilimanjaro na kiongozi wa upinzani bungeni, alisema maombi ni muhimu kwa ustawi wa taifa, hivyo yanapaswa kupewa uzito na kuwa sehemu ya utamaduni wa watanzania. "kutokana na umuhimu wake ndio maana tumeahidi kwamba tukifanikiwa kupata ridhaa ya kuongoza nchi hii kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 tutaanzisha utaratibu maalumu wa kuliombea taifa, katika maombezi hayo kila mmoja kwa imani yake aliombee taifa ili mungu aweze kufanikisha malengo yetu, maombi ni jambo muhimu sana kwa taifa lazima yapewe kipaumbele," alisema. Awali, kabla ya kuzindua kitabu hicho kiitwacho Vikwazo vya mafanikio yako na jinsi ya kuvishinda. Mbowe alitoa wito kwa watumishi wa mungu pamoja na viongozi wa serikali kutofanya kazi kwa maslahi binafsi, badala yake watumike kwa kutengeneza mazingira yatakayonufaisha kizazi kijacho badala ya kuendelea na hali ya sasa ambapo wanaonekana kufanya kazi kibinafsi zaidi. Hata hivyo, alisema ili hali hiyo iweze kufanikiwa kuna haja kwa watanzania bila kujali tofauti zao za kiimani kujikita zaidi katika maombi ili taifa liwe na viongozi wenye hofu ya mungu ambao watafanya kazi kwa maslahi ya taifa na kizazi kijacho kwani bila hofu ya mungu kutawala miongoni mwa viongozi ni vigumu kuwajibika kwa wanainchi bali wataendelea kujali maslahi yao binafsi na kuwaacha wanainchi wakiendelea kuteseka.
   
 2. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #2
  Jul 10, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Naanza kupata wasiwasi mkubwa hivi CDM wana mahusiano gani na ili Kanisa, Maranatha Christian Center, na huyu Mtume John Nengala Lobulu, ni nani CDM
   
 3. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #3
  Jul 10, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,002
  Likes Received: 584
  Trophy Points: 280
  aisee wee jamaa kweli ni mdini, umeanzisha thread yako halafu unajijibu ili uwavutie watu? acha kujiongezea mzigo wa dhambi kwa kueneza chuki ya udini, yaani wewe hata shetani atakukataa, sasa sijui utakuwa mgeni wa nani?
   
 4. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #4
  Jul 10, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  wasiwasi wa nini?mbona hata wimbo wa taifa unamtaja mungu!tatizo siku hizi hata graduates hawajui wimbo wa taifa.serikali huitisha maombi pindi mvua zigomapo kunyesha tuu,ndio maana nchi haipati maendeleo!
   
 5. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #5
  Jul 10, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Acha kuangaika! udini wangu na hizo chuki unazozisema zikuwapi? mimi ID yangu moja inanitosha sina haja na ID ingine, wewe changia hii thread kama huna cha kuchangia kaa pembeni members wengine watachangia
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  Jul 10, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  kwani waislam hamfanyi maombi? ile DUA ni nini mkiambiwa maombi akili yeeenu yooote inahamia kwa ukristu tu. mbina kwenye sherehe kunakuwa na maombi na dua au kwenye misiba utakuta sheikh na mchungaji wanaomba pale au ile dua si MAOMBI? wenzetu waislam hebu kaeni chini mtafakari mnakoelekea si kuzuri sisi km ndugu zenu tunawatakia mema
   
 7. O

  Omr JF-Expert Member

  #7
  Jul 10, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sasa yanini wote tuombe wakati anafahamiana na huyo mtume, si bora huyo mtume afikishe maombi yetu huko juu. Kwani nchi zilizoendelea ziliombewa na nani ? Acheni upumbavu ndugu zangu, maendeleo yetu hayawezi letwa na dua za mashehe wala mapadri. Nchi itajengwa kwa bidii zetu wenyewe na jinsi tunavyo endekeza siasa ndio tunazidi kurudi nyuma.
   
 8. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #8
  Jul 10, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Fanya ufanyalo bila Mungu ni kujilisha upepo!Fatilia historia ya marekani ndipo utajua Mungu anahitajika au shetani!
   
 9. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #9
  Jul 10, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Uwezi kujenga viwanda, uchumi, miondombinu kwa maombi, nchi zilizoendelea mbona atujasikia kuwa Uchumi wa China umekuwa kwa kufanya maombi
   
 10. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #10
  Jul 10, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  nahisi hapo ulipo umejifunga mabomu usijejilipua mtandaoni buree tukaikosa jf maana naona mbishi km umechanjia vile hahaaaa
   
 11. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #11
  Jul 10, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,672
  Trophy Points: 280
  Tatizo Pro-CDM-JF, wengi wenu hamtaki challenge kutoka upande wowote nyie uwa mnakubaliana kila jambo mnakosea, ushauri wangu kwako wewe na Pro-CDM-JF, lazima mkubali kuwa Breadth ili mkomae kisiasa
   
 12. Echolima

  Echolima JF-Expert Member

  #12
  Jul 10, 2011
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 3,169
  Likes Received: 531
  Trophy Points: 280
  Mtoa mada yuko Mdini zaidi ndiyo maana Roho ya Udini inamtafuna hata kukerwa na kauli ya Mh.Mbowe lakini kwa ujumla alisema kila mtu kwa Imani yake aombee Taifa tatizo liko wapi????au yawezekana ametumwa na chama cha MAGAMBA(CCM)
   
 13. J

  John Marwa JF-Expert Member

  #13
  Jul 10, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu huwa hasikilizi maombi ya Wenye dhambi! Ikumbukwe Chadema watamsimamisha Dr Slaa agombee tena Urais,na Dr Slaa hana Mke ni Mzinzi! Kama kweli CDM ina amini maombi basi isisimamishe wagombea wazinzi!
   
 14. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #14
  Jul 10, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hapo penye red panahitaji sahihisho:
  Mungu alimtuma mwanae kuwatafuta mwenye dhambi. Na alipokuja baadhi ya wanadamu waliojifanya hawana dhambi, mafarisayo nk walimshutumu pale alipokuwa akila na kushirikiana na wenye dhambi. Jibu lake lilikuwa rahisi "asiye mgonjwa haitaji daktari". Maombi kwa watu wasio na dhambi hayana maana ni sawa na mtu asiye mgonjwa kwenda kwa daktari. Acha wenye dhambi na mapungufu ya kimaisha wamwombe Mungu, nyie msio na dhambi na mnajitosheleza kimaisha ombeni kama yule farisayo aliyeomba kwa kumshukuru Mungu kwa kutomfanya mdhambi kama yule mtoza ushuru. "God have mercy on me a sinner"
   
 15. katabu

  katabu JF-Expert Member

  #15
  Jul 10, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kama yatakuwa maombi haya ya kawaida tu, bila ya kupitia kwa yule aliyepewa jina lipitalo majina yote (YESU) ni kujilisha upepo. Bora maendeleo yaletwayo kwa bidii za kibinadamu tu. Kama China na nchi nyingine ambazo hata mlemavu wanaweza kumfanya mungu wao.
   
 16. S

  Sharo hiphop JF-Expert Member

  #16
  Jul 10, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 662
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  imeandikwa, Heri mtu yule asiyekwenda katika shauri la wasio haki wala hakusimama kwenye njia ya wakosaji, zab 1:1. Safi Mbowe! Usikubali kusimama na hao wenye Magamba.
   
 17. T

  TEGEMEA JF-Expert Member

  #17
  Jul 10, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu ni muweza wa yote.Hata marekani kwenye noti zao wanasema "IN GOD WE TRUST"
   
 18. T

  TEGEMEA JF-Expert Member

  #18
  Jul 10, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani,acheni MUNGU AITWE MUNGU.Hata marekani wanalijua hilo nandio maana kwenye noti zao wakaandika"IN GOD WE TRUST"
   
 19. T

  TEGEMEA JF-Expert Member

  #19
  Jul 10, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  St ivuga upoo???!
   
 20. Asante

  Asante JF-Expert Member

  #20
  Jul 10, 2011
  Joined: Dec 18, 2009
  Messages: 1,960
  Likes Received: 297
  Trophy Points: 180
  Maombi kwa Mwenyenzi Mungu au maombi kwa shetani
   
Loading...