Iwapo CHADEMA itachukua dola, CCM mko tayari kuvaa viatu vya CHADEMA?

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
25,426
18,228
Nawauliza CCM iwapo CHADEMA ikishinda uchaguzi mko tayari kuvaa viatu vya CHADEMA?

1. Kuzuiwa kufanya mikutano ya hadhara na ndani miaka 5
2. Vyombo vyenu vyote vya habari vifungiwe na TBC isifu tu juhudi za Lissu na CHADEMA
3. Wanaharakati wenu bungeni na nje ya bunge waandamwe na watu wasiojulikana halafu uchunguzi usifanyike
4. Mkijaribu kufanya mikutano lazima mkutane na bomu ya machozi
5. Tume ya uchaguzi na msajili wa vyama kuwatishia
6. Viongozi wenu wakubwa wa CCM mali zao zitaifishwe au accounts zao zifungiwe hata kama ni mali halali
7. Viongozi wenu wa CCM wawekwe mahabusu halafu mkaombe hela za michango kwa ajili ya dhamana

Mtaweza kufanya yote hayo?
 
Ni upunguani kufananisha chama cha Mbowe na CCM.Chama cha vibaraka wa mabeberu ni cha kuogopwa kama ukoma. Chama saccos, mtaishia kuona ikulu kwenye TV tu pale Ufipa mkiwa na faru John wenu mkononi. Ni kipigo cha kutosha hiyo Oct 28.
 
Well said mkuu hakika umefanya Critical thinking. Huu udhalimu wa kutoheshimu katiba ni Udikteta wa Magufuli.

Amefanya unyama mwingi hadi anaomba kura kwa Kupiga Magoti. Mbingu na Ardhi vyote vimemkataa, Hawezi kuwa Rais tena.

CCM ikifanyiwa Udikteta huo baada ya kutoka madarakani ni kifo cha Mende Ndembendembe. Kutatokea lawama na mpasuko mkubwa wa chama, watamtafuta mchawi hadi kifo CCM hakiwezi kujenga hojakufanya harakati kushindana kwa Amani nk.

Wameishi maisha ya kubebwa kupendelewa.

Wazungu wameamua kusimamia haki Tanzania.
 
Kwel wewe ni zumbukuku
Ni upunguani kuifananisha chama cha Mbowe na CCM.Chama cha vibaraka wa mabeberu ni cha kuogopwa kama ukoma. Chama saccos, mtaishia kuona ikulu kwenye TV tu pale Ufipa mkiwa na faru John wenu mkononi. Ni kipogo cha kutosha hiyo Oct 28.
 
"Mkuki kwa nguruwe,kwa mwanadamu ni mchungu.' waswahili ,Watanzania wenzangu tutumie fursa hii Lissu abadili hatima ya taifa letu.
 
CCM tangu mwanzo hawakuandaliwa kuwa wapinzani wamezoea kushika dola wakiachia dola ndo kifo chao chama cha Upinzani kitakuwa chaumma tu hapa😂😂😂😂
 
CCM itakufa; uwepo wa CCM sasa hivi unasababishwa na nguvu ya dola sio uungwaji mkono na wananchi, siku ikiondoka madarakani na dola ikaondoka upande wao, CCM kama chama cha siasa Tanzania kitakufa rasmi.
 
CCM tangu mwanzo hawakuandaliwa kuwa wapinzani wamezoea kushika dola wakiachia dola ndo kifo chao chama cha Upinzani kitakuwa chaumma tu hapa😂😂😂😂
NCCR ndio wapinzani wa kweli kuliko, Chadema mabwabwa Wali nazi mawakala wa mabeberu wa Ubelgiji..
 
CCM itakufa; uwepo wa CCM sasa hivi unasababishwa na nguvu ya dola sio uungwaji mkono na wananchi, siku ikiondoka madarakani na dola ikaondoka upande wao, CCM kama chama cha siasa Tanzania kitakufa rasmi.
tangia 2010 CCM inabebwa na vyombo vya dola
 
CCM tangu mwanzo hawakuandaliwa kuwa wapinzani wamezoea kushika dola wakiachia dola ndo kifo chao chama cha Upinzani kitakuwa chaumma tu hapa😂😂😂😂
na ndo ukweli ,hizi mali zote za CCM kama viwanja na miradi zikitaifishwa sijui watatoa hela wapi ya kuendesha chama
 
Inategemea CHADEMA itachukua dollar ngapi? 10 au 5 ila exchange rate iko 2315 leo
 
Back
Top Bottom