Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 46,991
- 144,323
Kwa upande wa Watumshi wa Umma,Bajeti hii iliopita jana inamanisha jambo moja kubwa sana kwao nalo ni kubaki na mshahara ule ule wa tangu mwaka wa fedha wa 2015/2016 ulioanza July, 2015 na mshahara huo wataenda nao mpaka mwaka wa fedha wa 2021/2022(July 2021) hapa ikamanisha watakaa kwa kipindi cha miaka 6 na mshahara ule ule, na asipongeza tena hiyo July, 2021 iwapo CCM itarudi madarakani, maana yake watakaa kwa miaka 7 mpaka July, 2022 katika mwaka wa fedha wa 2022/2023.
Hakika hii ni hatari, na hili jambo lina madhara makubwa sana kwa watumishi, na madhara haya yatagusa mpaka mafao yao kwani mshahara mtu anaostaafu nao, ndio hutumika katika kukokotoa mafao yake(nijuavyo mimi); hivyo, athari za kutopandisha mishahara ya watumishi wa umma kwa miaka hii 6, itagusa kila mtumishi alieko katika utumishi wa umma leo hii hata kama bado ana miaka 10 au 20 ya kuendelea kuwa kazini unless utaratibu wa kukokokotoa mafao utakuja badilishwa huko mbeleni.
Kuirudisha CCM madarakani,hasa hii ya Magufuli, itakuwa ni kosa kubwa sana la kuendeleza unyanyasaji huu wa watumishi wa umma.