Ivi pro ndulu wa bot huoni kama uliwapotosha watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ivi pro ndulu wa bot huoni kama uliwapotosha watanzania

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Tabutupu, Jan 16, 2012.

 1. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,650
  Likes Received: 4,411
  Trophy Points: 280
  GAVANA wa Benki kuu ya Tanzania (BoT)Prof Benno Ndulu, amewahi kuzungumzia ubora wa noti mpya zilizotolewa mwaka jana .

  Katika mkutano wake na waandishi wa habari leo, Gavana Ndulu alisema noti mpya zina ubora na viwango vya kimataifa.

  Akifuatana na wataalamu wake wa ndani na mmoja kutoka kampuni iliyotengeneza noti hizo, Gavana Ndulu aliwahakikishia Watanzania kwamba hawatapata hasara na wala uchumi hautaathiriwa na noti mpya zilizotolewa


  Mtaalamu huyo kutoka kampuni ya Crane Currency ya Sweden, Peter Brown, alitoa mifano ya noti mbalimbali ikiwamo Dola za Marekani zilivyo na ubora unaofanana na noti mpya za Tanzania katika ubora.


  Hivi hizi note mpya ambazo huyu msomi alikuwa anazitetea na kusema zina ubora kama dolla za US na zina ubora wa kimataifa, haoni kama aliwapotosha na kuwadanganya wa tz watanzania.


   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Like father(JK) like son(Ndulu). Ndulu ni alama ya utawala wa JK
   
 3. H

  Huihui2 JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Huyu Prof Ndullu si ndiyo anasema inflation ni 20% wakati katika real sense ipo kwenye 40%- 55%. Naanza kupata wasiwasi juu ya umahiri wake kiuongozi bila kujali uwezo wake ki- akademia
   
 4. L

  LATTICE BOND JF-Expert Member

  #4
  Jan 16, 2012
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo watanzania tukisikia mtu fulani ni Professor au Dr. basi tunajiridhisha bila shaka yeyote kuwa huyo mtu ni bora sana!!!
  Ki ukweli wingi wa madarasa kichwani si sababu ya mtu kuwa na maamuzi mazuri!!
   
 5. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #5
  Jan 16, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,117
  Trophy Points: 280
  wakuu ni sahihi kabisa kwa anacho ongelea mtoa maada,

  ILA NAOMBA TUJE KWENYE UPANDE WA PILI WA SHILINGI, TUNAKUWA TUNACOMPLEIN SANA KUHUSU NOT PYA

  - Je utunzaji wa Not zetu unaeleweka? je ni kwa nin fedha zote za nje ukizikunja kunja ukienda kuzibadilisha hawazikubali?

  - Tumekuwa tunatunza fedha vibaya sana, mtu anakunja Noti kam sigara theni anaiweka mfukoni unategemea nini?

  - Cheki wakinamama sokoni, wanakunjakunja na kufunga na kanga.

  - Huwezi kunjakunja Dolla ya marekani wa pound ya Uingereza halafu utegemee ipokelewe dukani.

  MIMI NAZANI NA SISI TUJIFUNZE KUTUNZA FEDHA ZETU KWA USTARABU THENI NDO TULALAMIKE
   
 6. n

  namimih Member

  #6
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Nakubaliana sana na maoni yako kuhusu utunzaji wa noti, na pamoja na mifano kuhusu mama ntilie na wengineo ambao wanakuwa na haraka ya kuharibu noti zetu kwa kuzihifadhi haraka haraka kuliko kuzitunza kwa kuziweka taratibu, lakini inawezekana suala la usalama ambayo tayari inakuwa mada nyingine, au inaweza kuchelewa kuhudumia wateja, lakini pamoja na sababu zote nzuri kuhusu utunzaji ile sababu ya Prof.Ndullu kuwa ubora wa noti unapimwa kwa kuchuja rangi bado haiingii akilini. Nawakilisha
   
 7. Tabutupu

  Tabutupu JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 5,650
  Likes Received: 4,411
  Trophy Points: 280
  Ni sawa mkuu ,utunzaji ni kitu muhimu sana lakini kwa kesi hii hoja yako haina mashiko sana , unajua kwanini.
  Ukishika fedha ya Mkapa unajisikia umeshika kitu, lakini pesa ya JK na Ndulu naona kama nadanganywa. Mie binafsi napenda nipewe ile pesa ya Mkapa ni nzuri, ngumu, ina rangi nzuri, haichakai haraka, unakaa vizuri kwenye wallet etc.
   
 8. TheChoji

  TheChoji JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2012
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 672
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  Hivi ule mpango wa kuondoa noti za zamani kwene mzunguko uliishia wapi?
   
 9. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,137
  Likes Received: 2,172
  Trophy Points: 280
  Bado tunaendelea kutumia Noti za aina mbili hadi 2015? niadhani ni nchi pekee inayotumia mfumo huu...
   
 10. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #10
  Jan 17, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  ndullu ni muongo wa kutupwa....hafanyi kazi kwa kutumia weledi anatumia siasa kila wakati.....
   
 11. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,223
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280

  Nadhani bado wanatafakari iwapo waziondoe ama la, kwa sababu mpya zina viwango duni
   
 12. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #12
  Jan 17, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,137
  Likes Received: 2,172
  Trophy Points: 280
  wizi mtupu
   
 13. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #13
  Jan 17, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  mtoa mada umezingua kuhusu utunzaji wa noti.
  Pamoja na kuwa tunatunza noti vibaya, vipi kuhusu hizi za mwaka 2002? Ina maana watanzanzania wamebadilika ghafla na kuanza kuhifadhi noti kama ilivyo sasa hivi?
  Ukweli ni kuwa vinoti vya sasa havina ubora, suala la utunzaji ni shida kutokana na mazingira ya ufanyaji kazi. Imagine mtu kama Saddam Makuku wa Ilala Bungoni, kuku akaange yeye, wateja ahudumie yeye, na bado fedha apokee na kuzitunza vizuri? Si kila mpokea hela anakuwa amekaa mu-desk na droo lenye partition za hela.
  Ndulu ft. BoT sucks big time mazee...
   
 14. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #14
  Jan 17, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Ndullu sio mataalam wa mambo ya fedha, yeye ni mtaalam wa mambo ya usafirishaji na ndio maana alipoteuliwa ilibidi aombe aje na Dr. Massawe ambae alikuwa IMF ili aje amsaidie [ yeye alikuwa upande wa utafiti World Bank] In a nutshell mtu anaeiendesha BOT ni Massawe na Ndullu ni boya tu!!!
   
Loading...