Wana Jf jana ktk ukumbi wa kiss club mwanza tulikuwa na mastaa kibao waliopata kutamba uko nyuma,kilichonishangaza mimi ni kuona jinsi gani walivochoka yani hadi konyagi wanagongea kwa watu kweli?hapa nawazungumzia steve nyerere,dudubaya,jitaman na darkmaster.ila mimi nilistuka zaidi nilipomuona dudubaya alivyo nikajiuliza ivi huyu ndo dudu yule wa nampenda mpenzi wimbo uliopata kutamba na kumuingizia mkwanja mrefu na je dudubaya hizo pesa alizitumia kuwekeza kwenye nini?pia nilijiuliza sasa ndo kaamua kuamia mwanza au baada ya maisha ya dar kumuendea hali jojo?Ila nisingependa kuponda sana kwani hayo yalikuwa ni mawazo yangu tu ila mwenye information zaidi juu ya miradi ya dudubaya dar.es salaam anijuze ili nijue kwani hali yake ni mbaya sana.nawasilisha.